Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?

nakubali ulicho kisema

nadhani ni kwa mara ya kwanza ndugai kafanya kazi yake kama spika, ya kuhoji, kukosoa na kuishauri serikali tofauti tulivyo zoeleshwa kuwa spika anatakiwa aunge mkono kila tendo la serikali
 
Umeandika hii uzi kwa sababu umeguswa sana na makosa ya Ndugai au sababu Ndugai alikutia kitanzi kwenye kamati ya maadili? wakosaji ni wengi mno but ulikua kimya kwa nini uzi kwa Ndugai?
 
Job inabidi akuombe msamaha hata wewe, alikuchimba mkwara kipindi kile!
 
Swali zuri. Zamani kulikuwa na watu wazito na wanaosikilizwa. Hao humwita mkosaji na kumshauri cha kufanya naye hakuweza kubisha.
Siku hizi sijui kama hao watu mashuhuri bado wapo, kiukweli, walitamkwa kama wazee. Tena wakosaji siku hizi pia wabishi sana, hawaogopi wazee wenye nchi.
Kukiwa na jambo Nyerere alipenda kusema na wazee kupata ithibati. Wazee walikuwa na nguvu lakini leo kila mtu anajipa nguvu.
Sasa muhimu ni kuivunja hii nguvu ya kila mtu na kuondoa woga na unafiki.
 
P kiukweli nchi hii viongozi wazalendo wapo wachache Sana wengi wao wapo kwa masilahi yao binafsi ndo Mana kujiuzulu haiwezekani.Kiongozi asie mzalendo hawezi kuwa na msimamo.
 
Kweli kabisa. Angesimama kwenye maoni yake na Kama angeshurutishwa sana angejiuzulu uspika. Hapo angejiongezea heshima hata kwa wale wanaomdharau.
Sasa heshima yee ya nn? Mwenzako anataka cake ya taifa na vieiteee. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
We unaandika nini hizi takataka
 
Kwa kiburi alichokuwanacho Ndugai na leo kawa mdogo kama piriton huyu asijiuzuru aendelee kula tu ili tufaidi sinema ya bure atakavyokuwa chawa wa Samia, maana hiyo ndio adhabu aliyopewa.

Torturing aliyofanyiwa huyo mgogo ni adhabu tosha sana kwa mtu mwenye kiburi kama yeye, na utamu zaidi leo yeye ndio ametumika kumjenga mama kimamlaka na raia wote kuanzia leo wanajuwa nini maana ya Amiri jeshi mkuu.
 
Kama spika Ndugai angechukua uamuzi wa kujiuzuru angejijengea heshima kubwa,kinyume anakanusha akidai amenukuliwa vibaya.Kimsingi matamshi yawe yamenukuliwa vibaya au yawe ndiyo maneno halisi aliyoyatamka anapaswa kupisha
 
Awajibikeee
 
TABIA ZA NDUGAI KULINGANA NA MAVAZI:

1. Akivaa Joho la Spika;

"...Huna cha kunifanya. Pambana na kitu kingine lakini sio Ndugai."

2. Akivaa Suti ya Koti na Tai:

"Mhe. Rais sisi Bunge tunakushukuru na kukupongeza kwa kutuletea pesa nyingi...Shilingi Trilioni 1.3 ni nyingi na yote inaenda kutuletea maendeleo."

3. Akivaa Shati la Kitenge;

"Hebu fikiria, juzi mama ameenda kukopa sh.1.3 Trilioni. Miaka 60 ya Uhuru tutembeze bakuli...ipo siku nchi hii itapigwa mnada."

4. Akivaa Suti ya "Kaunda:"

"Nimekosa mimi, nimekosa sana. Nimekosa mimi, Mungu anisamehe, Watanzania nisameheni."

Kwa uzoefu huu, toa Wasifu wa Ndugai.🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…