NullPointer
JF-Expert Member
- Feb 7, 2011
- 3,461
- 2,273
hata pilot wa hivo ni wachache sanaMkuu,ina maana miaka 11 na miezi sita umeitumia angani?
Mbeya-Dar na fastjet mama mtu mzima kabeba na kuku kokoliko kufika airport kuku karuka huyooooo
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.
Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.
Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.
Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.
Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
Mimi nimepanda ndege za masafa tu...ba,klm,swissair,emirates.....sikupata tabu yoyote kwasababu nilisimuliwa na kuona vingi kwenye tv/movies....lakini sijawahi kui-enjoy wala sitakuja ku-enjoy flight....
Napanda coz i have to....safari za local nita-drive au kupanda bus....i hate flying,kitu kitapaa vipi hewani bila kushikiliwa???kikigoma??i hate flying.
hahahahahahaha nimecheka sana mkuu huyo wa pombe kali ulafi ulimponza
Mimi sikumbuki vizuri,ila nina zaidi ya masaa laki moja hewani
Umeona eeeh yan unacheka mpaka stress zinaishaa
Mi siku ya kwanza sikua na woga ilikua ni mwanza-dar... sema ile siku kesho yake naenda masomoni mamtoni aisee ule usiku sikulala nlikaa naimagine mchakato utakavokua hadi asubuhi nlikua wa kwanza kutoka kitandani maana sikusinzia, siku za nyuma nlikua nalala kinoma... nkatupia ka mshati kangu kameandikwa afrika afu nliwahi airport kinoma
he he he....ningekwambia logbook nini ungebisha kama ulivyombishia Masanja ndio maana nimekuwekea na tafsiri ya dictionary na inaonyesha wazi ni dictionary.....anyway sijaona kituko chako ulivyopanda ndege..... siku njema.
sitasahau nilipopanda KLM hadi schipol/amsterdam uholanzi, nilikuwa naunganisha kwenda nchi nyingine ya ulaya. wiki hiyo kuna kijana gaidi wa nigeria alikamatwa anataka kulipua ndege ya delta ya wamarekani, hivyo mwafrica yeyote akionekana alikua akapekuliwa vilivyo. huwezi amini, tulikuwa tumeongozana na wazungu wengi, lakini walipoona ngozi nyeusi tena inatoka africa, waliniweka pembeni wakaanza kukagua doc zangu zote polepole. they really humiliated me, askari mmoja akamwambie mwenzie "mwache uyo dogo hana tatizo", ndio nikaachiwa, lakini hata hivyo hawakuamini, mizigo yangu badala ya kupakiwa kwenye ndege yangu (kwasababu nilishachelewa ndege niliyotakiwa kuunganisha interval ya lisaa limoja) mizigo ilibaki, nilipata extension ya shirika lilelile la ndege bila malipo lakini kwa kupitia ufaransa na nikafika kwa kuchelewa masaa matano, ratiba yangu yote imevurugika. nilipofika airport yangu yamwisho nilikuwa kuna kifurushi wameweka dawa za mswaki, tshirt ya shilika la ndege na kisuruari wakaniambia nitatumia kuvaa, ila niache address ya wapi nitakaa. drive from the airport hadi mtaa niliokuwa naenda kuishi ni nusu saa. nikaondoka. kesho yake, askari walileta mabegi yangu yote. kuangalia, kumbe waliyachelewesha ili wayakague. HAPO NDIPO NILIPOONA UBAGUZI na ukatili wa wazungu. Mungu awasamehe......