Vipi kuhusu hiki kibali cha kuingia mjini kwa wenye pikipiki?

MNORWAY

Member
Joined
Feb 9, 2018
Posts
33
Reaction score
16
Naomba tusaidiane kimawazo hii kodi ya kibali cha kuingia mjini kwa wenye pikipiki imewekwa kwa ajili ya kuleta maandeleo kwa Dar es Salaam au imewekwa kwa ajili ya matumbo ya watu binafsi au kumkandamiza Mwananchi?

Inawezekana vipi mtu ananunua usafiri wake kisha analipia bima, sumatra, nenda kwa usalama, ambazo zote ni kodi haitoshi anazuiwa kuingia mjini eti mpaka alipie kibali cha kuingia mjini hili limekaaje nduguzangu?
 
hii nchi ukiifikiria sana unaweza kufa siku si zako....fanya yako tu mdau na uhakikishe mkono unaenda kinywani
 
Kwani tsh mnatozwa huko mjini mkuu?
 
... kama alivyosema mdau hapo juu lengo ni ku-discourage watu kwenda mjini na pikipiki. Ni vurugu sana hawa jamaa.
Si kila anaeingia mjini na pikipiki anavurugu mkuu
 
subiri siku ambayo mheshimiwa atakuwa jimboni kwako akimwaga sera, naomba umuulize naamini atakuwa na majibu ya kutosha kuhusu suala hilo na huenda lipo kwenye ilani ya chama!!
 
Si kila anaeingia mjini na pikipiki anavurugu mkuu
... Mkuu vurugu namaanisha wingi wa vyombo; huyu kakatiza hapa, yule kule, wengine wanapita katikati ya magari kwenye foleni, vichochoro, n.k. alimradi kila mmoja awahi anapokwenda ndio vurugu zenyewe hizo. Sikumaanisha kurushiana ngumi.
 
NI UONEVU TU.

SHERIA ZISIMAMIWE TU, KWA ANAYEKWENDA KINYUME - FAINI.

SIYO KUWAZUIA WATU KUTUMIA NYENZO WALIZO NA UWEZO NAZO.
 
... tatizo sio usimamizi wa sheria tu Chief; miundombinu iliyopo nayo sio rafiki kwa bodaboda. Sijui nchi nyingine huko kukoje kuhusiana na usafiri wa bodaboda kwamba wanajichomekachomeka ovyo popote wanapotaka au wana njia zao, n.k?
 
Tuulize sie tunavyoibiwa na hao bodaboda huk mitaani mkuu...simu ikiita ukiitoa tu haipo huko mjn si ndo itakua balaa
 
hii nchi ukiifikiria sana unaweza kufa siku si zako....fanya yako tu mdau na uhakikishe mkono unaenda kinywani
Ni kweli aisee ukianza kushangaashangaa mishangao haitaisha mpaka unaingia kaburini.
Vitu vingi vimekaa upande upande tu.
 
... Mkuu vurugu namaanisha wingi wa vyombo; huyu kakatiza hapa, yule kule, wengine wanapita katikati ya magari kwenye foleni, vichochoro, n.k. alimradi kila mmoja awahi anapokwenda ndio vurugu zenyewe hizo. Sikumaanisha kurushiana ngumi.
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]eti sio kurusha ngumi.
Ila huwa tunalaumu tu upande wa serikali lakini watu wa bodaboda na wenyewe sio waelewa hii inawafanya kuwa watu wasiosaidika.
Wewe angalia hata huko nje ya mji unakuta kwenye mataa gari zimepanga foleni kusubiria mataa yaruhusu hao wanakatiza tu mbele.
 
Naomba tusaidiane kimawazo hii kodi ya kibali cha kuingia mjini kwa wenye pikipiki imewekwa kwa ajili ya kuleta maandeleo kwa Dar es Salaam au imewekwa kwa ajili ya matumbo ya watu binafsi au kumkandamiza Mwananchi?

Inawezekana vipi mtu ananunua usafiri wake kisha analipia bima, sumatra, nenda kwa usalama, ambazo zote ni kodi haitoshi anazuiwa kuingia mjini eti mpaka alipie kibali cha kuingia mjini hili limekaaje nduguzangu?
Huo ni mradi wa kueatajirisha watu fulani wa Halmashauri ya Jiji ls Dsm. Hakuna mantiki mtu amenunua usafiri wake halafu unamzuia asiende mjini wkt tayari ameshalipia kodi za aina mbalimbali. Nasikia harufu ya *ufisadi* ndani ya halmashauri ya Jiji la Dsm
 
Back
Top Bottom