Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Vipimo hivi vimekuwa ghari Sana na hata kupatikana kwake kuna mlolongo mrefu Kwa mujibu wa taarifa ambazo tunazisikia,na inasemwa kuwa mara nyingi wahusika wanalofanya hilo zoezi mara nyingi hawatoi majibu halisi Kwa kuhofia ndoa kuvunjika.
Kama kweli tunataka jamii ambayo itawajibika Kwa matendo yake basi kipimo hiki ni muhimu Sana katika jamii ili haki za wanandoa wenye mashaka juu ya kizazi Chao itafutiwe ufumbuzi.
Ni kweli kabisa kipimo hiki kikipatikana Kwa gharama rahisi na watu wakapewa majibu halisi hapa mwanzoni kutakuwa na sintofahamu nyingi na migogoro mingi itatokea hususani katika ndoa ambazo kuna kubambikiana watoto ambao sio WA mume husika.
Lakini lengo ni kujenga jamii ambayo huko mbele ya safari iepukane kabisa na hizi Tabia za kubambikiana watoto kiholela holela, kwasababu wanawake katika ndoa watajua sasa mume anao uwezo wa kupata kipimo hiko na kujua uhalisia WA mtoto kama ni wake au laa.
Huu utaratibu utasaidia Sana kuepushwa hizi dhuluma ambazo wanaume hukutana nazo katika Maisha ya kila siku katika ndoa zao,unalea mtoto Kwa mapenzi yote lakini mwisho wa siku na baadae Sana huko unakuja kugundua kwamba mtoto fulani si WA kwako.
Kwanza dhuluma ni Kwa Baba ambaye amebambikiwa mtoto ambaye si wake lakini pili ni Kwa mtoto kwakukosa kumjua Baba yake halisi. Kwahiyo Kwa kipimo hiki kupatikana Kwa bei nafuu na Kwa urahisi kitapunguza Sana hizi Tabia za kuleteana watoto ambao sio WA kwetu na kufanya jamii kuepukana na Tabia ambazo zinazidi kushamiri kila kukicha.
Hakika wakina mama Wana Siri nyingi Sana wamezibeba vifuani mwao,na ndio maana wahenga walisema " asili ya mtoto aijuaye ni mama". Sasa pamoja na kipaji Kikubwa walicho nacho cha kutunza hizo Siri basi ifikie kipindi tuwaambie hapana mama zetu na dada zetu mmeshatuumiza vya kutosha,na sasa kilichobaki ni mwendo WA vipimo Kwa kwenda mbele Kwa wale ambao Wana mashaka na kizazi Chao.
Hii imenikumbusha story moja ya kweli ilitokea huko Mombasa,Baba alienda Uingereza kutafuta Maisha na kuacha familia yake nyumbani,baada ya Miaka mitatu akaja rasmi kuwachukua wakaishi wote ughaibuni,lakini akataka kujua uhalali WA watoto wake,katika vipimo ikajulikana kwamba mtoto mmoja Kati ya wale watatu sio wake,Ila sikujua je alienda nao wote huko ughaibuni au laa coz sikutaka kujua.
Haya ndio mambo ambayo hutokea kila siku katika Maisha yetu,lakini hii haituhusu Sisi ambao Mungu katujalia ukipata mtoto inatoka chata ambayo Katu haina mashaka ndani yake, ishu inakuja pale ambapo chata ya mtoto haisomeki kabisa hapo ndio penye shida na kuleta wasiwasi na hapo ndio mwanzo WA kipimo kuhusika.
Lakini Kwa upande wa Dini mwenye shamba ndio mwenye mtoto, Yani hata akitokea mtu kaja kulima kwenye shamba langu basi Yale mazao ni yangu mimi, Kwa maana wewe ukipita na mke wangu huyo mtoto sio wako ni WA kwangu kwasababu Mimi ndio mwenye mke,ni Sawa na wewe ukipita na mke WA mtu huyo mtoto sio wako.
Nahitisha Kwa kusema kwamba Kwa maoni yangu binafsi naona kuna haja kubwa Sana ya kipimo hiki kisionekani kuwa Ni cha watu wenye uwezo Tu au watu WA kundi fulani bali kiwe Kwa ajili ya watu wote ili hatimaye tukomesha kabisa hii tabia ambayo imezidi kujenga mizizi katika jamii yetu kwasasa.
Ni hayo Tu!