Kuganda kwa barafu Ni Suala la mda mfupi Kama kweli Ulaya ikikatiwa gesi ya Urusi Kama tulivyoambiwa na Pro-Russia mpaka wakatunga wimbo wa WINTER,WINTER,WINTER. Cha ajabu mpaka Sasa Ulaya haijaganda kumbe zilikuwa Propaganda za Urusi na MaPro Wake.
Pro-Russia pia walidai kwamba Wanajeshi wa Urusi wanasubili WINTER ili kuwafyeka wanajeshi wote wa Ukraine na Kuiteka KYIV eti Wanajeshi wa Urusi Ni wazoefu wa Vita msimu wa Baridi. Cha ajabu mpaka leo Bado Ukraine iko imara badala yake Mamio ya wanajeshi wa Urusi wanakaangwa na HIMARS huko kwenye Battle Field na Baridi likiwepo. Kumbe hii pia ilikuwa Propaganda za Pro-Russia.
Kuhusu Uchumi wa Urusi kuteteleka nadhani utakuwa haufuatilii Vyombo vya habari vya Urusi. Waziri wa fedha wa Urusi mwezi Desemba alikili wazi kwamba Ukuaji wa Uchumi wa Russia umepungua kutoka 4.6% mpaka 2.1% Mwaka 2022. Uuzaji wa bidhaa za Urusi nje ya Nchi umeshuka kwa 73%. Zaidi ya Mafuta ya Gesi anayouza kwa Bei ya Discount huko China na India,Hakuna bidhaa nyingine ya Urusi inayouzwa nje. Mbolea na nafaka za Urusi zinaozea kwenye Maghara.
Thamani ya Ruble kabla ya Uvamizi wa Urusi dhidi ya Dollar ya Marekani ilikuwa 1$= 68RU.Baadae Urusi ilipotishia kwamba nchi zote zitanunua Mafuta yake kwa fedha yake ya Ruble,Thanks ya Ruble ikapanda mpaka 1$=53%. Baada ya Ulaya na G7 kuweka ukomo wa Bei ya Mafuta ya Urusi kutovuka $60 kwa Pipa,Nenda kaangalie thamani ya fedha ya Urusi ipo 1$=72RU. Kwahiyo mpaka Sasa Ruble inaendelea kushuka Thamani. Ngoja tusubili Zuio la Urusi kuuzia Mafuta nchi zilizoweka ukomo wa Bei kuanza kufanya Kazi mwezi Feburuari tuone thamani ya Ruble itakuwaje.