Vipimo vya awali vya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu!

Vipimo vya awali vya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu!

Rest in peace John Pombe Magufuli.
Hongera kwa Mh Rais Samia kwa kukamata kijiti.
Mimi nikiwa muumini wa Sera na utekelezaji wa Ilani ya CCM nachelea kusema vipo vigezo muhimu vitakavyoelezea utendaji kazi wa Mh Rais Samia katika awamu ya sita ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa yale Serikali ya CCM iliyoyaahidi na kuaminiwa kuyafanya na wananchi wanyonge wa Tanzania.
Katika yote ambayo CCM iliyaahidi yapo mambo muhimu yakuzingatia ambayo yalivutia wapiga kura nikiwemo mimi.

Nitaorodhesha baadhi
1-Ukamilishaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Ujenzi wa bwawa la umeme,ujenzi wa SGR na ujenzi wa flyovers.
2-Ukamilishaji wa ujenzi na matumizi ya mji wa dodoma kama makao makuu
3-Elimu bure hadi kidato cha nne
4-Ukusanyaji wa mapato
5-Uanzishwaji wa somo la historia ya watanzania
6-Ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na hospitali za wilaya
7-Uanzishwaji wa bima ya afya kwa wote.
8-Udhibiti wa wakwepa kodi na mafisadi kwa kasi ile ile
9-Nidhamu na uwajibikaji ya watumishi wa umma
10-Uhai wa ATCL
11-Udhibiti wa rasilimali zetu

Naomba muongeze mengine ya muhimu.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Rahisi sana kusema ila ngumu sana kutekeleza hayo mambo ni pesa ndefuuu sanaaa.

Au wewe ni wale ambao wanamwachia mke elfu mbili halafu unasema, " nikute umepika wali nyama " !?
 
Rahisi sana kusema ila ngumu sana kutekeleza hayo mambo ni pesa ndefuuu sanaaa.

Au wewe ni wale ambao wanamwachia mke elfu mbili halafu unasema, " nikute umepika wali nyama " !?
mimi ndio hao mkuu na maisha yanaenda
 
Hongera mhe Rais kwa hatua ya kwanza muhimu ya uendelezaji wa mradi wa EACOP
 
Kilichokamilika ni daraja la Tanzanite ambalo halipo kwenye orodha yako ndugu mleta mada.
 
Sio lazima afanye hayo anaweza anza na bandari ya Bagamoyo...na yeye hapangiwi na ukimshauri ndio utaharibu kabisa.

Mama mpendwa nenda vile utakavyo na sio kwa matakwa ya hawa watu wasikupangie.
Bandari ya Bagamoyo nashauri isijengwe kwenye awamu hii la sivyo itakuwa ni fimbo ya wapinzani ndani ya chama chao na wapinzani wa nje watabeba Bango na kuzunguka nalo Tanzania mzima,,, akumbuke kuwa issue yao ya Bagamoyo JPM alilaani sana na watu wake wamo kwenye chama
 
Back
Top Bottom