Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Hivi kwa pale Mwanza plan B yake kwa ndege kubwa ni wapi? Poleni sana. Mi naomba Mungu lisinitokee hilo
Plan B kwa ndege ndogo ni RUBONDO Airstrip (kisiwani), kwa ndege kubwa labda KIA ama Nairobi . Inshallah tuombe dua (CHATTLE INT'L AIRPORT iishe tutakimbilia huko.

**Halafu kukitokea hivyo marubani wa Fastjet (wengi Wageni/Wazungu si wazoefu) huvizia PW atue kwanza yeye ndo afuatie.
 
Siku ya kwanza kupanda ndege ilikuwa 2011, niliwahi kufika Airport nikielekea SA na Baadae Germany, Ushamba kitu kibaya sana niliachwa na ndege OR Tambo kwa kutokufuata maelekezo ya boarding gate, huwezi amini nililala Airport for one day before connecting to Frankfult
Nilipata tabu sana OR Tambo airport kwa kutojua sehemu nitakayokuta mzigo wangu! Hakika ushamba ni mzigo jamani! Nilidhani mzigo unachukua kama vile unavoshuka kwenye basi
 
Nilipata tabu sana OR Tambo airport kwa kutojua sehemu nitakayokuta mzigo wangu! Hakika ushamba ni mzigo jamani! Nilidhani mzigo unachukua kama vile unavoshuka kwenye basi
Nani alikuelekeza sasa ndugu? maana sipati picha umepanda zako Fastjet (Bei ya Promosheni) unafika South (OR Tambo) Macho yanavyokutoka ukisubiri mzigo wako
 
Plan B kwa ndege ndogo ni RUBONDO Airstrip (kisiwani), kwa ndege kubwa labda KIA ama Nairobi . Inshallah tuombe dua (CHATTLE INT'L AIRPORT iishe tutakimbilia huko.

**Halafu kukitokea hivyo marubani wa Fastjet (wengi Wageni/Wazungu si wazoefu) huvizia PW atue kwanza yeye ndo afuatie.
Huo ni udhaifu mkubwa sana kwa hao marubani. Vipi kama Siku hiyo wakiwa wenyewe. Si yatakuwa majanga
 
Nani alikuelekeza sasa ndugu? maana sipati picha umepanda zako Fastjet (Bei ya Promosheni) unafika South (OR Tambo) Macho yanavyokutoka ukisubiri mzigo wako
Acha tu ndugu yangu, niliona kila abiria yupo busy na mishe zake, hakuna hata wa kumuuliza, Ilibidi niende kwenye madirisha ya ku check in kuuliza mzigo wangu nitaupata wapi. Niliuliza kwa kiingereza cha Kiswanglish mkuu si unajua tena.
 
Plan B kwa ndege ndogo ni RUBONDO Airstrip (kisiwani), kwa ndege kubwa labda KIA ama Nairobi . Inshallah tuombe dua (CHATTLE INT'L AIRPORT iishe tutakimbilia huko.

**Halafu kukitokea hivyo marubani wa Fastjet (wengi Wageni/Wazungu si wazoefu) huvizia PW atue kwanza yeye ndo afuatie.
Uko sahihi! namiss sana kisiwa kile!
 
Huo ni udhaifu mkubwa sana kwa hao marubani. Vipi kama Siku hiyo wakiwa wenyewe. Si yatakuwa majanga
Siku kama hawajatangulizana na PW na yakitokea hayo naona kama na wese nalo limeisha (maana nasikia hao marubani wa ki-south) hawajazi mafuta nje ya dar, kwa Tanzania. naona watalingurumisha kwa mzee wetu pale mitaa ya kati (Jina kapuni).
 
Acha tu ndugu yangu, niliona kila abiria yupo busy na mishe zake, hakuna hata wa kumuuliza, Ilibidi niende kwenye madirisha ya ku check in kuuliza mzigo wangu nitaupata wapi. Niliuliza kwa kiingereza cha Kiswanglish mkuu si unajua tena.
Ila pamoja na kwamba ulitumia kiingereza chenye asili ya kemia si ulieleweka? Pole ndugu, mimi hapo OR Tambo nusura niibue (Taxi dreva) ziggo lina wezere la maana anadai ananijua sijui nimetokea zimbabwe. Nikamuona huyu mwizi, aliponimaliza alikuwa anataka 300 USD/night. ila so far, South ni pazuri kuzidi hata Dubai kwa shopping zetu wa kuunga unga na hoteli pia+VISA FREE.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.

Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.

Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.

Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.

Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
U made my day,..namna vile ulikuwa unakula.....vingine ni viambata ila ukala kivyakevyake utimize lengo...nimecheka sana
 
PRECISION AIR ilitetereka tukitua mwanza kwa ajili ya mvua ilikuwa inanyesha nikamkumbuka mwanangu wa miaka 2 atakavyoishi bila baba (Yatima), Aisee, ndege tuzione angani tu.
 
Mie mara ya kwanza kupanda ndege nilitoka Dsm kwenda Mwanza. Process nzima hadi niingie kwenye ndege ilikuwa 'shughuli'. Nilikaa upande wa dirishani, tulipopita Ngorongoro crater eti sikuthubutu kuchungulia nje. Kisa? Niliogopa eti nikichungulia naegemea upande mmoja hivyo nikaona kama vile ndege italalia upande ule na kuanguka! Ama kweli ushamba ni kazi!
Nisaidie hii Process hatua moja Hadi nyingine jmatatu ndo naenda kuanza
 
Ndege za Middle East ndo zenye starehe Zaidi safarini. Hususani ETIHAD
 
  • Thanks
Reactions: SDG
402e48432f8aa18d8cf38e3dc4764ced.jpg
[emoji2][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom