Vipi Msuva wazee... sababu Samatta Samatta

Vipi Msuva wazee... sababu Samatta Samatta

Hatimae doto za winga wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva za kucheza soka la kulipwa Ulaya, zinakwenda kutimia baada ya dili lake na klabu ya Benfica inayoshiriki Ligi Kuu Ureno kukamilika.

Msuva kwa sasa anakipiga katika klabu ya Difaa El-Jadida ya Ligi Kuu ya Morocco iliyomsajili mwaka 2017 kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Yanga.

meneja wa mchezaji huyo Dkt. Jonas Tiboroha, alisema Msuva anatarajia kujiunga na timu hiyo Januari 2020 na kwamba makubaliano yao itamtoa kwa mkopo wa miezi sita kwenda Panathiakos ya Ugiriki. “Janauri mwakani huenda Msuva akawa katika timu ya Panathiakos, atacheza kwa mkopo wa miezi sita baada ya kusajiliwa na Benfica,” alisema Dkt Tiboroha.

Tangu amejiunga na Difaa el Jadida, Msuva amekuwa na kiwango kizuri muda hasa katika upachikaji mabao, akiwa ni msaada mkubwa kwa timu hiyo, hali iliyomfanya afukuziwe na klabu nyingi, ikiwamo Malaga ya Hispania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini nadhani wakikuta ndivyo sivyo huwa wanarekebisha
Sio jambo rahisi hivyo hususani kwa mtu kama Msuva ambae hata ukiingia online huwezi kuona reliable data kuhusu yeye na uhamisho wake kwenda Benefica!

Labda nikujuze jambo moja!! Wikipedia ni reliable source na vile vile sio reliable source! Sio reliable source kwa sababu mengi, hususani biographies za watu zinaandikwa na watu na sio Wikipedia! Mimi mwenyewe kwa kazi zangu za Freelancer nimeshafanya projects za kuandika Wikipedia Pages.

Wikipedia inaweza kuwa ni reliable source endapo chini ya ukurasa husika kutakuwa na references! Binafsi siwezi kutumia hoja ya Wikipedia kama chini ya mada husika hakuna reference, tena kutoka reliable sources. Maana yake ni kwamba, hata kama mtu ana-edit basi anatakiwa ku-edit kwa kutumia reliable secondary source!

Mchukulie Mbwana Samatta kwa mfano, hapa chini ni orodha ya reference iliyotumika kuandika ukurasa wake!!

Samatta.png


Kinyume chake, ukiingia kwenye page kuhusu Msuva, hakuna reference hata moja!!
 
Back
Top Bottom