Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Pamoja na kuwa na kauzoefu ka kwenda AFRIKA KUSINI ,na safri za Mwanza na Arusha ,QATAR AWAYS iLINIACHA HOI ,vIDEO' ILIYOKUWA MBELE YANGU SIKUWEZA KUITUMIA NILIBAKI NAANGALIA MWELEKEO WA NDEGE TU! HAD NAIROBI ALPOINGIA MDADA MMOJA MKIKUYU AKAWA ANAANGALIA MOVE ,SIKUJUA NI KITU GANI!
 
Yakwangu sio mara ya kwanza ila ni kioja balaa,ni mwaka 1997 December 22 kutoka Dar kwenda Amsterdam na KLM. Miezi hiyo kwa kawaida Dar ni joto sana so nilivaa kaptura ya jeans na Tshirt na nikisafiri sipendi kubeba mizigo ya mikononi kwani ni msahaulifu,hivyo mizigo yangu yote niliipitisha ipimwe ili nisibaki na kitu mkononi.

Safari ilikuwa nzuri mpaka tunafika,sasa karibu tunatua Amsterdam rubani anatutangazia hali ya hewa nasikia outside at ground level is -5 C,sikuwaza wala kushtuka sana coz kwa wakti huo ndani ya ndege ilkuwa pako poa sana.Ile tumefika wenzangu wote wanafungua mikoba yao na kutupia makoti marefu even air hostess mimi nabung'aa macho tu,tukashuka kwenye ndege kwenda ndani ya basi ili tuende terminal watu wote wananishangaa,nikaanza kuwa mweupe ule wa unga,mpaka tunafika lounge,mdomo hauwezi funguka.

Bahati nzuri wenyeji wangu kama walihisi manake waliomba ruhusa nikaletewa koti refu la sufi,gloves na Kofia mzula.Nilikuwa kama mfu nusu kuongea siwezi,vidole vya mikono vimekakamaa balaa mabegi nayaona yanapita ila siwezi kuyachukua,pale Amsterdam kuna sehemu wenyeji wanawaona arrival kwenye kioo,so waliniona the way nilivyoganda wakaomba waingie kunisaidia mizigo.

Mpaka naingia kwenye gari siwezi kuongea,hadi tunafika nyumbani heating system ilisaidia baada ya masaa mawili ndo niliweza kunyanyua mdomo.

Siwezi kusahau kioja hiki kwani wakati natoka Dar nilikuwa "Bontown" ila kule nilikuwa zoba (kila mjanja ana mjanja wake)
 

Hii kali dah ka tom vile akiwekwa kitimoto na Jerry
 
Haha ukifuata maelekezo na kutulia ndani ya ndege, hakuna hata mmoja atakayejua kuwa it's yo first time to be in flight. Ila nimecheka sana kwa expiriences za watu hahaha.
 

hahahhaha, u made my evening,km nakuona vile,poleh sana
 

Mi ningekunasa makofi..,
 
Hahahha,hii thread noma sanaa,nlikuwa nacheka kama chizi
heri yenu mshatua zigo la ushamba,mie hapa sijuiii ntaumbukaje,ila ntakuwa nauliza wazoefu...
 
niliachwa na ndege na mizigo ikapotea hadi nilipoletewa home. sitasahau
 
Duh, pole sana aise, vaa kaptula na tshirt unatoka mwanza kwenda dar, sio huko kwa wenzetu wasiolijua jua


 
Me leo ndo siku ya kwanza eti nina mzuka hadi sina usingizi wakati ndege yenyewe ni saa 7 reporting time. Naendelea kupitia comments nijifunze nisije kuumbuka
 
Me leo ndo siku ya kwanza eti nina mzuka hadi sina usingizi wakati ndege yenyewe ni saa 7 reporting time. Naendelea kupitia comments nijifunze nisije kuumbuka

Saa ngapi hewani mkuu? Hizo za domestic huwa ni saa1 tu unakua umeonja
 

duuh hapa sina usingizi nina safari ya kwanza leo mchana, umenipa wazo maana me mtu wa kuaamkaga za mbili asubuhi sasa nikijifanya nimeamka now hapo home wataniona nina mzuka na safari kweli.

Ngoja niendelee kuwepo kitandani
 

Mkuu asante kwa kuanzisha uzi huu maani umenisaidia mambo mengi. Kikubwa nilichojifunza ni kuuliza pale unaposhindwa au kutaka kitu. Natumahi uzi huu na comments zitanisaidia kwenye safari yangu.
 

Dawa ya meno....
 

Nimecheka sana mkuu.Dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…