Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Tar 16.10.2017 nlifika airport ya songwe mbeya mapeeemaa sna badae tukapewa taarifa ndege haitoondoka siku hiyo nikaisi ndo tayar shetan anafny yake gundu liendelee kuniganda baati nzur tulipelekwa hotel thn 17.10.2017 nilipanda ndeg kwa Mara ya kwanz ni raha sanaaaa kalikua ka lisaaa tuuu[emoji1][emoji1][emoji1] ntapand tena
 
Sitasahau siku bombardier imeteleza hapo angani nilitokaje kajasho kidg nife na presha[emoji28][emoji28][emoji1][emoji1]
 
bukoba -mwanza.....vile vindege vidogo...hiyo siku kulikuwa na mvua sana asubuhi..wakati tunaingia kwenye ndege tukaambiwa tuzime simu zetu ila kuna watu nikawaona wanaendelea kutumia simu wakiwa ndani kabla hatujaondoka...ile tunaondoka tu airport kandege kakaanza kuyumba yumba mara pailot akarudia tangazo watu wote wazime simu...mimi simu yangu nilitoa na betri kabisaaaa..
Hahaha
 
Mimi ilikuwa 1999,uelekeo nairobi, mke wangu akaniambia kwa uzoefu aliohadithiwa na babaake huko hewani mtu lazima usikie njaa sana,akaniandalia hotpot la makande, nasikitika sana maana lilibakia airport,kipindi hicho hakuna vifaa vizuri vya ku-detect madawa,kwa hiyo wakayafananisha na madawa!!! Ushamba gunia la misumari, unarekebisha mmoja, tisa inakuchoma!!!
Hahahaha
 
Mie mbona sitasahau,,,,,,,,,,
cku iyo nilijipodoa kama naenda harusini kufika airport parfume yng ikawekwa kwny dustibini niliumia sana.............
nilipoingia ndani sijui ni uoga nikaita air host aje kunifunga mkanda kasheshe wkt wa kushuka mkanda ukanishinda kufungua ikabidi jirani yng kk mmoja anisaidie..
mbavu zangu
 
mimi ilikua 2014 dar to mbeya. Nilikua napiga kelele kua Ticket yangu Haina City No. kumbe unapewa City No. pindi napanda.
nilipopanda nikawa nakenua meno kila mtu ananishangaa. alafu nilikua na viroba vya konyag
[emoji23][emoji23] we kiboko viroba
 
Dah! ndege ina speed jamani nilipanda AURIC AIR toka Njombe to Iringa ile naingia tu nasogea kwenye siti yangu ili nikae naambiwa "wa kushuka Iringa",nikadata nauliza wa kushuka Iringa mnamaanisha nini,yule kaka akasema tushafika Iringa,sikuonja hata siti ya ndege ikanibidi nishuke maana tuliisha fika Iringa,duh! ndege inakimbia jamani!
Kwan ndege inaweza ondoka kabla wengine hamjakaa na kufunga mikanda????
 
kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyng baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"
hahahaa
 
Back
Top Bottom