Kuna kiongozi mmoja naye pia ni member humu Jamiiforums. Watu walimwona kama kiongozi makini tangu awamu iliyopita na sasa pia.
Mimi nakwenda naye kinyume, hafai. Kiongozi yeyote anayesubiri aone nini kinatembea kwenye mitandao ndipo afanye kazi yake namfananisha na mtoto mdogo ambaye hajui la kufanya, atafanya lile analosikumwa na wazazi au jamii tu. Kiongozi wa namna hii hajui kuwa uimara wa taasisi au wizara ni upangaji na usimamizi wa sera bora.
Sera zenyewe hatuzuoni , zimeishia kuhifadhiwa kwenye makabati ya wizara HQ na kilichobaki ni kufuata mashinikizo ya vijana wa mitandaoni.
Leo ukiambiwa mweke ndani Anko T unafanya, mwoji mwijaku unamwoji.
Likitokea tukio online la unyanyasaji ndipo mtu anapita na huo upepo kupata kiki.
Haupaswi kushughulikia jambo moja moja, jamii ina matatizo maelfu kwa maelfu, hayo mawili matatu unayochukulia kiki kwa kuyaona mitandaoni ni kapicha tu.
Mna bajeti, mna nguvukazi. Tumieni mitandao ya kijamii kuelimisha, kuwakutanisha jamii pamoja. Sometimes vijana waache viti ofisini watoke mitaani wacheze na watoto, wawafundishe namna ya kukabiliana na unyanyasaji.
Ifanye jamii kuwa rafiki kwa jamii.
Mtaishi kwa kiki za mitandaoni miaka 5 , utakuja uchaguzi mwingine mtapita mtateuliwa tena mtaishi tena kwa kiki.
Matatizo ya jamii yatabaki pale pale.
Kama Anko T au mtu yeyote amevunja katiba vyombo vya Dola vipo vimshughulikie. Nyie jengeni jamii imara.