Vipindi vya dini katika shule za msingi na Sekondari za Serikali vifutwe

Vipindi vya dini katika shule za msingi na Sekondari za Serikali vifutwe


Wale waliofanikiwa kupata elimu ya darasani angalau ya darasa la saba na kuendelea watakumbuka vipindi vya dini ambavyo vilitengwa rasmi kulingana na madhehebu mbalimbali na wanafunzi wote ni lazima kuhudhuria katika vipindi hivyo.

Mara nyingi vipindi hivi huwa Ijumaa kuanzia muda wa saa nne ili kuwapa fursa waislamu kwenda msikitini kwa sababu mara nyingi wao huwa hawatumii madarasa kuswali katika vipindi vya dini kama wenzao Wakristo.

Wakati mjadala wa tija elimu yetu ukiwa mkali bungeni na mtaani ipo haja ya kuliangazia pia jambo hili na kuona kama kuna tija yeyote kuwa na hivi vipindi.

Ukiangalia kwa makini utagundua vipindi hivi vya dini havina tija yoyote kwa wanafunzi zaidi ya kuwachukulia muda wao ambao ungweza kutumika katika mambo mengine muhimu kama sanaa za uchoraji, uchongaji, kuimba, kuogelea, ushonaji n.k

Ni wakati sasa mamlaka zinazohusika na elimu zitoe muongozo wa vipindi hivi kufutwa na kuongeza mambo mengine secular au kupunguza muda wa wanafunzi kukaa darasani.
ww ni mjinga na mpumbavu na huna akili. hivi nyie mnashindwa kujua umuhimu wa dini kweli? unasema wanapoteza muda una akili wewe? Hizi dini ndio zilotufunza usafi, kuwaheshimu Wazeee, kusaidia masikini,.kuwapenda ndugu na.jirani zetu, kuacha anasa kama pombe na zinaa, kuepuka wizi, kuepuka Riba, yote haya ww unasema dini haina maana, sikulaumu ww ila jichunguze vizuri kama hukuzaliwa gesti basi niite Zumaridi
 
Mimi nafikiri uende shule za watoto wako ukawaambie walimu kuwa wanangu ni wapagani kwahiyo msiwalazimishe kuingia vipindi vya dini kwasababu wewe baba yao huamini katika Mungu..na sio kutaka vijana/watoto wetu wapotee kwa kukosa misingi mema ya imani/dini..
umemjibu vizuri sana, haya majinga yanaongezeka kila kukicha
 
Taifa au familia yoyote bila misingi ya dini (haijalishi Ni dini ipi)

Iyo familia itageuka familia ya hovyo Sana.
- Kuua
-kubaka
-wizi
-Chuki
-unafiki
-mapenz na Ndugu
-mapenz ya jinsia moja
-mapenz kinyume na maumbile
-mapenz na wanyama
-ukatili
- ulevi na madawA
-ushirikina
-umalaya na ukahaba
-Nidhamu mbovu
-uzalendo sifuri
-utii hamna

Ndo maana serikali
imeruhusu na inazilea taasisi za kidini (hazilipi Kodi) ili kuisaidia serkali kujenga mshikamano, Aman, utulivu na kutunza ustaarabu wa wananchi wake.



Sent using Jamii Forums mobile app
Basi Tanzania itakuwa mojawapo maana ulivyotaja hapo vimeshamiri sio tu Tanzania lakini nchi zote.
 
Kwa upande mmoja nakuunga mkono! Kwa kizazi hiki Masomo ya dini hayana faida kwao.
 
Baada ya kusoma huu Uzi,
Kuna Mambo kadhaa nimegundua kwa mtoa mada

1. Ana umri mdogo bila Shaka
(huenda Ni mwanafunzi bado)

2. Hana familia
(Hata Kama anayo Basi inalelewa na Ndugu,wakwe au wazazi wake)

3. Ana upeo mdogo Sana wa kufikiri.
(Haiwazii kabisa athari ya Jambo kabla ajalitekeleza, Anaendeshwa na mihemko)

4. Hana hofu ya Mungu kabisa
Endelea kujidanganya hivyo
 
Back
Top Bottom