Swet-R
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 5,613
- 8,082
Hatimae doto za winga wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva za kucheza soka la kulipwa Ulaya, zinakwenda kutimia baada ya dili lake na klabu ya Benfica inayoshiriki Ligi Kuu Ureno kukamilika.
Msuva kwa sasa anakipiga katika klabu ya Difaa El-Jadida ya Ligi Kuu ya Morocco iliyomsajili mwaka 2017 kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Yanga.
meneja wa mchezaji huyo Dkt. Jonas Tiboroha, alisema Msuva anatarajia kujiunga na timu hiyo Januari 2020 na kwamba makubaliano yao itamtoa kwa mkopo wa miezi sita kwenda Panathiakos ya Ugiriki. “Janauri mwakani huenda Msuva akawa katika timu ya Panathiakos, atacheza kwa mkopo wa miezi sita baada ya kusajiliwa na Benfica,” alisema Dkt Tiboroha.
Tangu amejiunga na Difaa el Jadida, Msuva amekuwa na kiwango kizuri muda hasa katika upachikaji mabao, akiwa ni msaada mkubwa kwa timu hiyo, hali iliyomfanya afukuziwe na klabu nyingi, ikiwamo Malaga ya Hispania
Sent using Jamii Forums mobile app