Chief nimeifuatilia story yako, inazidi nipa reflection ya mambo kadhaa ambayo nimekutana nayo kupitia (kwa waganga ambao nimeshatembelea kwao), watu niliofamiana nao in the course of life na wanawake [ni mmoja hasa] niliyekuwa naye. Huyu mwanamke alinifumbua macho kwa mambo mengi ya kusaka utajiri huko ziwa tanganyika. Noti alikuwa nayo hasa, licha ya kuwa alikua akinipenda na sometimes kunipiga tafu sana financially maana by that time nilikua broke, niliamua kuachana nae baada ya kuniletea story za maagano kati yangu na yeye [hiki ni kitu kibaya sana], ingawa haikuwa rahisi kuachana nae.
pia nilipokuwa university, kuna jambo lilitokea likanilazimu niwe na lala ghetto kwa jamaa yangu. Yule jamaa alikuwa na ghetto kama lile aliloimba ngwea. Kilichonishangaza jamaa alikuwa analala chini. Nimepoa pale geto siku tatu, ikabidi nijikatae nitafute kigesti hausi nipoe kwa muda, mishe za yule mkigoma nilikua sizielewi. Huwezi kuwa tajiri kama huna roho ngumu.