Valentina
JF-Expert Member
- Oct 12, 2013
- 24,684
- 28,777
Ha haaaaaDa! Nimecheka mpaka basi.
Mimi mara ya kwanza kupanda ndege ilikuwa 2008 Precision Air. Dar to shy naenda Nzega Resolute Mine kufanya field. Kwanza nilipopata email ya tiketi yangu sikulala siku hiyo. Nilipofika airport ndio mara ya kwanza kuona ngazi za umeme. Sikuzitumia kwa sababu ya uoga. Nilikuwa nimebeba spray1 Dawa ya mswaki, Kulikuwa na nyembe na mkasi kwenye begi vyote niliviacha airport.
Nilipokuwa ndani ya ndege haikuwa shida but kuna moment nilipata mshtuko mkubwa kidogo nipige kelele kwa sababu ya ndege kuchange altitude. Niliona kama utumbo unataka kutoka.
Kituko kingine wakati narudi Dar kutoka shy. Kwa sababu tiketi nilikatiwa na kampuni na pesa ya taxi nilishakula. Sikuwa na pesa ya taxi toka shinyanga mjini kwenda airport na nilitaka kutunza pesa nilokuwa nayo kwa sababu nilikuwa narudi chuo na Boom halieleweki linatoka lini. Ilibidi niulize nauli ya baiskeli mpaka airport ni sh ngapi. Shinyanga daladala ni baiskeli tu mpaka leo.
Jamaa akaniambia ni 3000 tu badala ya 35000 ya taxi. Asubuhi akaniijia tukaanza safari. Balaa tukapita short kati kwenye mashamba ya mpunga. Si tukapotea? Tukatokezea kwenye fance ya nyuma ya uwanja maana hata jamaa wa baiskeli sikumwambia kana naenda kupanda ndege yeye alijua naenda kutembelea ndugu tu karibu na airport. So ikabidi tuzunguke fance mpaka getini.
Kama si ndege kubadili arrival time ningeachwa.
Nilipofika airport wafanyakazi wa pale walinicheka baalaa. Wakasema hawajawahi ona mtu anakuja airport kupanda ndege kwa usafiri wa baiskeli.
Tiketi ya hiyo safari nimeitunza mpaka leo kama kumbukumbu toka 2008.
But namshukuru Mungu kwa sasa atleast nimezoea mpaka hivi vindege vidogo.