Vishkwambi walivyoahidiwa walimu vimeenda wapi?

Vishkwambi walivyoahidiwa walimu vimeenda wapi?

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,625
Reaction score
3,141
Vishkwambi walivyoahidiwa walimu kupata vimepotelea wapi.

Ingekuwa Enzi za JPM:-
(1) Vishkwambi vingekuwa vilishasambazwa muda mrefu.

(2) Hakuna Kishkwambi hata kimoja ambacho kingekwapuliwa kama ilifanyika sasa.
 
Kamfufue basi au kazikwe nae usione yanayoendelea
Hata wewe utazikwa tu muda wako ukifika usiweze, tena yeye alizikwa akiwa rais wa Tanzania na huwezi kulibadilisha hilo kwa chuki zako binafsi, wewe hakuna anae kujua hata wiliya moja tu. Siku yako ikifika hakuna atakae jua labda ndani ya family yako.
 
Mkuu acha kulaumu mtapewa tu,serikali ya awamu ya SITA ni sikivu,ikiahidi imeahidi na lazima itekeleze,madaraja ,nyongeza ya mishahara nk,yote imetekeleza.

Hapa ninapoandika naandika kwa kutumia kishikwambi tulichoahidiwa na mheshimiwa kasimu Majaliwa,mimi tayari nimeshapewa Cha kwangu

Pongezi kwa serikali yangu ya awamu ya SITA kwa kututendea vyema walimu.[emoji123][emoji123][emoji123]
 
Mapema mwezi Disemba mwaka uliopita 2022,waziri mkuu alizindua ugawaji wa Vishkwambi Dodoma kwa walimu wote nchini ili vikatumike kufundishia mashuleni.

Ugawaji wa vifaa hivi ulishaanza na bado unaendelea katika Halmashauri zetu kupitia idara ya Uthibiti ubora(zamani ukaguzi). Cha ajabu badala ya kugawa kwa walimu wote Kama Waziri mkuu alivyoelekeza umetoka mwongozo unaelekeza walimu wa vitengo pekee kupewa vifaa hivyo.

Nimefuatilia kwa ukaribu Halmashauri mbili Mbozi na Mpanda wanagawa Vishkwambi 7 kwa kila shule. Ukiangalia wastani idadi ya walimu kwa shule kwa mfano ni zaidi ya walimu 12, Kwa hesabu hiyo maana yake walimu wengi hawatapata vifaa hivyo. Sasa najiuliza Vishkwambi hivyo VIMEYEYUKIA WAPI?

Nilikuwa najaribu kuiweka video ya kauri ya waziri mkuu Kama rejea, akizindua zoezi lenyewe lakini imegoma. Ila ujumbe wangu umefika.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mapema mwezi Disemba mwaka uliopita 2022,waziri mkuu alizindua ugawaji wa Vishkwambi Dodoma kwa walimu wote nchini ili vikatumike kufundishia mashuleni...
Mtatumia vilivyopo kama ni kwa ajili ya kufundishia na vinatumika kufundishia somo gani
 
Sasa vile vishkwambi vitawasaidia nini walimu. Ule ulikua mchongo wa supplier na hela kashapiga, vina Quality mbovu sijapata kuona utadhani vilitengenezwa 2000's.

Kama wanawapenda walimu wawape latest products za vishkwambi ila sio zile takataka za Sensa.
 
Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya ugawaji wa vishikwambi kwa wafanyakazi. Mitandaoni kumekuwa na maoni tofauti juu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu.

Mimi nimekuja na maswalli ya kujiuliza:
1) Je agizo la Waziri Mkuu halikueleweka au limepuuzwa.

2) Utaratibu wa kuvigawa kwa watumishi wachache ni maagizo ya nani.

3) Hivi agizo la Waziri Mkuu linaufafanuzi?

4) Je madhumuni ya vishikwambi hivi ni nini na je yatatimia kwa walengwa wote?

5) Je Waziri Mkuu alitangaza ugawaji wa vishikwambi hivi bila kujiridhisha kuwa havitoshi? Au ni ukiritimba wa viongozi wa chini?

6) Je agizo la Waziri Mkuu lilikuwa linatofautisha maeneo? Mfano walalamikaji wanadai baadhi ya maeneo/ halmashauri Kila mlengwa kapata lakini baadhi ya maeneo/halmashauri wamepata walengwa wachache.

NB; Waziri Mkuu vi vizuri kutolea ufafanuzi juu ya suala hili, maana huu unaweza kuwa mradi wa watu.
Wafanyakazi chapeni kazi Taifa linawategemea ktk ukuwaji wa uchumi.
 
Waziri mkuu kama si kuhujumiwa na na watendaji wako huku chini basi uliwalaghai watumishi wako. Ama Kama kuna lolote jipya toa kauli , tuna kosa imani wananchi wako kwa mkanganyiko huu.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya ugawaji wa vishikwambi kwa wafanyakazi. Mitandaoni kumekuwa na maoni tofauti juu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu...
Kwani walamba asali waliwahi kushiba nini?
 
nikwamba!!,kwa mujibu wa jamaa yangu ambaye ni mwalimu, kila shule havizidi 8,anapata mkuu wa shule/mwl mkuu,makamu mkuu wa shule,mtaaluma,mtu wa stoo,anaehusika na usajili wa wanafunzi.SIO KILA MWL AMEPATA icho kishikwambi.huo ndio ukweli.
 
nikwamba!!,kwa mujibu wa jamaa yangu ambaye ni mwalimu, kila shule havizidi 8,anapata mkuu wa shule/mwl mkuu,makamu mkuu wa shule,mtaaluma,mtu wa stoo,anaehusika na usajili wa wanafunzi.SIO KILA MWL AMEPATA icho kishikwambi.huo ndio ukweli.
Sio kweli vinakuja kulingana na idadi ya walimu waliopo mashuleni manispaa ya ilala Kila mwl kapata
Na Kuna no IPO ukikosa unapiga kuwaambia

Mimi sipo ila Cha kwangu kipo
 
Mapema mwezi Disemba mwaka uliopita 2022,waziri mkuu alizindua ugawaji wa Vishkwambi Dodoma kwa walimu wote nchini ili vikatumike kufundishia mashuleni...
Wanatumia vishikwambi kufundushia , kwa kutumia ubao wa chaki😂.
Tumieni akili,
hivyo vishikwambi vina itaji msaada wa vifaa vingine vya tehama kama projectors, podiums ili lengo la kufundishia wanafunzi litimie
 
Back
Top Bottom