Viongozi wetu wa dini tumuombe Mungu Maarifa sio Mvua

Viongozi wetu wa dini tumuombe Mungu Maarifa sio Mvua

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Sitaki kupuunza nafasi za Viongozi wa Kiimani lakini haizuii ukweli kuwa wana nafasi ya kuielimisha Jamii zaidi ya kujaribu kuficha tatizo.

Ningetamani badala ya kufanya juhudi za kuomba mvua basi Wangechagua siku moja ya ibada watoke na Waumini wapande miti ili kutibu mazingira.

Mimi naamini Mungu hakubagua ni yupi ampe maarifa yupi asimpe...hivyo naamini hata Viongozi wetu wa Imani hawajabaguliwa kupewa maarifa.

Viongozi hawa wanafahamu ni nini sababu ya mabadiliko ya tabia nchi..iwe ni kwa kujifunza kwa Wanasayansi au kujfunza kupitia Vitabu vya kiimani.

Kama tunaamini Mungu alitupatia Dunia yenye kila kitu ni kipi sasa tunataka Mugu atupatie ambacho alisahau?.

Tunachohitaji ni Maarifa tu na kutumia akili alizotujalia huyohuyo Muumba na kila kitu kitakuwa sawa...leo hata tukipata mvua nayo ikizidi tutaanza tena kuomba apunguze.

Kutumia nguvu kwa kuendesha ibada za kuomba Mvua ni kama ule usemi wetu wa "usimpe Muhitaji Samaki, mfundishe kuvua kisha umpe nyavu".

Saudi Arabia is a nation where there is no river at all. Sure, there are a few lakes here and there, underwater sources, and oasis in the desert, still it consumes double the amount of water consumed by any developing nation in the world.28 Aug 2019Saudi Arabia is a nation where there is no river at all. Sure, there are a few lakes here and there, underwater sources, and oasis in the desert, still it consumes double the amount of water consumed by any developing nation in the world.

Bongo land.png
 
Hivi dini hizi zote zisingekuwepo ingekuwaje? Maana hizi akili za kuambiwa eti Mungu yupo kwenye majengo ya makanisa na misikiti, eti huyu kiongozi wangu wa kiroho! Ooh mara mtoleeni Mungu zaka na sadaka? Mara ooh usifanye hivi utachomwa moto!

Huu ufala bakini nao wenyewe mimi simo!! Kwenye dini kuna ujinga sana hasa wale waumini wenye kushika dini sana, dini zinafanya waumini wasijue mambo mengi na hata kama wanafanyiwa manipulation wao hawana habari wanamuwaza Yesu , Mungu, Muhammad na Allah, ma star wa maandiko/ main characters
 
Wacha waendelee kuomba mvua. Bila shaka hata ndege na wanyama pori wanaomba mvua pia.

Kwani sisi na wao tuna tofauti yoyote? Sote si ni waja wake mola tu?

Hiiiiii bagosha!
 
Hivi dini hizi zote zisingekuwepo ingekuwaje? Maana hizi akili za kuambiwa eti Mungu yupo kwenye majengo ya makanisa na misikiti, eti huyu kiongozi wangu wa kiroho! Ooh mara mtoleeni Mungu zaka na sadaka? Mara ooh usifanye hivi utachomwa moto! Huu ufala bakini nao wenyewe mimi simo!! Kwenye dini kuna ujinga sana hasa wale waumini wenye kushika dini sana, dini zinafanya waumini wasijue mambo mengi na hata kama wanafanyiwa manipulation wao hawana habari wanamuwaza Yesu , Mungu, Muhammad na Allah, ma star wa maandiko/ main characters

Kuna mwingine alifukuza Corona kwa maombi ya siku 3 tu.

IMG_20211119_091739_123.jpg

Laiti angefanya wiki angetuhamishia Canaan kabisa. Kuliko na asali na maziwa tukapata kuogelea 😁😁.
 
