Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Kwani wanaruhusu kufungua madirisha na kupiga kishoka
 
Mpaka sasa nina 200 USD ili DECEMBER na mimi nikwee pipa lolote la ULAYA (Swiss Air au KLM)
Robo ya mwaka imeisha una $200! Ulaya utaisikia! Halafu ukitaka kuichukia Ulaya kama unaenda mara ya kwanza nenda December,utajuta.
 
Mi pia kwa sasa nataka nipande SwissAir hata kama sio kwenda Afrika japo tu nitoke nilipo kwenda nchi nyingine ila ndani ya Europe nipaone tu na hapo Zurich maana hawa jamaa nauli zao mhhh ni juu sana ukilinganisha na KLM
Mimi nilihakikisha napanda ndege zote za mashirika ya Ulaya. First trip Dar-London nilipanda KLM kwa kweli nili-enjoy sana Amsterdam kwasababu connection yangu ilikuwa kama masaa sita baadae.

Then nikapanda British Airways wala siku-enjoy kwasababu unatoka London mara asubuhi unakutana na mabati yana kutu! Baadae nikapnda Swiss, aisee ile airport ya zurich ndio ilikuwa mpya,Loungee inaface runway bonge la view, then kubadili terminal moja kwenda nyingine unapanda vitreni havina dereva unabonyeza tu kinaondoka mpaka kwenye terminal yako chini kwa chini,ila shughuli nilivyopanda emirates, from London mpaka Dubai ndege kubwa nzuri mpya,kasheshe from Dubai Dar, ndege imechoka, imejaa waswahili ni kelele kama basi la mbagala,yaani pale pale dubai unajihisi tayari uko kariakoo! sasa hivi nachanga nipande ile A380

Kitu kilichonitoa ushamba ni Moving Walkway bado kidogo nidondoke Amsterdam mwaka 2000

 
Katika hiyo orodha hapo juu [emoji115] [emoji115] mi nahitaji Swiss tu..... Na naimani kama sio mwaka huu basi next mwaka
 

Kama unazo bado ni pm zitanifaa nikupe za Tz mimi mara nyingi nakwenda Niger na Benini huko ndiyo kwao.
 
hahaha hii komenti sijui kwa nini haiishi utamu, sio kwa suti ya sarafina aisee...
 
Kenya Airways acheni mchezo wa kuleta ndege mbovu mbovu Dar
 
Mimi nakumbuka ilikuwa mwaka 2012 nilipopanda Qatar Airways wakati naelekea chuo nje ya Tz.

Kwavile ndio ilikuwa mara ya kwanza sikutaka hata mbwembwe nyingi,nilikuwa nacopy na kupaste jinsi alivyokuwa anafanya mdada flani wa kifaransa pembeni yangu.

Safari ilikuwa nzuri tu.
 
Ulimuomba mchezo?
 
haaa, ko mnatutambishia au sio...? ngoja nianze mipango na mim nipande mwezi ujao then ntaleta mrejesho.! mana naona vijana kila mmoja analeta mbwembwe zake.
 
Wadau wiki ijayo nakwea tena pipa naelekea LOS ANGELES kwa KLM (kupitia AMSTERDAM) but this time around nishazoea msihofu wadau nitawawakilisha vema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…