Imetokea tu Gamond kutokubalika na wanaofanya hayo mara nyingi huwa ni wachambuzi na mashabiki wa Simba kwa kuanzisha kitu fulani cha kumkosoa. Mara utasikia rotation mara sijui hana mbinu alibebwa na Nabi lakini huyu kocha ni mwamba haswa. Aina yake ya mpira aisee haujawahi kupigwa mbugi kubwa kiasi hiki ndani ya kikosi cha Yanga. Msimu wake wa kwanza ndani ya Yanga ila ana achieve kikubwa ndani ya Yanga kitu ambacho hakijawahi kutokea. Kuna watu wanasema kuwa timu imejengwa na Nabi, kama mnadhani ni rahisi kuchukua timu mikono mwa mtu halafu uka maintain katika performance na kufanya vizuri zaidi kimataifa basi tumuulize huyo huyo Nabi kwanini kachukua Far Rabat iliyokuwa bora na bingwa wa ligi ya Morocco lakini kaishia raundi ya kwanza tu kwa kutolewa na Etoil du Sahel inayoburuza mkia kwa sasa kwenye kundi.
Yanga ilidhulumiwa haki yao kule Ghana kwa kunyimwa goli halali kabisa ambapo Yanga kabla hata ya mechi dhidi ya Belouizdad wangekuwa inaongoza kundi. Gamondi mpaka hapa kaifanyia makubwa Yanga akishirikiana na viongozi, na wachezaji. Big up kwake