Virusi vya corona: Rais wa Madagascar Rajoelina amewashutumu wakosoaji wa dawa ya mitishamba

Wahenga walisema "Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha"
Siku hizi hadi Afrika kuna Mabeberu...
Viongozi wenye mihemko, wafuata mkumbo akina Zitto Kabwe na wenzie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni dawa zipi za MITISHAMBA huku Afrika zinapitia taratibu za kisayansi? Mbona huwa ni vyakula vya asili tu ambavyo wala havina side effects kwa mwanadamu tofauti na hayo mafansidar ambayo ni makemikali ya viwandani?

Tatizo ni pale mnapoleta vigezo vya kisayansi kwa mitishamba ambayo ni asili pure. Ni sawa na kumlazimisha samaki aishi nchi kavu kama kigezo kikuu. Naunga mkono hoja ya Andy
Mkuu unajuwa matumizi ya mdalasini,ukichanganya na soya na kitunguu swaumu inashusha sana presa unaweza kufa usipojua kipimo sahihi?

Unajuwa matumizi ya kahawa kupiuta kiasi hupandisha presha?

Unajuwa matumizi holela ya juisi ya aloe vera mbichi unaweza kupata saratani kama ukizidisha matumizi?

Unajuwa kuna majani yakikugusa tu unaweza kufa kwa sumu yake? Fuatilia Poison ivy, poison oak, na poison sumac.

Unajuwa ndizi mbivu au nanasi ukichanganya kwenye juice ya matunda flani ni sumu inaweza kuuwa kirahisi hasa watoto?

Unajuwa mihogo pori flani ina sumu kali na mbaya ya cyanide inayoweza kuuwa familia nzima au kijiji kizima wakila muogo au uji wa muogo au ugali wa muogo huu?

Kuna majani wanaweka kwenye mshale au mkuki ambao ukimkwaruza tu mnyama hafiki umbali wa mita 100 anakufa.

Kwahivyo dawa kutokana na mimea au vyakula siyo kigezo cha kutokuwa na madhara kwa binadamu. Kuna watu wana allergy(mzio) na maziwa ya ng'ombe, karanga au samaki kiasi kwamba akila au kunywa tu anaweza kukosa pumzi au akashikwa homa kali na kufa kama asipopewa dawa ya allergy haraka.

Haya madhara ndiyo yanayo fanyiwa uchunguzi na majaribio kwenye tafiti za hatua ya kuidhinisha matumizi ya dawa flani.
 
Mkuu, Wangapi wamekufa tangu zigunduliwe dawa hizo? Hebu tuongee uhalisia na sio "unaweza." Hiki nikisemacho sio jambo jipya Afrika mkuu.

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Mkuu unaongea kama haujui tabia za waafrika.
Watu wengi wakifa ghafla baada ya kunywa au kula kitu ndugu wanasema kalogwa, hata maiti ikifanyiwa uchunguzi hospital ikaonekana mtu kafa sababu amekula sumu ni vigumu kuamini sababu ni mchanganyiko flani wa juisi ya matunda yasiyofaa kuchanganywa.

Unafikiri mbongo anae umwa saratani iliyotokana na kula sumu ya kuvu atahisi chanzo karanga mbovu au mahindi yaliyo oza au mchele ulioshika ukungu ambao alikula miaka zaidi ya saba au mitano iliyopita?

Mkuu kama umehudhuria clinic ya watoto ndani ya miaka 10 ya karibuni? Wanashauri watoto wasipewe lishe ya karanga kama enzi zetu sababu ya allergy na sumu ya ukungu inayo sababisha saratani.
Hii imekuja kugunduliwa miaka ya karibuni wakati zamani ndiyo wazazi wetu walikuwa wanalazimishwa waweke karanga kwenye lishe ya mtoto.

Sasa hivi madaktari wengi wa watoto wanashauri mtoto apewe maziwa ya formula na asipewe maziwa ya ng'ombe sababu kuna protin flani ambayo inasumbua watoto wengi tu, na bahati mbaya ngumu sana kujuwa mtoto anapata shida flani sababu ya maziwa ya ng'ombe unayompa.

Hiyo shida ya soya, cinamon na garlic kushusha presha mimi mwenyewe ni victim karibu iniue mwaka 2006, nilipewa na dada yangu mmoja nitumie kila siku kwenye chai kutibu ulcers. Nilidondoka chooni jua linawaka mchana kabisa baada ya kuitumia kwa vurugu siku kumi na kitu. Kumbe nilitakiwa nipewe maelekezo vizuri jinsi ya kuitumia na tahadhari za madhara yake.

