Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
- Thread starter
- #41
nani atashawishika na mawazo ya hovyo hovyo ambayo tena ni mihemko tu isiyo mbadala dhidi ya chochote ambacho ni changamoto?🤣Fikra mbadala na mawazo mapya ni kuwa na jamii inayoheshimu misimamo ya Vyama vingine vya Siasa bila kujali kuwa ni chama tawala au upinzani.Kuwa na Katiba bora inayotambua Vyama Vyote vya Siasa na kuvilinda pia kuvipa nguvu sawa bila kujali ni chama tawala au upinzani.Bila kunzigatia misingi ya Ujamaa na Kujitegemea pamoja na kuheshimu Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 basi tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu maana zama hizi za giza ili uwe kiongozi basi unatakiwa uwe mwanaccm jambo ambalo ni upumbavu uliopitiliza.Uongozi unatokana na mtazamo wa mtu na fikra zake na jinsi jamii wanavyokubaliana naye na siyo shinikizo kutoka kwenye chombo chochote cha nchi(Serikali,Bunge na Mahakama) kwani kukiwa hivyo basi maadili na sifa za viongozi wa nchi hayapo kabisa.
Mwisho ni kuishi kwa kulipana fadhila huku sehemu kubwa ya Wananchi wakiishi kama hawapo kwenye nchi yao.Kupoka haki za raia wengine kwa sababu ya kuendekeza uchama na dola kusimamia hilo kumesababisha hali ya kutoaminiana na upendo wa wengi umepungua.Vile vile machawa na makupe wamezaliwa ili waendelee kuinyonya nchi vizuri na kunufaisha familia zao bila kufanya kazi za ujenzi wa Taifa.Mungu alinusuru hili Taifa maana wapumbavu wanaongezeka kila siku kwa sababu ya maslahi kutoka ccm.
misimamo ya vyama vyenu bakini nayo ndani ya vyama vyenu. Yaani ajitokeze kiongozi tu kwasababu ya kuchochewa na ulevi na mihemko yake tu ndio uje kubabaisha watu walioko makazini? alaa?
Jamii imekukataa wewe, chama chako na fikra zako potofu, unalazimisha? wananchi wamekutaa unailaumiu CCM, bunge au mahakama? Vina hudikaje sasa kwa mfano? uko timamu kweli?🤣
Taifa hili liko kwenye ulinzi na mikono salama ya Mwenyezi Mungu. Na hata vitabu vya Mungu vinasema, malaka zote za dunia zimetoka kwa Mungu.
Na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu..
Na kwasababu hiyo viongozi wazuri wako CCM hata ukinuna shauri yako 🐒