Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Serikali kupitia halmashauri zake imekuwa ikisisitiza sana suala la usafi wa mazingira mitaani, na hata kufunga biashara ikiwemo maduka kwa saa kadhaa kwa kinachodaiwa kuwa ni siku ya usafi hivyo kila Mwananchi aingie mtaani kufanya usafi.
Kuna ugumu gani Wananchi wangewezeshwa kwa kuwekewa mapipa maalumu ya Kutupa taka kando ya barabara kila baada ya Mita kadhaa nchini kote.?
Hii ingesaidia sana kufanya mikoa na Majiji yote kuwa safi kwa kuwa wananchi hawatotupa taka ovyo na taratibu baada ya muda watakuwa wameelimika matumizi ya mapipa hayo ya taka
Viongozi wetu wamekuwa sio viongozi wakuacha Alama kwa kujiongeza bali kufuata mkumbo kwa kutoa matamko tu kwa wananchi bila kuangalia namna ya kuboresha na Kumsaidia Mwananchi.
Viongozi wa leo anachojua akiteuliwa tu basi kazi yake ni kutoa matamko /Amri ambayo wananchi wanatakiwa kafuata . Lakini sio kujivika mzigo wa yeye kuwa kiongozi kwa kufanya Mageuzi chanya bali Wamekuwa bendera fata upepo.
Nchi za Africa nyingi zimekuwa maskini kutokana na aina ya viongozi tulio nao leo.