Sasa ningekuwa naamini majini na uchawi si ningesema nilipigwa na jini huko chooni kama wengi wanavyo husianisha na vifo vya kuanguka chooni? Kwa vile mimi mdadisi nikajua chanzo hiyo dawa nikaacha na shida ikaisha haikujirudia tena.
 
unaelewesha vizuri sana mkuu.
Nimekuelewa kuwa huenda hiyo dawa ya mad ikawa na side effect ila isijulikane kwasasa. ni kweli tuwe makini sana
 
Mkuu watu wanakunywa pombe miaka nenda rudi na side effect ipo,hapo ni suala la kuokoa maisha ya watu,WHO kwanini basi wasilete hiyo yao waliyogundua ?mtu anachofanya ni kwamba apone ,kwahiyo ujiangalie unakufa wakati WHO bado hawajagundua dawa.
Issue sio kutoka Africa mkuu issue imefuata taratibu za dawa kuweza kutumika kwenye mass.
Dawa kabla hajaidhinishwa kutumika kwa binadamu inapitia ktk phase mbalimbali so ikifuzu ndo inaruhusiwa kutumika kwa binadamu ten kwa kuangalia side effects za dawa kama binadamu anaweza tolerate izo side effects.

Dawa ya madagascar kupigwa vita ni sahihi hata km dawa iyo ingegundulika ndan white house,so ugunduzi wa dawa lazim ufuate international standards ili itumike otherwise tutaendelea kuua figo na maini due to toxicity of drug ambazo hazijaidhinishwa.
 
Madagascar ina maambukizi na siyo wagonjwa ,na hiyo siyo chanjo ni dawa
Sasa shida yake ni nini? Wao hawakatai wanahitaji uthinitisho wa kisayansi, hakuna dawa inayoitwa dawa pasipo uthibitisho yeye awapelekee tu uthibitisho au ametumia hisia tu na macho? Kaona watu wamepewa baada ya muda wamepona kasema hiii dawa ndio imewaponya, na Kama imewaponya hiyo dawa mbona ana idadi kubwa ya wagonjwa kuliko hata Uganda? Wewe una dawa halafu una wagonjwa wengi kuliko nchi nyingi za Africa huo tunaita ni uchuro
 
Mbona tunapenda kuwa wababaishaji sana bila sababu?

Tuifanyie majaribio , tatizo liko wapi?
 
Mkuu unaongea kama haujui tabia za waafrika.
Watu wengi wakifa ghafla baada ya kunywa au kula kitu ndugu wanasema kalogwa, hata maiti ikifanyiwa uchunguzi hospital ikaonekana mtu kafa sababu amekula sumu ni vigumu kuamini sababu ni mchanganyiko flani wa juisi ya matunda yasiyofaa kuchanganywa.

Unafikiri mbongo anae umwa saratani iliyotokana na kula sumu ya kuvu atahisi chanzo karanga mbovu au mahindi yaliyo oza au mchele ulioshika ukungu ambao alikula miaka zaidi ya saba au mitano iliyopita?

Mkuu kama umehudhuria clinic ya watoto ndani ya miaka 10 ya karibuni? Wanashauri watoto wasipewe lishe ya karanga kama enzi zetu sababu ya allergy na sumu ya ukungu inayo sababisha saratani.
Hii imekuja kugunduliwa miaka ya karibuni wakati zamani ndiyo wazazi wetu walikuwa wanalazimishwa waweke karanga kwenye lishe ya mtoto.

Sasa hivi madaktari wengi wa watoto wanashauri mtoto apewe maziwa ya formula na asipewe maziwa ya ng'ombe sababu kuna protin flani ambayo inasumbua watoto wengi tu, na bahati mbaya ngumu sana kujuwa mtoto anapata shida flani sababu ya maziwa ya ng'ombe unayompa.

Hiyo shida ya soya, cinamon na garlic kushusha presha mimi mwenyewe ni victim karibu iniue mwaka 2006, nilipewa na dada yangu mmoja nitumie kila siku kwenye chai kutibu ulcers. Nilidondoka chooni jua linawaka mchana kabisa baada ya kuitumia kwa vurugu siku kumi na kitu. Kumbe nilitakiwa nipewe maelekezo vizuri jinsi ya kuitumia na tahadhari za madhara yake.

Sasa ningekuwa naamini majini na uchawi si ningesema nilipigwa na jini huko chooni kama wengi wanavyo husianisha na vifo vya kuanguka chooni? Kwa vile mimi mdadisi nikajua chanzo hiyo dawa nikaacha na shida ikaisha haikujirudia tena.
Ni kizazi hiki kinaweza kudhania hayo kwani watu wanaelekezana kutumia mchanganyiko wa madawa alimradi tu KISAYANSI yaweza kuwa tiba. Lakini kwa mwenye umri mkubwa atajua watu walitumia sana tu hizo tiba mbadala kuanzia utotoni na leo hii binafsi sijawahi kushuhudia hayo madhara unayoyasema katika umri huu

Ninachosrma, hizi tiba sio kitu kigeni kwangu, bali kigeni ni perception. Sio kila mtu anaweza kuchukua miti akachanganya kupata dawa kwani ipo yenye sumu pia. Ndio maana kuna wataalam wa tiba asilia pia. Hiyo ni field inayojitegemea lakini ukweli ni kuwa iko juu mno kuliko sayansi katika baadhi ya magonjwa, hasa yanayoitwa SUGU yasiyo na tiba kisayansi.

Lakini pia, licha ya maendeleo ya sayansi, wako watu wengi sana wamekufa ama kulemaa kutokana na matumizi ya dawa BORA za kisayansi. Unalijua hilo? Katika miti shamba madgara yanakuwepo masharti yake yasipozingatiwa. Nakupa mfano, iko tiba ya mifupa ilitumika sana usukumani kwa aliyevunjika. Tabibu alijipaka dawa kisha kusogeza mikono jirani na eneo lililovunjika BILA KUGUSA mwili na mifupa ikakaa sawa. Sasa kama dawa ikigusa mwili mguu ulioza.

Hoja yangu si kubeza sayansi, bali ni kushangaa nia njema ya sayansi kwa sasa wakati tiba hizi zipo karne na karne. Ingia youtube tafuta Dr. Seba uone alifsnya nini na sababu ya kifo chake ni nini.

Asante

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Issue sio kutoka Africa mkuu issue imefuata taratibu za dawa kuweza kutumika kwenye mass.
Dawa kabla hajaidhinishwa kutumika kwa binadamu inapitia ktk phase mbalimbali so ikifuzu ndo inaruhusiwa kutumika kwa binadamu ten kwa kuangalia side effects za dawa kama binadamu anaweza tolerate izo side effects.

Dawa ya madagascar kupigwa vita ni sahihi hata km dawa iyo ingegundulika ndan white house,so ugunduzi wa dawa lazim ufuate international standards ili itumike otherwise tutaendelea kuua figo na maini due to toxicity of drug ambazo hazijaidhinishwa.
Yaani unataka kusema miti dawa ithibitishwe na sayansi dawa?

Eleweni haitatokea hata siku moja daktari wa binadamu akakubali dawa mitii, ndio maana wapo wanaoamini kuwa HAKUNA waganga wa kienyeji.

Wangapi wanavunjika miguu wanaambiwa kukatwa huko mahosptali ila miti dawa inawaponya?

Acheni uzungu wa ajabu nyie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nacho jiuliza hawa watu wanaotetea miti shamba ambayo haijathibitishwa kama inatibu. Wakiuguwa magonjwa kama malaria, typhoid, pneumonia, TB, ameoba nk. Wanakunywaga miti shamba au Wana kwenda hospitali? Ndio si katai miti shamba inatibu lakini ni vizuri ifanyiwe utafiti ili kupata uhakika kama dawa nyingine. WHO wameweka standard procedures ili kuepuka madhara ya muda mfupi na mrefu pia. Naamini 100% wote hawa wanaotetea miti shamba wanatumia dawa za hospitali, tusiwe wanafkii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Andry Rajoelina

Bwana Rajoelina anasema kwamba taifa la Ulaya lingekuwa limetenegenza dawa hiyo, majibu ya mataifa ya magharibu yangekuwa tofauti

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amesema kwamba wakosoaji wa dawa ya mitishamba ambayo haijajaribiwa ambayo anaipigia debe kuwa tiba ya Covid-19 inaonyesha tabia ya ubwenyenye ya mataifa ya Magharbi dhidi ya Afrika.

Shirika la Afya duniani limeonya dhidi ya kutumia dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio. Dawa hiyo ya rais Rajoelina haijapitia majaribio ya wanadamu.

Muungano wa Afrika pia umesema kwamba inataka kuona data ya kisayansi kuhusu uwezo na usalama wa dawa hiyo kwa jina Covid-Organics.

''Iwapo ingekuwa ni taifa la Ulaya ambalo liligundua dawa hiyo , je kungekuwa na wasiwasi? sidhani'', bwana Rajoelina alisema katika mahojiano na shirika la habari la ufaransa 24.

Madagascar imeripoti wagonjwa 193 wa Covid-19 na hakuna kifo hata kimoja. Dawa hiyo ilifanyiwa majaribio watu 20 katika kipindi cha wiki tatu, mshauri wa rais huyo aliambia BBC wakati bidhaa hiyo ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita - hatua ambayo haiendani na muongozo wa WHO kuhusu majaribio.

WHO inasema kwamba vipimo na utafutaji wa watu waliokaribiana na wagonjwa ndio njia bora ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Licha ya madai hayo , mataifa kadhaa ya bara Afrika ikiwemo Nigeria, Guinea-Bissau, Equitorial Guinea na Liberia , tayari yameagiza dawa hiyo inayozalishwa kutoka kwa mmea wa pakanga - mti unaotumiwa kutengeneza dawa ya malaria pamoja na miti mingine ya Malagasy.

WHO imesema kwamba Waafrika wanahitaji kupata dawa ambayo imepitia majaribio ya kuridhisha hata iwapo inatoka katika tiba za kitamaduni.

Katika mahojiano hayo ya runinga, bwana Rajoelina alisema wanasayansi wa Afrika hawafai kudharauliwa.

Lakini kuna ushahidi kuonyesha kwamba dawa ya Covid-Organic ina uwezo.

'Dawa ya Madagascar inakataliwa kwa kuwa inatoka Afrika '
😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Attachments

  • IMG-20200514-WA0002.jpg
    IMG-20200514-WA0002.jpg
    84.7 KB · Views: 10
Issue sio kutoka Africa mkuu issue imefuata taratibu za dawa kuweza kutumika kwenye mass.
Dawa kabla hajaidhinishwa kutumika kwa binadamu inapitia ktk phase mbalimbali so ikifuzu ndo inaruhusiwa kutumika kwa binadamu ten kwa kuangalia side effects za dawa kama binadamu anaweza tolerate izo side effects.

Dawa ya madagascar kupigwa vita ni sahihi hata km dawa iyo ingegundulika ndan white house,so ugunduzi wa dawa lazim ufuate international standards ili itumike otherwise tutaendelea kuua figo na maini due to toxicity of drug ambazo hazijaidhinishwa.
babu zetu dawa zao zilipitia phases gani ?na walijitibu kwa mafanikio kuliko midawa yao inayopitia phases unazozitaka. Hivi hadi sasa unadhani kuna mzungu anakuwazia mema mwafrica.Subiri uugue/uuguliwe utaomba hata mbichi.
 
Andry Rajoelina

Bwana Rajoelina anasema kwamba taifa la Ulaya lingekuwa limetenegenza dawa hiyo, majibu ya mataifa ya magharibu yangekuwa tofauti

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amesema kwamba wakosoaji wa dawa ya mitishamba ambayo haijajaribiwa ambayo anaipigia debe kuwa tiba ya Covid-19 inaonyesha tabia ya ubwenyenye ya mataifa ya Magharbi dhidi ya Afrika.

Shirika la Afya duniani limeonya dhidi ya kutumia dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio. Dawa hiyo ya rais Rajoelina haijapitia majaribio ya wanadamu.

Muungano wa Afrika pia umesema kwamba inataka kuona data ya kisayansi kuhusu uwezo na usalama wa dawa hiyo kwa jina Covid-Organics.

''Iwapo ingekuwa ni taifa la Ulaya ambalo liligundua dawa hiyo , je kungekuwa na wasiwasi? sidhani'', bwana Rajoelina alisema katika mahojiano na shirika la habari la ufaransa 24.

Madagascar imeripoti wagonjwa 193 wa Covid-19 na hakuna kifo hata kimoja. Dawa hiyo ilifanyiwa majaribio watu 20 katika kipindi cha wiki tatu, mshauri wa rais huyo aliambia BBC wakati bidhaa hiyo ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita - hatua ambayo haiendani na muongozo wa WHO kuhusu majaribio.

WHO inasema kwamba vipimo na utafutaji wa watu waliokaribiana na wagonjwa ndio njia bora ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

WHO inasema kwamba vipimo na utafutaji wa watu waliokaribiana na wagonjwa ndio njia bora ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Licha ya madai hayo , mataifa kadhaa ya bara Afrika ikiwemo Nigeria, Guinea-Bissau, Equitorial Guinea na Liberia , tayari yameagiza dawa hiyo inayozalishwa kutoka kwa mmea wa pakanga - mti unaotumiwa kutengeneza dawa ya malaria pamoja na miti mingine ya Malagasy.

WHO imesema kwamba Waafrika wanahitaji kupata dawa ambayo imepitia majaribio ya kuridhisha hata iwapo inatoka katika tiba za kitamaduni.

Katika mahojiano hayo ya runinga, bwana Rajoelina alisema wanasayansi wa Afrika hawafai kudharauliwa.

Lakini kuna ushahidi kuonyesha kwamba dawa ya Covid-Organic ina uwezo.

'Dawa ya Madagascar inakataliwa kwa kuwa inatoka Afrika '

Rajoelina ni KICHAA kabisa!
 
Back
Top Bottom