Vipers SC Vs Horoya AC | CAF Champions League | St. Mary's Stadium | 18.02.2023

Vipers SC Vs Horoya AC | CAF Champions League | St. Mary's Stadium | 18.02.2023

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Its Super Saturday!!

Ni banduka bandua katika ligi ya mabingwa Africa leo.

Vibonde wa kundi C, Vipers SC ya Uganda leo watashuka dimbani pale St. Mary's Stadium, Kitende kuwakaribisha Horoya AC.

Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza, Vipers walibugia goli 5-0 dhidi ya Raja Casablanca.

Huku Horoya AC wakiibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Simba SC.

Mashabiki wa Simba watakuwa wanaufatilia mchezo huu ili kuangalia namna gani ya kujipanga vizuri kwa mechi zinazokuja dhidi ya wapinzani hao.

Mchezo huo utapigwa saa 10:00 kwa masaa ya Africa ya Mashariki.

Mechi itakuwa mubashara kwenye chaneli 225 ya DStv.

Utabiri: Vipers 1-1 Horoya
 
Kocha wa Raja ni mate wangu tulisoma wote Lupaso sec. miaka mingi iliyopita. Huyu jamaa bwana ni mtu wa majivuni na mpenda sifa sana toka tukiwa shuleni. Ila kwa leo naona kavuka mstari eti ameniambia leo ataisambaratisha simba kama siyo wiki basi mkono.

Mimi nimembishia kwamba Raja hii hii iliyo nafasi ya 4 batola pro haiwezi mpiga mnyama wiki. Ila nimemwambia mkono inawezekana sana ikiwa watapitia kwa babu onyango
 
Its Super Saturday!!

Ni banduka bandua katika ligi ya mabingwa Africa leo.

Vibonde wa kundi C, Vipers SC ya Uganda leo watashuka dimbani pale St. Mary's Stadium, Kitende kuwakaribisha Horoya AC.

Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza, Vipers walibugia goli 5-0 dhidi ya Raja Casablanca.

Huku Horoya AC wakiibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Simba SC.

Mashabiki wa Simba watakuwa wanaufatilia mchezo huu ili kuangalia namna gani ya kujipanga vizuri kwa mechi zinazokuja dhidi ya wapinzani hao.

Mchezo huo utapigwa saa 10:00 kwa masaa ya Africa ya Mashariki.

Mechi itakuwa mubashara kwenye chaneli 225 ya DStv.

Utabiri: Vipers 1-1 Horoya
Huo ujasiri wa Simba kufuatilia game ya vipers unatoka wapi? wanakikumbuka Raja kampiga mtu hamsa, wakikimbuka kile kiugonjwa chao cha kupigwa hamsa hamsa, matumbo yanawakata kama wana amoeba.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Hii mechi inabidi Horoya apigwe sio vinginevyo hata sare haihitajiki hapa
 
Kisa tu hao Vipers wamefungwa na Waarabu, tena wakiwa ugenini! Basi na nyinyi mnajiona mna uwezo wa kuwafunga nje ndani! Ok. Time will tell.
Kwakuwa walikupiga kwenye siku zako hapo lupaso unahisi na sisi hatuwezi kumfunga kama wewe..
 
Back
Top Bottom