Kiwalani finest
Senior Member
- Jul 6, 2024
- 116
- 85
Viongozi watokanao na rushwa hutegemea nguvu ya fedha — haijalishi fedha ni za haramu au za halali.
Nakumbuka Aprili 2019, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati huo akiwa Makamu wa Rais, alisema:
Katiba yetu ya CCM ya mwaka 1977, Ibara ya 5(4), inataka tuwaenzi waasisi wa taifa. Waasisi wetu walipiga vita rushwa huku wakisisitiza kuifuata katiba kwa uadilifu na uaminifu.
Tumekwama wapi mpaka tunaogopana kuwajibishana?
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema Aprili 2019:
Nakumbuka tarehe 05/04/2025, Prof. Ibrahim Khamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania, akiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Jengo la Mahakama Dodoma, alisema:
Aprili 2019, Mheshimiwa Samia alisema:
Watia nia wengi hutumia njaa za muda mrefu za wajumbe na baadhi ya viongozi kama njia ya kupenya kuwa viongozi. Baadaye, hulipa fadhila kwa rushwa na kuwanyamazisha maskini kwa matumaini hewa.
Kimsingi, kila kiongozi akiwa na uadilifu na akaacha usanii, kila kitu kitaenda sawa. Tatizo ni watu kukufuru kupita hata Firauni. Hawana hofu ya Mungu, wanafanya kazi za uongozi kana kwamba hawakuapa.
Wanajisogeza kwa viongozi wa dini ili waonekane waumini, lakini hawasikilizi hata maneno ya hao viongozi wa dini.
Hapa ndipo walipofaulu kuwahadaa wanajamii wasiopambanua maana ya Ibara ya 8(1)(a)(b)(c)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 (toleo la 2005), hivyo kushindwa kutumia Ibara ya 26(1)(2) kuwawajibisha viongozi wasiotimiza wajibu.
Aprili 2019, Mheshimiwa Samia alisema katika kongamano la kumuenzi Karume:
Tusome Katiba ya CCM 1977 toleo la 2022, Ibara ya 5(4), na tuiishi kwa vitendo.
Tarehe 12/07/2021, Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka akiwa Rungwe alisema:
Laiti maneno haya yangetekelezwa, vilio vya walala hoi vingeisha. Lakini leo hii, wenye nacho wanalindana kwenye maovu huku maskini wakipewa matumaini yasiyo na mashiko.
Maskini hubaki maskini, na mwenye nacho hulindwa hata anapokanyaga katiba.
Aprili 2019, Mheshimiwa Samia alisema:
Tunataka kuona walio lalamikiwa wanachukuliwa hatua kwa kuzingatia Ibara ya 8(1)(a)(b)(c)(d), na wananchi wapewe mrejesho wa hatua hizo bila dharau.
Tuna jukumu la kumsaidia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzingatia Katiba ya nchi Ibara ya 35(1).
Tarehe 28/03/2025, Prof. Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, akiwa kwenye maombi ya Lailatul Qadr alisema:
Nikashtuka ndotoni, katika ulimwengu wa kiroho, huku nikisema:"Twendeni tu, Mwenyezi Mungu yupo na anaona."
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
— Mathias Mugerwa Kahinga

"Nimefundishwa na Karume, ninalo liona silo niseme, na nitasema."Mwisho wa kunukuu
Katiba yetu ya CCM ya mwaka 1977, Ibara ya 5(4), inataka tuwaenzi waasisi wa taifa. Waasisi wetu walipiga vita rushwa huku wakisisitiza kuifuata katiba kwa uadilifu na uaminifu.
Tumekwama wapi mpaka tunaogopana kuwajibishana?
