Vishkwambi sita kwa walimu zaidi ya 20, nini maana yake?

Vishkwambi sita kwa walimu zaidi ya 20, nini maana yake?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Inawezekana ni kweli wana nia ya dhati kuwawezesha walimu katika TEHAMA, lakini kwa ugawaji huu haitasababisha mgawanyiko au upendeleo?

Naona shule x leo wamegawiwa walimu watano na mkuu wa shule!

Je, ni sawa?
 
Ungetusaidia kuongeza nyama kwenye uzi labda tungejua namna ya kuchangia, hata hivyo vishikwambi kama havitoshi hakuna namna yakuweza kugawiwa kwa kila mwalimu.

Pole sana, next time kitapita kwako wala usihofu, mchanganuo ukikaa sawa kitakufikia
 
Inawezekana ni kweli wana nia ya dhati kuwawezesha walimu katika tehama, lakini kwa ugawaji huu haitasababisha mgawanyiko au upendeleo?
Naona shule x leo wamegawiwa walimu watano na mkuu wa shule!
Je, ni sawa?
fuatilia kwa mratibu Elimu ngazi zote ikishindikana fika kwa Afisa Elimu au hata DED, ninachojua tablet vimegaiwa kwa idadi kamili ya waalimu Tanzania. usikute vimegaiwa kwa wadada wa kazi wao huko majumbani!!
 
Walimu jiondoeni kwenye dhahama hizo kwa kujinunulia wenyewe. Hii itasababishwa msitukanwe
 
Hapana ni kwa walimu wachache.
Na kama ujuavyo walimu wengi ni waoga, hawawezi kuhoji!
Labda waandishi wa habari wasaidie kuhoji na kutoa takwimu sahihi
 
Hapana ni kwa walimu wachache.
Na kama ujuavyo walimu wengi ni waoga, hawawezi kuhoji!
Labda waandishi wa habari wasaidie kuhoji na kutoa takwimu sahihi
Kusubiri waandishi wa habari itawagharimu muda mrefu
 
Walitangaza sio kila mwalimu atapewa

Walimu wa masomo ya sanaa kishwambi hawapewi unless wawe na vyeo vya juu

Kama shule ina somo la ICT mwalimu wa hilo somo ana uhakika wa kupewa kishkwambi.

Mwalimu mkuu na mwalimu wa academic nae lazima apewe kishkwambi
 
Walimu jiondoeni kwenye dhahama hizo kwa kujinunulia wenyewe. Hii itasababishwa msitukanwe
Kwanini walimu? Mbona sekta nyingine wanapewa vitendea kazi na serikali na hawajawahi kutukanwa?
 
Back
Top Bottom