Viongozi Wastaafu, Mfateni Rais Samia na Msaidieni Kuituliza Nchi. Mambo Yamekuwa mambo huko ulimwenguni

Vyovyote usemavyo Nchi ya Tanzania iko mikono salama chini ya Samia, kiuchumi na kiusalama. Tusonge mbele, nyie wengine jipangeni tu kumtembelea Segerea kumpelekea sabuni na mikate
Inatakiwa hata hiyo mikate na sabuni mzuie. Lakini NRNE.
 
Unataka Watukanwe na Mchengerwa?
 
Hawatakuelewa! Fisiemu ni wapuuzi sana!
 
Mzanzibar ana hasara gani, akimaliza kuiba mali anaenda kwao Zanzibar mnabaki na sifa mbaya nyie
Hao mnaita Wazanzibar wamekuwa wanakuza uchumi vizuri sana na ku improve hali ya maisha kwa kiasi kikubwa.

Mzee Ruksa alifanya kazi tukufu, hata huyu mnayembeza ila baada ya kutoka mtazikubali takwimu zake
 
Hao mnaita Wazanzibar wamekuwa wanakuza uchumi vizuri sana na ku improve hali ya maisha kwa kiasi kikubwa.

Mzee Ruksa alifanya kazi tukufu, hata huyu mnayembeza ila baada ya kutoka mtazikubali takwimu zake
Mzee Ruksa alikuwa hovyo sana alisema Kila kitu Ruksa, wa kwake anasema Kila mtu ale kwa urefu wa???
 
Mzee Ruksa alikuwa hovyo sana alisema Kila kitu Ruksa, wa kwake anasema Kila mtu ale kwa urefu wa???
Kwa umri wangu nilikuwapo Dar es Salaam mwaka 1982-84 wakati wa kipindi cha maduka ya kaya. Hicho ndiyo kipindi tulikuwa tunapanga foleni ya sukari, mchele nk. Mzee Ali Hassan Mwinyi akaingia mwaka 1985 akafanya soko huria la biashara. Kwamba kila mwenye mtaji alete biashara yeyote kwa kufuata sheria.

Ndiyo ikawa mwisho wa maduka ya kaya na kuvaa sulfate badala ya nguo na biashara ya mitumba ikashamiri. Hali iliendelea kuboreshwa kadri miaka ilivyokwenda mbele na BWM naye akapokea kijiti akaendeleza.

Ukiniambia Mwinyi alikuwa wa HOVYO then naona mahali instability kuwapo ni Mirembe hospital kuangaliwa afya ya akili
 
Maoni: Tuungane Kuitetea Tanzania Yetu – Sauti ya Haki, Maridhiano, na Busara

Nimesoma makala hii kwa umakini na hisia nzito, na siwezi kukaa kimya bila kuunga mkono kila neno lililoandikwa. Ni kweli kabisa—taifa letu Tanzania linapitia kipindi kigumu, na haitaji kejeli wala uzembe wa kifikra, bali sauti ya hekima, ujasiri, na uwajibikaji wa kizalendo.

Hatima ya Taifa Haitaki Kunyamaza

Tunapoona hali ya kisiasa inazidi kuwa ya taharuki—kwa kukamatwa kwa viongozi wa kisiasa, kwa kuendelea kwa ukandamizaji wa haki ya kutoa maoni, na kwa kuongezeka kwa jicho la dunia kututazama kwa wasiwasi—ni wazi kuwa jambo la msingi limepotea katika uongozi wa sasa: utambuzi kuwa mamlaka ya dola ni dhamana ya wananchi. Sauti ya mwananchi si tishio—ni dira. Kukosoa si uasi—ni uzalendo wa kweli.

Viongozi Wastaafu Wana Nafasi ya Kipekee

Mwandishi ametamka jambo la msingi sana: viongozi wastaafu wana nafasi ya pekee, si kama watawala wa zamani tu, bali kama walezi wa taifa. Hawa ni watu waliopitia misukosuko ya historia ya nchi yetu, waliosimamia vipindi vigumu, na waliobeba matumaini ya mamilioni. Ni wao, zaidi ya mtu mwingine yeyote, wanaoweza kumshauri Rais Samia kwa lugha ya busara isiyo na hofu, kwa lengo la kulinda heshima ya taifa letu.

Tusipofanya Mabadiliko Sasa, Tutalazimika Kujitetea Kesho

Mwandishi ameeleza wazi: kuendelea kutawala kwa mabavu ni kujiharibia mustakabali wa kidiplomasia, wa uwekezaji, na hata wa mshikamano wa kitaifa. Tundu Lissu hakuwa na bunduki. Alikuwa na hoja. Alikuwa na sauti. Alikuwa na matumaini ya mamilioni waliodai mabadiliko kwa njia ya amani. Kumweka ndani kwa sababu hiyo si tu udhalilishaji wa haki—ni uthibitisho wa hofu ya mfumo unaoogopa uwajibikaji.

Watanzania Tusiogope: Haki Haitolewi kwa Hiari, Inadaiwa kwa Umoja

Tusiendelee kuishi kwa hofu iliyozoeleka. Tusiwe watu wa kusema, “mimi natafuta hela, sihusiki na siasa.” Maamuzi ya kisiasa yanaamua kodi yako, biashara yako, elimu ya mtoto wako, na hata usalama wa familia yako. Ukiyakwepa leo, utateseka kimya kesho. Tuwe na ujasiri wa kuunga mkono sauti zinazotaka mabadiliko ya msingi. Tuwe mabalozi wa maridhiano, wa haki, na wa katiba mpya.

Hitimisho: Tunahitaji Taifa Linalosikiliza, Si Linalonyamazisha

Naunga mkono mwito kwa Rais Samia Suluhu Hassan: chagua busara kuliko mabavu. Chagua maridhiano badala ya taharuki. Sikia kilio cha Watanzania—si kwa kuwa umedhulumiwa binafsi, bali kwa kuwa wewe ndiye kiongozi mkuu wa taifa hili. Na kwa viongozi wetu wastaafu, tafadhali, simameni tena—si kwa ajili ya madaraka, bali kwa ajili ya heshima ya Taifa letu.

Mwacheni Lissu. Mfungulieni Tanzania njia ya haki, maridhiano, na matumaini.

#NoReformNoElection ✊🏾 #KatibaMpyaSasa 📢 #TumeHuru 🗳️
 
Umemtaja Warioba hivi unajua aliyemnasa vinao warioba ni mkuu wa mkoa ? Je uongozi huu unaheshimu viongozi wastaafu ? Haya maswala ya kuishi na Upinzani walitakiwa wamuite Kikwete wamshauri maana ndiye Rais pekee aliyeishi vizuri na upinzani. Maana hadi Mbowe alimwita hamnazo na hakufanywa kitu.
 
Hao mnaita Wazanzibar wamekuwa wanakuza uchumi vizuri sana na ku improve hali ya maisha kwa kiasi kikubwa.

Mzee Ruksa alifanya kazi tukufu, hata huyu mnayembeza ila baada ya kutoka mtazikubali takwimu zake
Kuna tofauti kubwa kati ya kukuza uchumi na kukuza rushwa
 
Hoja inamashiko, ila kwa jinsi nchi inavyokwenda hakuna Anaetaka hili. Na wananchi wamezidi kuijua serijaki yao vizuri zaidi na mstaksbali wa nchi unajichora vema kabisa. Majuto ni mjukuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…