Viongozi wetu hata sijui ni nani aliyewaloga

Viongozi wetu hata sijui ni nani aliyewaloga

cleokippo

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2014
Posts
2,149
Reaction score
1,852
Viongozi wetu hata sijui ni nani aliyewaloga

Naandika kwa masikitiko makubwa sana , nimemskia mh wazir na mbunge wa Arusha mjini akidai kwamba anataka awajengee wana Arusha msikiti wenye thamani na dola milioni 100 ambazo ni sawa na tsh zaid ya bilion 21

Sasa swali langu kwa mh wazir nchi yako inachangamoto nyingi sana ikiwemo changamoto ya madawati , maana mashuleni mpaka leo hii watoto wanakaa chini

Kuna changamoto za vitabu, zipo changamoto za vifaa tiba

Zipo changamoto pia za miundombinu ya barabara

Tena kama kwenu uko kanda ya ziwa kila kukicha wakazi wa jiji la mwanza wanalalamika kwamba barabara za mwanza mjini ni nyembamba hivyo zinasababisha msongamano

Na wewe kule ndio kwenu lakini huna hata habar napo

Ila sasa ikifika wakati wa kampen unajinadi kuwa wewe ni mtoto wa kule wakati ukiwa kwenye system unapasahau

Zipo pia changamoto nyingi tu hata hapo Arusha lakin cha kuskitisha kwa upeo wako umeona kama msikiti ndio kitu bora zaid

Inshort kama kiongozi unatakiwa ufanye kitu ambacho kitaweza kuwanufaisha majority

Ingekupendeza mh hiyo pesa ni kher ikaninua madawati , vifaa tiba au hata kiwanda ili vijana wapate ajira
 
Hizo changamoto wakizitatua watakosa cha kuwadanganya kama ahadi uchaguzi wa 2030, hvyo wameziacha kimkakati kabisa.
 
Kuna kipindi ishu ya deni la taifa lilikuwa linazungumzwa sana, samia akatoa maelekezo kwamba deni la taifa litajwe kwa dola na sio Tsh, unajua ni kwanini?

N kwa sababu, viongozi wanadhani wanaongoza wapumbavu.
 
Kwanza msikiti sio tija, nani ataenda kuswali nyakati hizi aache kufanya shughuli zake akamsikilize sheikh akibwabwa hadithi za mtume na allah wake? Mambo ya ajabu sana haya kujenga msikiti
 
Uongozi wa awamu hii wamekuja kupumzika tu
 
Wanafanya kum empress mama kwamba wanajali dini yake..upuuz mtupu..hii nchi inahitaji kijana kama traore...huu ujinga hutauskia
 
Kuna kipindi ishu ya deni la taifa lilikuwa linazungumzwa sana, samia akatoa maelekezo kwamba deni la taifa litajwe kwa dola na sio Tsh, unajua ni kwanini?

N kwa sababu, viongozi wanadhani wanaongoza wapumbavu.
Yaani wamejisahau kabisaaa😂😂😂😂😂😂😂
 
Wewe unataka watatue chanagamoto wakoswe ahadi za uchaguzi kila baada ya miaka mitano?

Halafu kujenga msikiti imekuwa nongwa kwa kila mtanganyika.
Ila angesema atajenga kanisa msingetoa mapovu.
 
Back
Top Bottom