Yakwangu sio mara ya kwanza ila ni kioja balaa,ni mwaka 1997 December 22 kutoka Dar kwenda Amsterdam na KLM. Miezi hiyo kwa kawaida Dar ni joto sana so nilivaa kaptura ya jeans na Tshirt na nikisafiri sipendi kubeba mizigo ya mikononi kwani ni msahaulifu,hivyo mizigo yangu yote niliipitisha ipimwe ili nisibaki na kitu mkononi.Safari ilikuwa nzuri mpaka tunafika,sasa karibu tunatua Amsterdam rubani anatutangazia hali ya hewa nasikia outside at ground level is -5 C,sikuwaza wala kushtuka sana coz kwa wakti huo ndani ya ndege ilkuwa pako poa sana.Ile tumefika wenzangu wote wanafungua mikoba yao na kutupia makoti marefu even air hostess mimi nabung'aa macho tu,tukashuka kwenye ndege kwenda ndani ya basi ili tuende terminal watu wote wananishangaa,nikaanza kuwa mweupe ule wa unga,mpaka tunafika lounge,mdomo hauwezi funguka.Bahati nzuri wenyeji wangu kama walihisi manake waliomba ruhusa nikaletewa koti refu la sufi,gloves na Kofia mzula.Nilikuwa kama mfu nusu kuongea siwezi,vidole vya mikono vimekakamaa balaa mabegi nayaona yanapita ila siwezi kuyachukua,pale Amsterdam kuna sehemu wenyeji wanawaona arrival kwenye kioo,so waliniona the way nilivyoganda wakaomba waingie kunisaidia mizigo.Mpaka naingia kwenye gari siwezi kuongea,hadi tunafika nyumbani heating system ilisaidia baada ya masaa mawili ndo niliweza kunyanyua mdomo.
Siwezi kusahau kioja hiki kwani wakati natoka Dar nilikuwa "Bontown" ila kule nilikuwa zoba (kila mjanja ana mjanja wake)