Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Wadau wiki ijayo nakwea tena pipa naelekea LOS ANGELES kwa KLM (kupitia AMSTERDAM) but this time around nishazoea msihofu wadau nitawawakilisha vema.
Wadau wiki ijayo nakwea tena pipa naelekea LOS ANGELES kwa KLM (kupitia AMSTERDAM) but this time around nishazoea msihofu wadau nitawawakilisha vema.
nikusindikize mkuu? mimi sijawahi af umri unaenda
 
Haka kauzi niliwahi kukapitia mwaka jana nikiwa hata sijui ndege nitapanda lini?

Kalinisaidia kujifunza baadhi ya vitu ambavyo ningekutana navyo. BTW March 2015 nikakwea pipa for the first time in my history, ka fastjet pyaa Dar-Mwanza. Mwezi July ikawa tena from Mza to Dar and back to Mwanza

Hope this April, nitakwea tena kuja huko Dar na kurudi na nitatoka nje ya nchi kabla mwaka haujaisha.

Nilichojifunza, kwenye plane hamna jipya kwa sisi watoto wa mjini au ukiwa mjanja mjanja hutaaibika.

Asante my employer, my company kwa kunitua ushamba. Viva my Company.
 
Haka kauzi niliwahi kukapitia mwaka jana nikiwa hata sijui ndege nitapanda lini? Kalinisaidia kujifunza baadhi ya vitu ambavyo ningekutana navyo. BTW March 2015 nikakwea pipa for the first time in my history, ka fastjet pyaa Dar-Mwanza. Mwezi July ikawa tena from Mza to Dar and back to Mwanza.
Hope this April, nitakwea tena kuja huko Dar na kurudi na nitatoka nje ya nchi kabla mwaka haujaisha.

Nilichojifunza, kwenye plane hamna jipya kwa sisi watoto wa mjini au ukiwa mjanja mjanja hutaaibika.

Asante my employer, my company kwa kunitua ushamba. Viva my Company.

Wow! I wish na mimi nipande kwa mara ya kwanza mwaka ujao wa fedha! Make kwa sasa hata nauli ya fast jet sina
 
Mara ya kwanza kuoanda ndege nilikuwa nakwenda Uingereza. Niliogopa kula kwenye ndege. Nilipofika Amsterdam nilipotea njia ikabidi nitafutwe kwa kuitwa jina kwenye loud speaker kabla ya kupatikana na kukimbizwa kwenye ndege.

Nilipokuwa ninakwenda chuoni nilianguka kwenye escalator kwani ilikuwa mara ya kwanza kuziona. Acha tu. Nilichubuka miguu nikashindwa kutembea kwa takriban wiki moja. Ushamba kazi aisee.
 
Mara ya kwanza kuoanda ndege nilikuwa nakwenda Uingereza. Niliogopa kula kwenye ndege. Nilipofika Amsterdam nilipotea njia ikabidi nitafutwe kwa kuitwa jina kwenye loud speaker kabla ya kupatikana na kukimbizwa kwenye ndege. Nilipokuwa ninakwenda chuoni nilianguka kwenye escalator kwani ilikuwa mara ya kwanza kuziona. Acha tu. Nilichubuka miguu nikashindwa kutembea kwa takriban wiki moja. Ushamba kazi aisee.
Hahahaha pole sana mkuu
 
Mwezi Januari nilienda NEW DELHI duuh pale airport hakuna sijui kutangaza wala nini ni KIMYA KIMYA tu ukisubiri matanagazo utastukia ndege ishakuacha.
 
Delhi ule uwanja bomba kupitiliza, pengine kushinda hata Dubai pale hakuna kelele/matangazo ni ww kuangalia screen tu.
 
Mara ya kwanza kuoanda ndege nilikuwa nakwenda Uingereza. Niliogopa kula kwenye ndege. Nilipofika Amsterdam nilipotea njia ikabidi nitafutwe kwa kuitwa jina kwenye loud speaker kabla ya kupatikana na kukimbizwa kwenye ndege. Nilipokuwa ninakwenda chuoni nilianguka kwenye escalator kwani ilikuwa mara ya kwanza kuziona. Acha tu. Nilichubuka miguu nikashindwa kutembea kwa takriban wiki moja. Ushamba kazi aisee.
Ha ha ha till Rolling On The Floor Laughing.
 
Daaah niko ofisini, yaani bosi wangu yuko pembeni ila haoni nafanya nini mezani kwangu, yaani nimesoma thread yote nilikuwa nachekea tumboni, ila kuna mda kule kujibana kisauti kikatoka ikabidi nijikaushe na kakikohozi nikijifanya ni kikohozi kimenishika, hahahahaaaaa mmenichekesha mnoo wachangiaji wa hii mada.

Mie bana mara ya kwanza kupanda pipa ilikuwa wakati niko mdogo hata darasa la kwanza sijanza, tulienda Moshi kulikuwa na msiba ilikuwa air Tanzania ilikuwa na giza mnoo na hakukuwa na A/C sina memory nayo sana ila sikuona tofauti yoyote na ussafiri mwingine labda kwakuwa nilikuwa mtoto.

Nilipata sarafi nyingine nje ya nchi na mzazi wangu alienda kikazi, ilikuwa tunaenda Italy kwanza tuliachwa na ndege mara ya kwanza, tulichukua taxi kumbe ahikuwa na mafuta kufika njiani ikazima wakati huo hadi kupata taxi nyingine na ilikuwa alfajiri saa kumi na moja hivyo kufika airport ndege ishaondoka saa nyingi na safari ikasogezewa hadi wiki iliyofuata ndo tukafanikiwa kuondoaka.
Kwenye ndege ilikuwa KLM tulihudumiwa vizuri sasa nikapewa walkman (viredio vidogo ambavyo unaplay casset unasikiliza mziki na headphones zake) Mie kupewa ile baada ya kupewa msosi nilianza kusikiliza hadi usiku watu wanalala mama ananiambia lala mie namwambia sina usingizi nikajifanya nunda bana nikakesha nasikiliza mziki. Ile kufika alfajiri ndo macabin crew wanapita kuwapa watu vitafunwa kabla ya kushuka looh mie lepe la usingizi na mama kufikiria kunibeba mie, na mizigo aliyonayo nilikula makwenzi hayo hadi usingizi ukaisha hheheheheheheee.

Tulipofika Italy nyumba tuliyofikia ilikuwa toilet wametenga sinki za haja ndogo na za haja kubwa. Mie na akili zangu za utoto pamoja na kuwa mama alishanipa melekezi jinsi ya kutumia nikabanwa na kubwa na ndogo sasa nikasema wacha nipige nikae kwenye sinki la ndogo kisha nikimaliza ndogo nahamia sinki la kubwa kisha naflash. Weeh ile nakaa namalizia haja ndogo si ikaunganisha na kubwa hapohapo, sasa ile sinki ya haja ndogo inakachujio kama ka chai ukiflash kubwa inabaki palepale weeeh jasho lilintoka na maza alikuwa makali balaa....

Usitake kujua nilisolve vipi hilo tatizo maana nilikaa huko toileta kwa masaa mawili looh sitakaa nisahau. Hizi safari za ukubwani zilianza wakati naenda dubei ilikuwa poa kwani nilikuwa na mwenyeji then hizi za kikazi za nchini na nairobi wala hazijanipa shida thanks kwa muanzisha mada looh!!!
U made my day.
Uliamisha mzigo nn
 
Back
Top Bottom