Virusi vya Corona vinakufa kwenye miale ya jua hivyo basi msimu wa kiangazi Corona itatoweka?

Virusi vya Corona vinakufa kwenye miale ya jua hivyo basi msimu wa kiangazi Corona itatoweka?

Corticopontine

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2019
Posts
677
Reaction score
1,326
Mwanasayansi mmoja nchini Marekani leo Aprili 24 ameeleza kuwa virusi vya corona vinaharibiwa kiurahisi na na miale ya jua hivyo kuna matumani makubwa ya ugonjwa huo (Covid-19) unaoitesa dunai ukaisha wakati wa kiangazi.

hata hivyo tayari Shirika la Afya Duniani WHO lilisema mwanzoni mwa mwezi Aprili kwamba kukaa juani ama katika sehemu zenye joto jingi la zaidi ya nyuzi 25 hakuzuii kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Mwanasayansi mwandamizi katika taifa la Marekani William Bryan ambaye ni mshauri wa masuala ya afya katika Serikali ya Bwana Donald Trump amewaeleza waandishi wa habari kulingana na utafiti uliofanyika huenda maambukizi ya corona yakapungua au kukoma wakati wa kiangazi.

“Utafiti wetu wa kuvia sana ni kuwa miale ya jua inaonekana kuua virusi vya corona waliopo mahali na waliopo hewani, kuongezeka kwa joto na unyevunyevu vyote vimekuwa na athari mbaya kwa ukuaji wa virusi vya corona,” amesema Bryan wakati akizungumza katika ikulu ya Marekani.

Hata hivyo utafiti huo haujawekwa kwa umma ili kuruhusu watalaamu huru nao kutoa mawazo yao lakini duru za sayansi zinaeleza kuwa kuna uhusiano mkubwa wa virusi hivyo kuuliwa na mionzi lakini hakuna uthibitisho kama mionzi iliyotumika ni sawa na ile inatokana na jua wakati wa kiangazi.
 
Mleta mada labda kama unaishi mkoani; lakini kama upo Dar ambapo rate ya maambukizi ishanoga nakuhakikishia kwa 100% utaacha ku post huu upuuzi wako sio muda mrefu wewe mwenyewe bila kuombwa na mtu kwa kile utakachokua unakiona kama wewe mwenyewe akitokukuta.

Nakupa week 3 ukipost nitag sema kilatha (ahadi pale pale kwa muhusika).
 
Kw
Mleta mada labda kama unaishi mkoani; lakini kama upo Dar ambapo rate ya maambukizi ishanoga nakuhakikishia kwa 100% utaacha ku post huu upuuzi wako sio muda mrefu wewe mwenyewe bila kuombwa na mtu kwa kile utakachokua unakiona kama wewe mwenyewe akitokukuta.

Nakupa week 3 ukipost nitag sema kilatha nipe £100 yangu; hilo ni deni najipa.
Kwani huu msimu wa kiangazi? Huoni hata maambukizi ya DSM yameongezeka wakati wa mvua hizi zinazonyesha??;
 
Kw

Kwani huu msimu wa kiangazi? Huoni hata maambukizi ya DSM yameongezeka wakati wa mvua hizi zinazonyesha??;
Nimekupa week 3 zaidi halafu Corona hana adabu anaua watu maskini zaidi ambao miili yao dhaifu kwa nchi ambao hilo kundi limejaa subiri mziki ndio una changanya.
 
Mleta mada labda kama unaishi mkoani; lakini kama upo Dar ambapo rate ya maambukizi ishanoga nakuhakikishia kwa 100% utaacha ku post huu upuuzi wako sio muda mrefu wewe mwenyewe bila kuombwa na mtu kwa kile utakachokua unakiona kama wewe mwenyewe akitokukuta.

Nakupa week 3 ukipost nitag sema kilatha nipe £100 yangu; hilo ni deni najipa.
Umesahau kwamba maambukizi yameshamiri wakati huu wa mvua mbona hautumii akili? Unaambiwa wakati wa kiangazi siamini kama jamii Forum ina vilaza wasioelewa kama ww
 
Nimekupa week 3 zaidi halafu Corona hana adabu anaua watu maskini zaidi ambao miili yao dhaifu kwa nchi ambao hilo kundi limejaa subiri mziki ndio una changanya.
Wiki tatu hizi ni kuanzia tarehe ngapi hadi tarehe ngapi,maana naona kila wiki zinabaki wiki tatu.
Hapo weka wazi ili hiyo aisje akakosa bure,si unajua watu wanatambika.
 
Mbona huku kwetu tunaogelea kwenye jua na maambukizi ni 500%
Sio kweli wanaoambukiza na washinda kwenye magari na maofisi yenye air condition washinda juani corona Haina mpango nao ikisogelea inakutana na Moto inatimua mbio yenyewetu wa Moto utafikiri kaipuliwa kwenye chungu Cha Moto
 
Sio kweli wanaoambukiza na washinda kwenye magari na maofisi yenye air condition washinda juani corona Haina mpango nao
Kwa hiyo Corona inaweza ikawa haina mpango je wakati wa magharibi na usiku jua hakuna ina maana virusi navyo huwa vinalala?
 
Back
Top Bottom