Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Zanzibar haziendi ndege zinaenda hiace zenye mbawa
Ndege zinaenda Europe, Asia, mid East, America n.k
 
Kwani unaishi wapi mbona cku kupanda ndege kawaida sana mpaka JK kasema jana kwea fastjet kwenda mwanza au mbeya au Kilimanjaro katalii then rudi ulikotoka
 
Upande ndege ukienda wapi? Umemaliza shule? Umefika la ngapi.
 
Mkuu mimi hii ndege ya chini nilipanda kipindi kile ngorika inafukuzana na buffalo, gari za kwanza asubuhi. Wacha kabisa! Nilipofika korogwe nilishuka mwenyewe

Mkuu umenichekesha sana. Ila mimi nilikua naipenda sana Bufallo isee, yaani nikifunga shule nisipopanda bufallo sina raha, yaani bora hata nisimame. Sasa kuna siku nikapanda Kilimanjaro zile za miaka ile, isee lile roli ni noma.

Tumefika korogwe tumekula sasa tunatoka kuondoka konda anamwambia dereva, oya mnyama huyo anapita, ile Buffalo anapita jamaa kaingia lami, ebana eee mbona niliufarahia ule mtanange, nikatamani hata tusifike safari yetu.

Baada ya kabuku ndio tukaja kumpita jamaa tena kwa mbinde sana, maana yaliongozana kama sekunde kadhaa hivi hadi Buffalo akaachia tupite. Yaani nilikua sipandi gari ambayo haikimbii. Toka siku hiyo usafiri wangu ukawa kilimanjaro. Gari ambalo hatulipiti gari nyingine silipandi tena.
 
Shikamoo Fastjet ndo mlitutoa Gundu watu Wa nyanda za Juu Kusini hususani MBEYA
 
Nataarifiwa mbeya inaenda fastjet tu kwa sasa. Air Tanzania na Precision walishachemsha!!!
 
kuna haja ya kutoa/kupeana TIPS kuanzia unapoingia pale AIRPORT (madereva) jinsi ya kuminya kile kidubwana cha kuruhusu geti kufunguka/ Kuchukua tiketi, parking, kulipia parking, kuingia sasa kwenye ukaguzi wa awali, kucheck-in (kwa kutumia mashine, ATM pale uwanjani kwa baadhi ya ndege), ku-drop mizigo, kisha ishu za IMMIGRATION (international departure) ukaguzi wa pili na kisha kusubiria kukwea pipa
 
ha ha hizo pesa zitafutie tu album uziweke huko makumbusho ya kwamba uliendaga cameroon au kama vipi nenda pale airport ukiwakuta wale crew wa Ethiopian au KQ wape kama ikitokea wameenda huko wakazitumie
 
Ndugu Clasi hesabu hasara tu hapo maana hata ungekuwa na Naira za Nigeria kwa Bongo hamna bureau itazikibali mimi niliendaga Eritrea kurud na mihela yao hapa hakuna anayekubali nkisafirigi tena nikaenda Nairobi nao wananishangaa na hela hizo basi nikatia kwenye bahasha nikapelekea maharusi zawadi
 
Wiki ijayo naelekea dubai nitafaidije huko kwenye ndegeee
 
Back
Top Bottom