jamani nafikiri NN maelezo yake yanaeleweka, cha kuongeza hizi ni shared network kwa ngazi ya dunia, ila zipo za kwa nchi kama vile ken-switch kenya,Zim-switch Zimbabwe, umoja-switch -TZ (bahati mbaya hatuna national switch inayounganisha mabenk yote -TZ). ili card yoyote iweze kutumika kwenye ATM au POS n.k, lazima kadi hiyo iwe imerusiwa kutumika hapo, ndo maana unaweza kuta ATM ina visa au Mastercard au vyote (na mitando mingineo kama Europay), kama wewe kadi yako ni ya visa lazima utumia kwa ATM ambayo ina-support visa kadhalika kwa mastercard lazima hiyo ATM iwe ina-support mastercard au vyote.
kinachotoke mabenki yenye ATMs yanakuwa na connection kwenda kwenye mtando husika(Visa/mastercard). Anapokuja Mteja wa benk A mfano mwenye Visa card kwa ATM ya benk B (zote ziko Visa) transaction hii upelekwa visa na bank B, then Visa, watajua hii card ni mteja Benk A, wataipeleka huko kwa ajiri ya kuangalia balance kama inatosha kutokana na kiwango mteja alichoomba, then response hurudi kwa style hiyohiyo hadi kwenye ATM na kutoa pesa. vinginevyo utaambiwa kadi yako haitabuliki.
kuna aina ya transactions kama 3 (on-us,not-on-us na remote-on-us)
on-us = inamaanisha ATM yako mteja wako (kwa kawaida gharama huwa ndogo)
not-on-us = ATM yako Mteja si wako (hivyo basi km ni visa/mastercard unawasukimizia huko waangaike nayo) gharama iko juu kidogo kulipa mwenye ATM, mwenye card na visa
remote-on-us=ATM si yako bali Mteja ni wako
kwa kuangilia trx hizo mwisho wa siku mabenki huweza kurudishiana fedha walizo chukuwa wateja wao (net figure) tofauti ya unachodai na unachodaiwa