Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Ha haaaaa
 
Mimi 2003 kwenye KLM kwenda Schiphol Amsterdam NETHERLAND nilitaka kula vitaulo vya kuoshea mikono, nijua chapati lakini ghafla nikaona jirani yangu anafuta mikono na kukirudisha kwenye tray nami chapchap nikamuiga.
Ha ha ha. Uuuuuwi. Hio KLM mie ndio ilinikomesha. Pata picha nimetoka msalani halafu nikapotea / nikasahau siti yangu iko wapi (usiniulize siti namba maana hata nilikuwa sijui kama kuna siti namba)😕, Balaa la pili kufika Amsterdam, hizo ngazi zao za kutambaa na kupanda ilikuwa majanga...
 
India kiukweli wamejipanga Mumbai airport nako si kama hapa kwetu JNIA
 
Tuisubirie dar airport mpya sijui itaitwa Ngosha Intl Airport?
 
Ha ha ha ha
 
ushamba mbaya sana was 2008 yaan ndege ilipoacha aridhi nilicheka sana hadi niliyekaa nae akaniuliza vipi...nikamwambia we acha tu
Ha ha ha mama were umenifanya nionekane kituko hapa ..
 
Atc mkileta hizo ndege mpya tupande bure basi kwa angalau wiki 2 kama mabasi ya mwendokasi Dar au sukari ile iliyokamatwa kwenye magodauni
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
daaah nimecheka sana hahahah
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
Ha ha ha ha

Kimeo cha mwaka
 
Ulijiona kama umejipaka majivu ama nini??? pole
 
Hii kali kuliko zote
 
Duu kumbe ww ndio nilikubebea perfum zako kwenye kandoo kangu kasamaki wakati tunatoka Mwanza kuja dar
Naona wengi tumekamatwa na malotion na manukato....siku ya kwanza jamaa airport alinipa huo ujanja wa kumuomba mtu mwenye kandoo ka samaki(kama wewe)pale Mwanza anitunzie hadi Dar but nikaona udwanzi kufika Dar nianze kukutafuta tena hiyo kazi ngumu.
Nikatupia vyote kwenye ndoo la uchafu nikakwea pipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…