Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)


Dah.....humu ndan leo vicheko tu
 
Ukitaka kujua ushamba wa wanyakyusa tembelea Songwe international airport mbeya, yaani watu wanatembea yapata 10kms kuja kushangaa fastjet
 
Ulikuwa mzembe wa kusoma hukuiona reporting time.
+Ni kazi especially siku ya kwanza. Aidha wakati mwingine zinachanganya hata kwa mzoefu! Ndio maana kasema kishajifunza!
 
Ukitaka kujua ushamba wa wanyakyusa tembelea Songwe international airport mbeya, yaani watu wanatembea yapata 10kms kuja kushangaa fastjet
Jamani so nice safi sana watu wa Mbeya tena ina mandhari mazuri saaana. Nakumbuka tulivyokuwa wadogo tulikuwa tunaupara na kwenda stesheni, Dodoma.

Mpaka kwenye kichwa cha treni nikiwa na dada zangu, mdogo wangu, kaka yangu aliyekuwa kinara wetu alikuwa na guts mpaka anaongea na dereva wa Treni. No wonder sasa hivi ni Engineer Mahiri!
 
Ukitaka kujua ushamba wa wanyakyusa tembelea Songwe international airport mbeya, yaani watu wanatembea yapata 10kms kuja kushangaa fastjet

Ukome wewe, kichwa chako! Uwanja wa ndege hapa Mafiati umekuwepo miaka na miaka nani anaenda Songwe?
 

sisi wanyiha hatuna ushamba huo
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...

Dah..... Hiiii kali sna, nmecheka sna leo
 

Binafsi pia sijawahi zoea wala kupenda usafiri huu wa ndege, huwa napanda kama nina safari ya kikazi tu, otherwise kitu cha basi kama ni safari binafsi, taking off and landing huwa ni wakati mgumu sna maishani mwangu mana huwa nahisi kila kitu tumboni kinatoka.

Last month this year nlikuwa mtwara nkifanya juu chini mpaka wakati wa kurudi nikapanda basi mana nlikuwa kila nkiifikiria safari nakosa raha kabisa, tena ndo ukiwa kwa vindege vidgo lahaaa ndo balaa zaidi
 
kwikwikwi we utakuwa mpare tu next time mwambie akuandalie chapati unaziweka kwenye handbag

 

Hii rekodi yenu haijapatapo kuvunjwa, nyie ni masupa staa wa airport.
 
Ilikuwa 2012 ndo kwa mara ya kwanza napanda ndege niko kwenye FASTJET ya kutoka MWANZA kuja DAR, nilikuwa na mihemuko balaa, niliiwazia hii safari kwa muda wa wk 2, nakumbuka nilipiga picha kila sehemu nilipopata Aiport, nje ya ndege na ndani ya ndege mpaka leo zipo nimezihifadhi kwa ajili ya wanangu, wajukuu na vitukuu.



Kali zaidi tulipokuwa hewani ndani ya NDEGE nikamwita mhudumu nimwulize wapi TOILET, akanionyesha, nikaenda japo sikuwa na haja yoyote nikaishia kutema mate kwenye sink la chooni , kuflash, nikanawa mikono, nikasukutua mdomo na kutoka zangu.



Tulipotua pale JKNIA asubuhi saa 09:40 akili ndo ikazidi kupagawa baada ya kuyaona yale MADEGE mengine makubwa makubwa yanapaa na kutua, nikaashangaa kama dakika 15 hivi na kutoka zangu nje, pale nje sasa madereva TAX full kushupalia, wapi kaka, twende na hii, bei poa tu, kwenda kuuliza bei toka pale mpaka TEGETA sh ngapi eti naambiwa elfu 35, nikajisemea moyoni shwaiiiiinnn sana, wakati nimetoka Mwanza mpaka Dar nauli elfu 32 tena kwa NDEGE halafu kutoka hapa mpaka TEGETA elfu 35, nikaachana nao na kwenda kupanda zangu daladala kwa nauli ya sh 950 ila nyumbani niliingia 13hr shauri ya foleni.
 
ungekuwa kikojozi ungekoma ubishi

 
Wanyakyusa watani zangu kwa ushamba mnaongoza nchi hii no wonder joti hafiki kwa mzee mwalubandu huenda huyo mzee kaenda kushangaa ndege airport
 
Wanyakyusa watani zangu kwa ushamba mnaongoza nchi hii no wonder joti hafiki kwa mzee mwalubandu huenda huyo mzee kaenda kushangaa ndege airport. Badilikeni nyie kina mwakifulefule
 

mkuu umenichekesha sana hasa hii namba nne na namba tatu kwi kwi kwi kwi kwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…