Kuna kundi la wastaafu wasomi ambao Magufuli hakulitumia vilivyo kwani hakuthamini experience kama ni nyenzo muhimu katika kuendesha nchi; Samia alitumie kundi hili kuleta maendeleo hasa katika sehemu za ushauri kwenye bodi za wakurugenzi wa mashirika!!
Mfano mzuri nihapo ATCL. Magufuli aliwajaza watu wake aliotoka nao TANROADS kama asante ya kumsaidia kupata URAIS ili hali shirika la ndege linahitaji weledi wa hali ya juu kuliendesha. Matokeo yake ndege zikanunuliwa bila mpango na shirika likapata hasara ambayo ingeweza kuepukika hasa wakati huu wa pandemic. Kuna wataalam wa mambo ya usafirishaji [ Transport Economists] ambao wanatumiwa na taasisi za nchi za nje ambao tungeweza kuwatumia.
Rais ashauriwe kama ikiwezekana kusimamisha ununuzi wa hizo ndege nyingine ambazo marehemu alikuwa anajigamba kuwa ameziagiza kwani kwa hali ya sasa ya shirika hakuna justification ya kuongeza capacity.