Viongozi wetu ni picha halisi ya jamii yetu

Viongozi wetu ni picha halisi ya jamii yetu

Ndio inaweza onekana kauli ya kushangaza lakini ndio ukweli halisia kwa asilimia nyingi tu.

"Viongozi wetu ndio picha halisi ya jamii yetu"

Kwa asilimia kubwa viongozi wetu wanawakilisha tamaduni,malezi,tabia na fikra za watu wa jamii yetu kwa kiwango kikubwa.

Vile wafikiriavyo viongozi wetu, vile watendavyo viongozi wetu ndilo kundi kubwa la jamii yetu hufanya hivyo ni kundi dogo sana ndani ya jamii yetu lililo tofauti na tabia za wanajamii wengi ambao pia viongozi wetu wamo.

Namna walivyo viongozi wa jamii au mataifa ya wazungu ndivyo ilivyo jamii ya kizungu kufikiri,kutenda,malezi, tamaduni na mienendo.

Namna walivyo viongozi wa jamii/mataifa ya waarabu ndivyo hivyo jamii ya waarabu inavyo enenda kwa kiasi kikubwa.

Namna walivyo viongozi wa jamii au mataifa ya Asia China, Korea, Japan ndivyo walivyo watu wa jamii hiyo katika kuwaza na kutenda.

Namna walivyo viongozi wa CCM Tanzania ndivyo walivyo viongozi wa Chadema,ACT, CUF n.k na ndivyo walivyo Watanzania wengi kutenda, kunena, kufikiri, tabia, malezi, tamaduni na mfumo mzima wa kimaisha.

Vita dhidi ya hali yetu tuliyo nayo haiwezi kuwa nyepesi kwa sababu jamii yetu kubwa ipo kama walivyo wale wanao tuongoza sasa. Wenye fikra mpya,malezi tofauti, tamaduni tofauti na mfumo mzima wa maisha tofauti na jamii ni wachache sana.
Nakubaliana na wewe. Ila kuna namna ya ku-improve hili. Njia yenyewe ni kuwepo na uchaguzi huru na wa haki ambao utaleta mashindano ya viongozi kushindana. Kiongozi akishajua kuwa nikifanya vibaya nitaondolea wakati wowote nakuhakikishia ataongeza jitahada.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]ss mkuu c hawajaweka sehemu ya kutupa taka ktk majiji makubwa hvyo uwezi tembea na kopo tupu Toka sehemu Moja kwenda nyinginee .
Dustbins zipo na watu hawana utaratibu wa kuzitumia
 
Nakubaliana na wewe. Ila kuna namna ya ku-improve hili. Njia yenyewe ni kuwepo na uchaguzi huru na wa haki ambao utaleta mashindano ya viongozi kushindana. Kiongozi akishajua kuwa nikifanya vibaya nitaondolea wakati wowote nakuhakikishia ataongeza jitahada.
Kenya wanauchaguzi huru nafikiri unakubaliana nami ila kuna mataifa hata huo uchaguzi yanausikia tu ila ukicompare na wakaenya ni mbingu na ardhi.

Viongozi hawajali kuhusu muda watakao hudumu madarakani bali wanajali kuhusu mipango yao watakayo kamilisha waingiapo madarakani.

Uchaguzi huru na haki sio utatuzi wa matatizo licha ya kwamba binafsi naunga mkono uchaguzi wa huru na haki kwa sababu zangu nyingine kabisa.
 
Back
Top Bottom