Vipindi vya dini katika shule za msingi na Sekondari za Serikali vifutwe

China, Japan, Korea, Vietnam, Sri Lanka, Thailand na nchi nyingi za Asia hazijawahi kuwa na habari na kitu kinaitwa Biblia au Quran ila zina sheria na wanaishi kama binadamu waliostaarabika kwa kiwango cha juu sana.
Satan agents kumbe mpo jf?
Mungu kwanza mengine baadae, hayo maarifa yanatoka kwa Mungu, sheria zote zimetoka kwenye Biblia tukaziboresha, mtito akikulia dini hawoi mwovu, acha upuuzi wako wa kumdharau Mungu wa Israel.
 
Mimi nafikiri vingefanyiwa maboresho zaidi kwa kuangalia sifa na ufanisi wa wakufunzi wa vipindi hivi.
Kwani kwa sehemu kubwa vimekuwa vikipoteza muda wa watoto kujifunza kutokana na kutotiliwa maanani katika mitaala.
Pengine vingetumika kama psychotherapy na maswala mengine yanayohusisha mental health wellness pamoja na imani vingekuwa na manufaa sana katika kuwajenga watoto kiakili na ukuaji.
 
Mimi vipindi vya dini vilinisaidia sana kuwa mwanafunzi mwenye tabia nzuri. Nilikuwa mkorofi shuleni, lakini Neno la Mungu (kupitia kwa walimu wa dini waliokuwa wanakuja kufundisha) lilinisaidia kubadilika na kuwa mwanafunzi mtulivu. Kizazi cha sasa ni cha dotcom. Usipowafundisha wanafunzi mambo ya dini watafundishwa na ulimwengu; wataokota mambo machafu kutoka kwenye mitandao then tutaendelea kulia lia kwamba siku hizi kuna mmomonyoko wa maadili.
 
Umenena,iliyo kweli tupu.
 
Kwanini usi ishaur serikali ianzishe hayo masomo ya sanaa unayo yataka, kwan hujui dini ina msaada mkubwa kwa watoto bila dini cjui tu mambo yatakuaje.

umewaza vizuri lakini sio kwa kutumia akili
 
Kwani kuwa na vipindi vya dini ya kiislam au kikristo ndiyo hofu ya Mungu?
 
Hata wapagani ni raia kamili na wana haki zote katika hii nchi. Kuna shule zinalazimisha kwa viboko wanafunzi wote waende kwenye vipindi vya dini. Hii sio sahihi.
Sio kweli,hakuna mwanafunzi anayelazimishwa kwenda kwenye vipindi vya dini.
 
China, Japan, Korea, Vietnam, Sri Lanka, Thailand na nchi nyingi za Asia hazijawahi kuwa na habari na kitu kinaitwa Biblia au Quran ila zina sheria na wanaishi kama binadamu waliostaarabika kwa kiwango cha juu sana.
Aliyekudanganya,kakudanganya sana,hizo nchi,zina watu wengi wanaomini uwepo wa Mungu,kuliko nchi zote duniani.
 
Umesema kweli tupu.
 
Acha mzaha
 
Kuna faida nyingi za kulea watoto ktk misingi ya hofu ya Mungu kuliko kutofanya hvyo.
 
Misingi ya imani/dini wajengee nyumbani kwako, kanisani, msikitini au kwa waganga wa kienyeji. Hiyo haipaswi kuwa kazi ya serikali. Zaidi sana kuna shule za seminary na za mashirika ya dini, wafanye hiyo kazi.
 
Misingi ya imani/dini wajengee nyumbani kwako, kanisani, msikitini au kwa waganga wa kienyeji. Hiyo haipaswi kuwa kazi ya serikali. Zaidi sana kuna shule za seminary na za mashirika ya dini, wafanye hiyo kazi.
Kwani wewe unaumia wapi mkuu,.??naona jambo hili linataka likutoe machozi ya uchungu,..
 
Kuna wengine wengi walikuwa na tabia mbovu sana, tena wakiwa viongozi wa dini shuleni.
Shule inaendeshwa kwa sheria na taratibu kama mwanafunzi hazifuati kuna adhabu zake zimeainishwa, sio kazi ya vipindi vya dini kudumisha amani, utulivu na utaratibu shuleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…