Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Mi siku ya kwanza sikua na woga ilikua ni mwanza-dar... sema ile siku kesho yake naenda masomoni mamtoni aisee ule usiku sikulala nlikaa naimagine mchakato utakavokua hadi asubuhi nlikua wa kwanza kutoka kitandani maana sikusinzia, siku za nyuma nlikua nalala kinoma... nkatupia ka mshati kangu kameandikwa afrika afu nliwahi airport kinoma
 
Sitazungumzia siku ya kwanza ila nitazungumzia mara ya mwisho last sunday morning 16/02/2014, nilikuwa natokea Dar kuja mwanza . Nilichokishuhudia siku ile sijawahi kukiona airport ya J.inter. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kupanda fastjet -foleni ilikuwa ni kubwa sana kwenda kuhakiki tickeck .

Kioja nilichokiona kingine (nadhani labda ni ushamba wa kutokupanda fastjet ) ukipandisha ngazi kwenda kwenye chumba cha kusubiri kupanda ndege kuna scanner pale -pale ndipo nilistaajabu tena kulikuwa kuna watu wengi hatari (abiria wa fastjet) mpaka wengine tunaning'inia kwenye ngazi (sio zile automatic stairs).Kutokana na kwamba ndege walishatangaza watu waanze kuingia ikawa sasa ni kugombania kukaguliwa ili mtu asiachwe -mparangano kama ule niliwahi kuuona mara ya mwisho na mimi nikiwemo ,kwenye daladala za kutoka mbagala kwenda ubungo 2004 kituo cha kizuiani na ubungo kwenyewe jioni kurudi mbagala . Sio kwamba nachekesha ila ndicho kilichotokea pale.

Kilichopoza mvurugano ule ni jamaa wa pale kuwatoa wasiwasi abiria kuwa hakuna atakayeachwa maadamu wote tumefika pale na wanatuona . Hii kwangu nakiri kwamba ni-ushamba wa kutokuwahi kupanda fastjet .

Ndugu zangu wengine ambao mmezoea ndege nyingine unakuwa mfalme unanyenyekewa -hapana hapo kwa fastjet mnapigana vikumbo kama kawa kwenye kila steji ya kukwea pipa.
 
Mimi nimepanda ndege za masafa tu...ba,klm,swissair,emirates.....sikupata tabu yoyote kwasababu nilisimuliwa na kuona vingi kwenye tv/movies....lakini sijawahi kui-enjoy wala sitakuja ku-enjoy flight....
Napanda coz i have to....safari za local nita-drive au kupanda bus....i hate flying,kitu kitapaa vipi hewani bila kushikiliwa???kikigoma??i hate flying.
 
me ilikuwa mtwara kwenda Dar, bahati nzuri nilisafiri na mtu mzoefu sasa chabo nililokuwa napiga we acha kila kitu naigilizia. Ila kahawa ilinimwagia chapachapa sababu ya mchecheto, mmmh.. ushamba acha tu
 
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.

Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.

Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.

Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.

Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.

hahahahahahaha nimecheka sana mkuu huyo wa pombe kali ulafi ulimponza
 
Mie pia nikiri kuwa sipendi kupanda ndege ila huwa ninatamani sana kufika sehemu fulani na njia pekee ni kupanda ndege. Ni kama kusema kuwa ili ufike Peponi, ni lazima ufe.

Kwa taarifa yako tu ni kuwa NDEGE ni usafiri ulio SALAMA kuliko usafiri wowote ule duniani. Mara nyingi sana ndege zinapata ajali na kuanguka kwa makosa ya Binadamu ya Kizembe au kwa makusudi kwa kupigwa bomu au kulazimisha vitu. Ninasema kulazimisha vitu ni pale ambapo rubani analazimishwa kupaa huku akiwa kachoka, akili yake si nzuri, kutua kwa lazima sehemu ambayo ni hatari nk. Ila kwa mazingira ya kawaida, ni salama sana. Ndiyo maana kila siku iendayo kwa Mungu, kuna ajali kibao za magari hapa Tanzania pekee na ajali chache sana za ndege DUNIANI.
Mimi nimepanda ndege za masafa tu...ba,klm,swissair,emirates.....sikupata tabu yoyote kwasababu nilisimuliwa na kuona vingi kwenye tv/movies....lakini sijawahi kui-enjoy wala sitakuja ku-enjoy flight....
Napanda coz i have to....safari za local nita-drive au kupanda bus....i hate flying,kitu kitapaa vipi hewani bila kushikiliwa???kikigoma??i hate flying.
 
Huwezi kuamini hadi leo ni Mnywaji mzuri sana mara anapoamua kunywa. Kuna siku alikunywa hadi akajigonga mezani na akapoteza fahamu. Mungu bariki watu wakampa huduma ya kwanza na akachukua Taxi kurudi nyumbani.

Ila namsifu na ulevi wake wote, jamaa ni Family Man na anajali familia yake na Wazazi wake. Kwa sasa ni Mhandisi mzuri sana wa IT na mchapa kazi mzuri. Ila akiamua kuipiga chupa, anaitandika hadi Chupa inamkomesha.
hahahahahahaha nimecheka sana mkuu huyo wa pombe kali ulafi ulimponza
 
Mimi ilikuwa mwaka jana mwezi kama huu naenda zangu mwanza kutokea Dar...ilikuwa utata! kwanza siku mbili kabla ya safari sikupata usingizi kabisa....nikawa naota ndoto za hatari tupu! siku ya safari nilikuwa naangaika sana pale eapot, make kila procedure kwangu ilikuwa mpya katika maisha yangu! ila kiujanjaujanja tu nikafanilikiwa!

