Viongozi walioshindwa kuweka sera nzuri wanaishi kwa mihemko na miluzi kama mbwa

Viongozi walioshindwa kuweka sera nzuri wanaishi kwa mihemko na miluzi kama mbwa

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Kuna kiongozi mmoja naye pia ni member humu Jamiiforums. Watu walimwona kama kiongozi makini tangu awamu iliyopita na sasa pia.

Mimi nakwenda naye kinyume, hafai. Kiongozi yeyote anayesubiri aone nini kinatembea kwenye mitandao ndipo afanye kazi yake namfananisha na mtoto mdogo ambaye hajui la kufanya, atafanya lile analosikumwa na wazazi au jamii tu. Kiongozi wa namna hii hajui kuwa uimara wa taasisi au wizara ni upangaji na usimamizi wa sera bora.

Sera zenyewe hatuzuoni , zimeishia kuhifadhiwa kwenye makabati ya wizara HQ na kilichobaki ni kufuata mashinikizo ya vijana wa mitandaoni.

Leo ukiambiwa mweke ndani Anko T unafanya, mwoji mwijaku unamwoji.

Likitokea tukio online la unyanyasaji ndipo mtu anapita na huo upepo kupata kiki.

Haupaswi kushughulikia jambo moja moja, jamii ina matatizo maelfu kwa maelfu, hayo mawili matatu unayochukulia kiki kwa kuyaona mitandaoni ni kapicha tu.

Mna bajeti, mna nguvukazi. Tumieni mitandao ya kijamii kuelimisha, kuwakutanisha jamii pamoja. Sometimes vijana waache viti ofisini watoke mitaani wacheze na watoto, wawafundishe namna ya kukabiliana na unyanyasaji.

Ifanye jamii kuwa rafiki kwa jamii.

Mtaishi kwa kiki za mitandaoni miaka 5 , utakuja uchaguzi mwingine mtapita mtateuliwa tena mtaishi tena kwa kiki.

Matatizo ya jamii yatabaki pale pale.
Kama Anko T au mtu yeyote amevunja katiba vyombo vya Dola vipo vimshughulikie. Nyie jengeni jamii imara.
 
Itoshe kusema huna akili kama unaona anayofanya huyo anko T ni sahihi
 
Itoshe kusema huna akili kama unaona anayofanya huyo anko T ni sahihi
kama mtu kavunja katiba ni jukumu la polisi na vyombo vingine vya Dola kushughulikia na si wizara. Wizara kazi yake ni kuweka ustawi endelevu na si kufanya kazi za zimamoto za kuparamia mambo
 
Ingekuwa busara kama ungeishauri hiyo wizara ifanye nini? Hakuna anayejua kila kitu na pengine wakawa na mipango bora ambayo ipo katika mchakato kwajili na kushughulikia hiyo kero.

Pamoja na kwamba una dukuduku lakini umetumia maneno makali sana. Ukumbuke huyu ni mzazi na ni binadamu.

Haya uliyoyafanya ndio tunaita ukatili wa kijinsia. Taifa bora linaendeshwa kwa kuzingatia usawa, haki na kuheshimiana. Pengune waweza kuwa mkubwa kuliko mlengwa, lakini heshimu watu, heshimu mamlaka. Asante.
 
kwa namna moja ama nyingine upo sawa mkuu
 
Back
Top Bottom