Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Sijui kwanini nilichukulia kawaida saana

Same wit me, nliona kawaida tu ingawa ki ukweli nlikua na mchecheto sanaa nlijitahidi kuificha. Kuna ushamba mwingine wakijinga sanaa...kuna ndugu yangu flan alipata a trip to malaysia na organisation flan for like 4 days..

Bas nakwambia aliaga ukoo mzima that anaenda Malaysia....unajua unakuta watu hawajawahi panda pipa before but alivyokua anajitapa tapa alikua anaonekana mseng* sanaa. He was like 25 of age. Ukimkumbusha leo mnaweza mkagombana.
 
kazi zaidi ipo kwenye ukaguzi watu kibao huacha mi-poafyumu, dawa za mswaki pale na wale wakaguzi hawakuelekezi uweke kwenye begi kubwa (la kucheck-in) wao wanafurahi maana baadae wanagawana. USHAMBA GUNIA LA KONO KONO
 
Ulikuwa ukitegemea kusindikiza hadi ndani ya ndege ndio uendelee kutoa maagizo ya kule aendako
 
kwa mara ya kwanza nilipanda mwaka 2012 south africa airways...basi kikafika south sasa natakiwa kubadilisha ndege kwenda zimbabwe..duuu sisahau ilikuwa ni muda mfupi sana wa kubadilisha ndege na mm ni mshamba mpaka napata ndege ya zimb jasho limenitoka balaa mana ile airport ya south africa ni kubwa balaaa...ila thanks kwa sasa nimezoea
 
Duh nimepanda juzi wakuu nimetoka dar kuja mwanza asee pale inapaa nilidata na ile kuyumba yumba kwenye mawingu na hali ya hewa juu haikuwa poa nusura ushuzi utoke ila nashkuru mungu tulifika salama japo sikuwa na uoga sana nilijifnya mjuzi kwenye baadhi ya mambo kama kufungua meza na kwenda chooni...ila fast jet huu utaratibu wakuuza vicoca cola elf 3 sio ishu me nilijua tunapewa bure hahahah dah niliinjoy nangoja return kurudi dar asee
 
ndege aisee ina utamu wake hasa kwa majirani yaani wk kabla ya kuondoka lazima ujisemeshe stori za kusafiri na ndege ili uonekane bab kubwa
 
Ingia www.fastjet.com halafu nenda kwenye plan your trip ama book a flight. Hapo utaje tarehe mbali mbali na kuangalia bei manake zinatofautiana. Usisahau kucklick return ili upate ya kwenda na kurudi. Ukikata ticket mapema kama wiki 2 ama 3 kabla nauli inakuwa chini sana
Jambo sana ndugu zangu.Kuna mtu anae jua gharama za kusafiri kwa fast jet from Dar to mwanza.Msaada please, hasanten
 
Huu uzi ni darasa tosha ila wakuu naombeni msaada kucheck-in online kwa fastjet unafanyeje?
 
Sina tofauti na Dennis Bergkamp yule legendary wa Arsenal naogopa kusafiri na ndege hadi basi.. . nilishautoa akilini huo usafiri. ..sijui naogopa nn
 
Mara ya kwanza kupanda ndege dk 2 kabla nilikula ugoro ili nisiskie chochote kinachoendelea! ilikuwa kutoka dar kwenda kenya
 
Utamu wa ndege usafiri mchana ndo utaenjoy
 
Sijawahi panda ndege ndo natarajia kupanda kwa mara ya kwanza, Je! Ni vitu gani vya msingi kuzingatia ni muhimu kweli kufika masaa mawili kabla?
 
HAHAHAHAAA
Mimi day one ilikua natoka kilimanjaro kwenda Mwanza na Precision air,sasa ninejipanga kabia mabegi yangu maana before safari nlishapewa miongozo na waru mbalimbali.

Nafika KIA nabanana na watu wanaongojasame ndege from nairobi,Nilikaa na mwarabu mmoja ye ndo kwanza kavaa simple chini ana ndala na mabuti kabeba kwenye mfuko wa rambo nkaduwaa mmhh huyu na rambo ndani ya ndege zinaruhusiwa??

Nawaza atarudishwa tu uyu kumbe mi ndo ushamba umenilemea kule ndani kama kwenye bus tu hamna kipya
Kingine ule uoga wangu nilisoma magazeti yote yaliyokuwa apo kwenye siti ya mbele yangu

HAHAHAHAA nasahau niliogopa kunywa chochote coz nmewaza kale ka glass kanaweza kakatikisika nikajimwagia soda bure, nlikuwa nawaza ndege inatikisika muda wote
 

Uwiii mbavu zangu mie..
 

Aiseee nimecheka mpaka mbavu zinaniuma sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…