Hakika mama anahujumiwa. Walimu walitangaziwa kuwa kila mmoja atapewa vishikwambi vilivyotumika kwenye zoezi la sensa mwaka jana na kwamba vingine vilinunuliwa ili kuendana na idadi ya walimu.
Ajabu sasa waliopewa vishikwambi ni mwl mkuu au mkuu wa shule, mtaaluma, mhasibu na malezi tu.
Je, vingine vimeenda wapi?
Bora kukaa kimya ukatenda kuliko kuwatumainisha walimu halafu usitekeleze. Unawapa hasira uliowaahidi.
Najiuliza hivi hizi ni hujuma anazofanyiwa rais wetu?
1. Vishikwambi hewa
2. Nyongeza ya mishahara 23.3% hewa.
Duuuu! Hujumaaaaa