Kubwa,ni pale ndege ilipokuwa inaanza kupaa! nilihisi kufakufa vile...halafu niliduwaa,mwanza ndani ya saa moja tu nishaingia!

Ahsante fastjet kwa kuni update!
 
Jamaa alipanga kubana matumizi akaingia kwenye ndege akiwa anakataa kila kinachogawiwa ndani ya ndege kwamba itakuwa gharama sana.

Alipigwa njaa mbaka basi wakati wa kushuka akawambia wenzake mmejifanya kula Ngoda mletewe bill jamaa wakamwambia hakuna bill mbona vile ulishalipia?
 
Mi siku ya kwanza sikua na woga ilikua ni mwanza-dar... sema ile siku kesho yake naenda masomoni mamtoni aisee ule usiku sikulala nlikaa naimagine mchakato utakavokua hadi asubuhi nlikua wa kwanza kutoka kitandani maana sikusinzia, siku za nyuma nlikua nalala kinoma... nkatupia ka mshati kangu kameandikwa afrika afu nliwahi airport kinoma

hahaaaaaaaaa chezea kupanda ndege lol..usingizi haaukuja hata
nikisoma hii thread nacheka sana
 
Full kujipiga picha, kushangaa wahudumu na kuangalia nje nione mawingu na nyumba zilivyondogo chini na kukadilia mahali mnapoweza kuwa kama ningesafili kwa gari.
 
Mkuu TCleverly
Sikutaka kuendelea na thread hii kwani naona jamaa alivaa jezi mapema na refa hakuja niliona bora nichomoke
Jerrymsigwa ahsante kwa elimu sie wengine ni maimuna kwahiyo usiwe na hard felling
he he he....ningekwambia logbook nini ungebisha kama ulivyombishia Masanja ndio maana nimekuwekea na tafsiri ya dictionary na inaonyesha wazi ni dictionary.....anyway sijaona kituko chako ulivyopanda ndege..... siku njema.
 
sitasahau nilipopanda KLM hadi schipol/amsterdam uholanzi, nilikuwa naunganisha kwenda nchi nyingine ya ulaya. wiki hiyo kuna kijana gaidi wa nigeria alikamatwa anataka kulipua ndege ya delta ya wamarekani, hivyo mwafrica yeyote akionekana alikua akapekuliwa vilivyo.

huwezi amini, tulikuwa tumeongozana na wazungu wengi, lakini walipoona ngozi nyeusi tena inatoka africa, waliniweka pembeni wakaanza kukagua doc zangu zote polepole. they really humiliated me, askari mmoja akamwambie mwenzie "mwache uyo dogo hana tatizo", ndio nikaachiwa, lakini hata hivyo hawakuamini, mizigo yangu badala ya kupakiwa kwenye ndege yangu (kwasababu nilishachelewa ndege niliyotakiwa kuunganisha interval ya lisaa limoja) mizigo ilibaki, nilipata extension ya shirika lilelile la ndege bila malipo lakini kwa kupitia ufaransa na nikafika kwa kuchelewa masaa matano, ratiba yangu yote imevurugika.

nilipofika airport yangu yamwisho nilikuwa kuna kifurushi wameweka dawa za mswaki, tshirt ya shilika la ndege na kisuruari wakaniambia nitatumia kuvaa, ila niache address ya wapi nitakaa. drive from the airport hadi mtaa niliokuwa naenda kuishi ni nusu saa. nikaondoka. kesho yake, askari walileta mabegi yangu yote. kuangalia, kumbe waliyachelewesha ili wayakague.

HAPO NDIPO NILIPOONA UBAGUZI na ukatili wa wazungu. Mungu awasamehe......
 
sitasahau nilipopanda KLM hadi schipol/amsterdam uholanzi, nilikuwa naunganisha kwenda nchi nyingine ya ulaya. wiki hiyo kuna kijana gaidi wa nigeria alikamatwa anataka kulipua ndege ya delta ya wamarekani, hivyo mwafrica yeyote akionekana alikua akapekuliwa vilivyo. huwezi amini, tulikuwa tumeongozana na wazungu wengi, lakini walipoona ngozi nyeusi tena inatoka africa, waliniweka pembeni wakaanza kukagua doc zangu zote polepole. they really humiliated me, askari mmoja akamwambie mwenzie "mwache uyo dogo hana tatizo", ndio nikaachiwa, lakini hata hivyo hawakuamini, mizigo yangu badala ya kupakiwa kwenye ndege yangu (kwasababu nilishachelewa ndege niliyotakiwa kuunganisha interval ya lisaa limoja) mizigo ilibaki, nilipata extension ya shirika lilelile la ndege bila malipo lakini kwa kupitia ufaransa na nikafika kwa kuchelewa masaa matano, ratiba yangu yote imevurugika. nilipofika airport yangu yamwisho nilikuwa kuna kifurushi wameweka dawa za mswaki, tshirt ya shilika la ndege na kisuruari wakaniambia nitatumia kuvaa, ila niache address ya wapi nitakaa. drive from the airport hadi mtaa niliokuwa naenda kuishi ni nusu saa. nikaondoka. kesho yake, askari walileta mabegi yangu yote. kuangalia, kumbe waliyachelewesha ili wayakague. HAPO NDIPO NILIPOONA UBAGUZI na ukatili wa wazungu. Mungu awasamehe......

dah so sad
 
Back
Top Bottom