Virusi vya corona: Anna Mghwira atangaza malori ya Kenya kutovuka mpaka wa Tanzania wa Holili

Virusi vya corona: Anna Mghwira atangaza malori ya Kenya kutovuka mpaka wa Tanzania wa Holili

Nchi yenye ombwe la uongozi hili ni kawaida. Yoyote anaweza KUROPOKA chochote hata kama hana mamlaka husika.

Swala la mpaka limekuwa na mkoa tena? Hili swala zito, ndio maana hata wenzetu ni Rais ndio katangaza. Mama kashapona Korona huyu au karudi kazini mapema kabla ya wakati?
 
Mama yupo sawa kabisa. Kama Kenya wesha kataa magari kuingia au kutoka hayo malori yatatokea wapi kuja Tz ka sio kwa njia za panya? Huko ndio uambukizi umejaa hivyo hatuyataki hayo malori.

Tena amesema; Kama umepewa ruhusa na Kenya kuingiza huo mzigo wako basi pokelea pale mpakani uchukue lory la Tz likubebee mzigo wako. Hebu jaribu kufikiri; Sisi haturuhusiwi kuingia tena Kenya, ila wao waingie tu kwetu kujifanyia lolote watakalo
 
Kama Kenya wakifunga mpaka tusiruhusu magari kuingia Tanzania.
 
Ummy Mwalimi si keshakanusha hii taarifa.

Sent From Galaxy S20 Ultra
 
Soon huyu atatumbuliwa,kwanza alijitangaza ana corona,pili hafuati njia ya mkuu wa nchi,kwa picha ninayoiona hatadumu
Hatumbuliwi MTU ameshapewa maagizo afunge mpaka magari ya Kenya yasiingie Tanzania.
 
Kuna ajabu gani sisi kufunga mipaka? wao wafunge nyie msifunge huo ni ujinga, piga ban kila kitu kisimame kila mtu akae kwenye nchi yake, mnazunguka as if Kenya ni G8.
 
Hiyo ni habari ya kutoka kwa Magufuli kwenda kwa RCs wa Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Arusha. Ummy aliikanusha maana haimuhusu yeye. Ni kama hasira hivi ya kulipa kisasi.
Wakenya ndiyo walianza Kenyatta amefunga mpaka unataka sisi tusifunge waendelee kuja tu. No way jino kwa jino!
 
Panadol tunatengeneza hapa hapa TZ zipo. Blue Band siyo muhimu sana lakini tuna product kama hizo zinatoka SA.
Na hili la sisi kuingiza bidhaa kutoka SA linawauma roho kweli.....manyang'au ni watu wa kuogopa kama ukoma maana hawaaminiki...
 
Tabia za kiongozi wetu zinaonekana kwenye hayo matamshi, naamini yeye ndie atakuwa amewaagiza hao "subordinates" wake wazuie hayo malori.

Halafu akiwa anahutubia kanisani anaonekana mnyenyekevu, kumbe moyoni amejaa kisasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu nawe uwe unaelewa! Kenyatta jana ametangaza wanafunga mpaka na Tanzania sasa ulitaka sisi tuwabembeleze kwa lipi?
 
Naona wanaleta trade war eeee?

Mawe kuna moto anautafuta!
Wakenya hawatutishi kabisa tunawamudu sana tu na kuanzia kesho tunaanza kuwaorodhesha wote walioko TZ ili ikibidi tuwarudishe kwao. Jino kwa jino hawawezi kutufundisha jinsi ya kushughulikia corona nchini mwetu.
 
Back
Top Bottom