Vipi Gamond anafaa au bora Nabi

Vipi Gamond anafaa au bora Nabi

Hizo kauli huwa zinasemwa na Ma-mbumbumbu!

Ni wapi na lini umeona Wapenzi na mashabiki wa Klabu Bora Afrika ya Young Africans wakisema Gamondi Hafai?
Hakuna shabiki wa Yanga aliyekuwa na wasiwasi na Gamondi, Nabi alifeli miaka miwili sisi kushiriki CAF na tukamvumilia, sembuse Gamondi?
 
Imetokea tu Gamond kutokubalika na wanaofanya hayo mara nyingi huwa ni wachambuzi na mashabiki wa Simba kwa kuanzisha kitu fulani cha kumkosoa. Mara utasikia rotation mara sijui hana mbinu alibebwa na Nabi lakini huyu kocha ni mwamba haswa. Aina yake ya mpira aisee haujawahi kupigwa mbugi kubwa kiasi hiki ndani ya kikosi cha Yanga. Msimu wake wa kwanza ndani ya Yanga ila ana achieve kikubwa ndani ya Yanga kitu ambacho hakijawahi kutokea. Kuna watu wanasema kuwa timu imejengwa na Nabi, kama mnadhani ni rahisi kuchukua timu mikono mwa mtu halafu uka maintain katika performance na kufanya vizuri zaidi kimataifa basi tumuulize huyo huyo Nabi kwanini kachukua Far Rabat iliyokuwa bora na bingwa wa ligi ya Morocco lakini kaishia raundi ya kwanza tu kwa kutolewa na Etoil du Sahel inayoburuza mkia kwa sasa kwenye kundi.

Yanga ilidhulumiwa haki yao kule Ghana kwa kunyimwa goli halali kabisa ambapo Yanga kabla hata ya mechi dhidi ya Belouizdad wangekuwa inaongoza kundi. Gamondi mpaka hapa kaifanyia makubwa Yanga akishirikiana na viongozi, na wachezaji. Big up kwake
Mbungi inayopigwa sasa hivi Yanga ni zaidi ya Samba la Brazil.
 
Katika watu ambao ata afanye mazuri gani bado atasakamwa ni Gamond.

Mashabiki wa yanga wanakuambia Kwa Gamond hakuna kocha hapo, eti Gamond hana mbinu za kuivusha yanga.

Lakini ukitazama statics zinambeba sana Gamond.

Swali ni je Gamond anatosha au hatoshi.
gamondi anatosha kwa sasa,kila kocha no mzuri kwa wakati wake
 
Asiye tambua ubora wa Gamondi hajui mpira huyo jamaa ni master wa kweli big up MG..
Yanga inacheza soka safi magoli ya mipango na sio dondokela..
 
Acha umbea mtoto wa kiume, lini mashabiki wa Yanga tulimkataa Gamond? Nabi alikaa miaka miwili bila kushiriki michuano ya CAF na akavumilia, sumbuse Gamondi? Zile zilikuwa propaganda tu za mashabiki wa Simba.
Sawaaa
 
Katika watu ambao ata afanye mazuri gani bado atasakamwa ni Gamond.

Mashabiki wa yanga wanakuambia Kwa Gamond hakuna kocha hapo, eti Gamond hana mbinu za kuivusha yanga.

Lakini ukitazama statics zinambeba sana Gamond.

Swali ni je Gamond anatosha au hatoshi.
Neno ni Statistics (Takwimu). Ni wengi sana huwa wanashindwa kulitamka
 
Hizo kauli za kumsema Gamondi mlizianzisha nyie na wajomba zenu ORUMA Na JEMEDARI
 
Acha umbea mtoto wa kiume, lini mashabiki wa Yanga tulimkataa Gamond? Nabi alikaa miaka miwili bila kushiriki michuano ya CAF na akavumilia, sumbuse Gamondi? Zile zilikuwa propaganda tu za mashabiki wa Simba.
Simba hawampendi Gamondi kwasababu kawapiga 5 , na wanahofu akibaki anaeza ongeza idadi ya magoli ktk marudiano ..
 
Hizo kauli huwa zinasemwa na Ma-mbumbumbu!

Ni wapi na lini umeona Wapenzi na mashabiki wa Klabu Bora Afrika ya Young Africans wakisema Gamondi Hafai?
Ni kweli.

Sisi makolo ndo tuna tabia ya kumsakama na kumsema Gamondi.

Mtuvumilie tu watani mana tangu mtubugize lile kono la nyani hatupo sawa kisaikolojiia.
 
Back
Top Bottom