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema Aprili 2019:
"Hotuba za Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, ukizisikiliza, utahisi moyoni kama yupo hai. Sasa tujiulize, yale tunayoyafanya leo ndiyo aliyoyazungumza miaka hiyo?"Mwisho wa kunukuu
Nakumbuka tarehe 05/04/2025, Prof. Ibrahim Khamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania, akiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa Jengo la Mahakama Dodoma, alisema:
"Kulikuwa na Jaji mmoja aliyejulikana kama Jaji mwenye kanzu nyekundu. Alikuwa wa kwanza kuleta huduma za Mahakama Kuu akitumia reli. Alisema anayeshika mfuko wa fedha ndiye mwenye maamuzi."Mwisho wa kunukuu
Aprili 2019, Mheshimiwa Samia alisema:
"Tutizameni tunayoyafanya leo: ni uzushi mwanzo mwisho, ni uongo mwanzo mwisho."Mwisho wa kunukuu
Watia nia wengi hutumia njaa za muda mrefu za wajumbe na baadhi ya viongozi kama njia ya kupenya kuwa viongozi. Baadaye, hulipa fadhila kwa rushwa na kuwanyamazisha maskini kwa matumaini hewa.
Kimsingi, kila kiongozi akiwa na uadilifu na akaacha usanii, kila kitu kitaenda sawa. Tatizo ni watu kukufuru kupita hata Firauni. Hawana hofu ya Mungu, wanafanya kazi za uongozi kana kwamba hawakuapa.
Wanajisogeza kwa viongozi wa dini ili waonekane waumini, lakini hawasikilizi hata maneno ya hao viongozi wa dini.
Hapa ndipo walipofaulu kuwahadaa wanajamii wasiopambanua maana ya Ibara ya 8(1)(a)(b)(c)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 (toleo la 2005), hivyo kushindwa kutumia Ibara ya 26(1)(2) kuwawajibisha viongozi wasiotimiza wajibu.
Aprili 2019, Mheshimiwa Samia alisema katika kongamano la kumuenzi Karume:
"Mzee wetu, Hayati Karume, na Baba wa Taifa walituambia rushwa ni adui wa haki na walikuwa wakilalamikia rushwa katika hotuba zao nyingi."Mwisho wa kunukuu
Tusome Katiba ya CCM 1977 toleo la 2022, Ibara ya 5(4), na tuiishi kwa vitendo.
Tarehe 12/07/2021, Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka akiwa Rungwe alisema:
"Mawaziri, Makatibu Wakuu, washuke mpaka vijijini waone uhalisia. Wasikilize changamoto na wamsaidie Mheshimiwa Rais vyema.""Heshimuni sheria na katiba ya nchi. Msiwe kikwazo kwa utekelezaji wa sheria. Serikali ikitunga sheria, ina nia njema kwa wananchi.""Chama cha Mapinduzi hakitavumilia vitendo vya uvunjifu wa sheria na katiba."Mwisho wa kunukuu
Laiti maneno haya yangetekelezwa, vilio vya walala hoi vingeisha. Lakini leo hii, wenye nacho wanalindana kwenye maovu huku maskini wakipewa matumaini yasiyo na mashiko.
Maskini hubaki maskini, na mwenye nacho hulindwa hata anapokanyaga katiba.
Aprili 2019, Mheshimiwa Samia alisema:
"Baada ya kukalia kiti, wewe ndiye wa kwanza kuchukua ardhi za watu. Je, si sisi tunao dhulumu haki za wananchi? Mzee wetu Hayati Karume alitufundisha tukipata cheo, tuwatumikie watu na tusimamie haki zao."Mwisho wa kunukuu
Tunataka kuona walio lalamikiwa wanachukuliwa hatua kwa kuzingatia Ibara ya 8(1)(a)(b)(c)(d), na wananchi wapewe mrejesho wa hatua hizo bila dharau.
Tuna jukumu la kumsaidia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzingatia Katiba ya nchi Ibara ya 35(1).
Tarehe 28/03/2025, Prof. Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, akiwa kwenye maombi ya Lailatul Qadr alisema:
"Mtu mwenye akili akiona ishara kidogo tu, tayari ameishaelewa."Mwisho wa kunukuu