Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Wadau nimetua hapa SYDNEY salam salimini hata mapicha sijapiga maana ile tunataka kupaa tu tukaambiwa tuzime simu, yaani safari ilivyokuwa ndefu sina hamu tena na ndege kiherehere chote kimekwisha aisee ile nimekwea pipa la kuja Sydney nimejikuta mwafrika peke yangu ndege nzima daaaH!!! ila Wazungu aisee ni noma huku kwao pazuri ajabu
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...

Hahahaha...
 
Mie mbona sitasahau,,,,,,,,,,
cku iyo nilijipodoa kama naenda harusini kufika airport parfume yng ikawekwa kwny dustibini niliumia sana.............
nilipoingia ndani sijui ni uoga nikaita air host aje kunifunga mkanda kasheshe wkt wa kushuka mkanda ukanishinda kufungua ikabidi jirani yng kk mmoja anisaidie..
tinna cute naomba unijuze ni kwanini hawaruhusu hizo perfumes? Na je ni conditions zipi kwa ujumla za kuzingatia wakati wa kusafiri na ndege?
 
Last edited by a moderator:
Wengine hatujawahi kupanda ndege,wakuu tunaomba mtujuze mapema mambo gani ya kuzingatia kabla ya kupanda,mfano vinavyopaswa kubebwa na visivyopaswa.
 
Ndgu secrete pole na hongera ya kupanda MADEGE ya maana mpaka SYDNEY ni hatua muhimu katika maisha pia. Sasa wewe ulikuwa muoga tu kutokuwasha simu ukiwa angani, walikataza tu pale wakati ndege inapaa. Usisahau kupiga picha wakati wa kurudi
 
andreakalima asikuambie mdege niliopanda kuanzia joburg mpaka Sydney unatisha kwanza una ghorofa, mavyakula ndo usiseme kila saa unaulizwa/unaletewa. Hakika wazungu wanafaidi
 
Mi izi za ndani dar- mwanza,kia,zanzibar,kigoma,katavi, na ndege zetu za kibongo na za jeshi zote,ombi langu wiki ijayo natarajia kusafi kupitia Dubai sina uzoefu na haya nadege makubwa, naomba kujua namna ya kutumia headphone, kulaza kiti kama ni tofauti na ndege zetu na kukunjua kimeza cha msosi kama ni tofauti ,,,,asante
 
Duh, sitasahau zile ngazi za lift pale JKNIA zilivyoniumbua, nilianguka alafu kuangalia kila mtu ananikodolea na pole zao nikaona kama za kinafiki wakati inawezekana walikuwa sincere, otherwise mambo mengine nilichukulia poa
 
ghona18 yaani we ukiingia kwnye ndeg kuwa mdadisi hasa kwa jirani yako (anachofanya na wewe fanya) maana vtu vingine hatuwezi kumaliza hapa JF.
 
Nina safari Mashariki ya mbali huko first time kupanda ndege kubwa huu uzi naufuatilia sana.
 
Hahahahahaha lol! Kama nakuona vile baada ya kupiga mueleka huku ukijikokota taratibu kuinuka na kuangalia kama kuna watu wamekuona jinsi ulivyopiga mueleka na kukuta kila mtu anakukudolea wewe lol!!!! Ukabaki unajibaraguza tu na kuendelea na zoezi lako 🙂🙂 la kuinuka.

Duh, sitasahau zile ngazi za lift pale JKNIA zilivyoniumbua, nilianguka alafu kuangalia kila mtu ananikodolea na pole zao nikaona kama za kinafiki wakati inawezekana walikuwa sincere, otherwise mambo mengine nilichukulia poa
 
Hahahahahaha lol! Kama nakuona vile baada ya kupiga mueleka huku ukijikokota taratibu kuinuka na kuangalia kama kuna watu wamekuona jinsi ulivyopiga mueleka na kukuta kila mtu anakukudolea wewe lol!!!! Ukabaki unajibaraguza tu na kuendelea na zoezi lako 🙂🙂 la kuinuka.

Acha kabisa, nilikuwa embarrassed balaaa, yaani nilihisi kila mtu alijua ni my first time
 
Ndege ni kitu cha ajabu pamoja na uzito wa watu na mabegi yao lakini inapaa juu
 
duuh mkuu ukachukua na wasindikizaji kwenye HIACE wewe ni nooma!!! Airport si watu walistuka sana
 
Mie nilipanda nikiwa na miaka 11 wakati naelekea China na Baba,sikuifaidi sana maana nilikuwa nacheza cheza tu na kusikiliza mziki.
 
Back
Top Bottom