Hivi dini hizi zote zisingekuwepo ingekuwaje? Maana hizi akili za kuambiwa eti Mungu yupo kwenye majengo ya makanisa na misikiti, eti huyu kiongozi wangu wa kiroho! Ooh mara mtoleeni Mungu zaka na sadaka? Mara ooh usifanye hivi utachomwa moto! Huu ufala bakini nao wenyewe mimi simo!! Kwenye dini kuna ujinga sana hasa wale waumini wenye kushika dini sana, dini zinafanya waumini wasijue mambo mengi na hata kama wanafanyiwa manipulation wao hawana habari wanamuwaza Yesu , Mungu, Muhammad na Allah, ma star wa maandiko/ main characters
Bora umeshtuka mapema mkuu,hakuna kitu naona ni ukichaa kuamini Kuna kiumbe nje ya mfumo wetu wa kawaida wa kibinadamu unatucontrol,hapana haiwezekani yaani hiyo Mungu yupo kwenye fikra tu za Watu ila kiuhalisia hayupo na hajawahi kuwepo,ukiwaambia wathibishe uwepo wake watapiga poyoyo weeeee na kutolea mifano vitu halisia vya hapa hapa duniani na angani kumthibitisha kiumbe aliyepo kwenye fikra zao
Yaani ni zaidi ya Wendawazimu aisee!
 
Ni ujinga tu kama ujinga mwingine.

Maombi hayasaidii chochote, ni upuuzi tu…. mvua ina sayansi yake.
 
Magaidi yamekata miti na kuleta ukame, wao wanaleta mboyoyo za maombi…. just another big joke.!
 
Bora umeshtuka mapema mkuu,hakuna kitu naona ni ukichaa kuamini Kuna kiumbe nje ya mfumo wetu wa kawaida wa kibinadamu unatucontrol,hapana haiwezekani yaani hiyo Mungu yupo kwenye fikra tu za Watu ila kiuhalisia hayupo na hajawahi kuwepo,ukiwaambia wathibishe uwepo wake watapiga poyoyo weeeee na kutolea mifano vitu halisia vya hapa hapa duniani na angani kumthibitisha kiumbe aliyepo kwenye fikra zao
Yaani ni zaidi ya Wendawazimu aisee!
Mimi sipo mbali na kuamini hivi...na nimeshapost au kuocmment mara kadhaa mijadala inayorandana na hiyo.

Ingawa kwa mtazamo wangu sioni vibaya kuwa na Mafundiso haswa yanayoelekeza matendo chanya.

Kwa mfano sioni ubaya wowote tukifundishana kwa Maandiko chanya na mifano ya Watu waliotenda mema na kuvuna mema...kwani kwa upande mwingine ni hatari kuwa na jamii isiyo na 'kioo' kitakachowaonesha kuwa kuna mema na kuna mabaya, na kuna faida za kuwa Mwema na kuna madhara ya kukosa kutendeana mema.

Na mara zote nipo kinyume kabisa na wanaotumia hizi imani na Wafuasi wao kupotosha na kuwaaminisha yasiyokuwepo...Miongoni wetu wanaibuka Wachache na kujaribu kuzitumia imani hizi hizi kujinufaisha tena kwa kuwaaminisah Waamini mambi yasiyoingi kabisa kichwani.

Hivu kw nini Dini hizi zisielimishane ya kuwa ni vibaya kukata miti hovyo, ni dhambi kutokupanda Mti kabisa hapo unapoishi...kwamba ni neema na thawabu kubwa kuhakikisha mazingira yanayokuzunguka ni ya kijani.

Badala yake tumekuwa na Wajanja wanaowaaminisha Wamini kuwa kwa kuchanga pesa na kumpa yeye basi wtapata thawabu...hakika huu ni uhuni na inapaswa kukemewa.
 
Huwezi omba mvua kwanza bila kuomba toba kwanza
 
Back
Top Bottom