Vision ya Rais Dkt. Magufuli ni kuipeleka Tanzania mbele kupitia njia waliyopita Singapore

Vision ya Rais Dkt. Magufuli ni kuipeleka Tanzania mbele kupitia njia waliyopita Singapore

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,086
Huwa ni kwa vile watu ni wagumu sana kuelewa. Vision ya Rais Dkt. Magufuli ni kuipeleka Tanzania mbele kupitia njia waliyopita Singapore. Singapore walikuwa masikini mara 3 ya Tanzania ya leo. Miaka ya mwanzo ya 70 walikuwa na GDP per capita $320. Sisi leo GDP per capita ni $930. Leo Singapore wana zaidi ya $60,000.

Kama Rais Dkt. Magufuli anavyofanya, walianza na elimu ya bure na kuwekeza sana kwenye vyuo vya ufundi. Wakahakikisha wanapata wataalan wa kutosha. Waliekeza sana kwenye miundombinu ya umeme, mabarabara, bandari, viwanja vya ndege, technologia ya mawasiliano etc, walichochea sekta kama za utalii na huduma nyingine. Waliekeza sana kwenye afya hadi kuvutia medical tourism. Walipambana na rushwa na kutoa adhabu kali sana hasa death penalty kwa wahujumu uchumi.

Wali sacrifice bla bla za kisiasa na ku focus kwenye maendeleo. Mwandishi mmoja anasema:-

"Singapore's model of sacrificing freedom for business is highly controversial and heavily debated. Regardless of philosophy, though, its effectiveness is undeniable."

Lakini kikubwa ambacho Rais Dkt. Magufuli amekipania sana kipindi hiki ni kujenga mazingira mazuri ya kuvutia mitaji ya ndani na nje. Inabidi kupitia upya tena kwa kuchukua mfano wa Singapore sera za kodi, sheria na sera za kazi, sera za ardhi, sera za fedha, sheria za utatuzi wa migogoro, sera za biashara kwa ujumla nk.

Tukifanikiwa hapo Tanzania ni 'a new Singapore in the making.'

Tumuunge mkono JPM na wale ambao wamepewa majukumu ya kumshauri na kumsaidia wajaribu kujielimisha sana na kuweka pembeni maslahi binafsi.
 
Tatizo ulivo mpumbavu,wewe ndio unaetaka tuende katika uelekeo huo. Alafu unataka kutuaminisha JPM ndo ana vision hiyo, kwa kuuwa biashara kwa hizi kodi zao unazotakiwa kulipa kutoka kwenye mtaji na sio faida?
 
Huwa ni kwa vile watu ni wagumu sana kuelewa. Vision ya Dkt. JPM ni kuipeleka Tanzania mbele kupitia njia waliyopita Singapore. Singapore walikuwa masikini mara 3 ya Tanzania ya leo. Miaka ya mwanzo ya 70 walikuwa na GDP per capita $320. Sisi leo GDP per capita ni $930. Leo Singapore wana zaidi ya $60,000...

Umeandika juu ya SINGAPORE MODEL kuwa Jiwe ndio anayoifuata kama suluhisho la maendeleo ya Tanzania!!! The three pillars za hiyo model ni; MERITOCRACY, PATROTISM na INTERGRITY.

Kufanikiwa kwake kunategemea kama atakuwa muumini wa kweli wa hayo mambo matatu. Akiendelea na kuteua watu wa kanda ya ziwa katika nafasi serikalini na kwenye mashirika hata kama hawakidhi hivyo vigezo, atakuwa anatwanga maji kwenye kinu!
 
Huwa ni kwa vile watu ni wagumu sana kuelewa. Vision ya Dkt. JPM ni kuipeleka Tanzania mbele kupitia njia waliyopita Singapore. Singapore walikuwa masikini mara 3 ya Tanzania ya leo. Miaka ya mwanzo ya 70 walikuwa na GDP per capita $320. Sisi leo GDP per capita ni $930. Leo Singapore wana zaidi ya $60,000...
Hiyo nchi unayosema ,kwanza mahakama zilikuwa huru hivyo kumfunga yeyote awe Rais au kinyago yeyote, Bunge lilikuwa huru kuisimamia serikali, Vyama vya wafanyakazi vilikuwa huru kufanya mipango yao, Demokrasia ilikuwa inawaka kweli kweli lakini Tanzania ni kinyume chake yaani mtu mmoja ndio anaamua kila kitu.

Jana kituo kimoja cha habari kinaripoti kuwa kuna wahamiaji Haram kutoka Ethiopia wameingia nchini huko kwao kuna maisha magumu sasa nikajiuliza mbona hawa wanandege za kusafiri kama elfu kumi hivi na maisha yao ni dhaifu sana ili hali huku kwetu tunaambiwa ukiwa na ndege maisha yanakuwa mazuri sana?

Bado sikupata Majibu !Jana pia bwana Jafo anasema kuna wanafunzi wamefaulu lakini hawataweza shuleni kwa wakati hivi waziri ameshindwa kujua kwa miaka miwili iliyopita kwamba idadi ya wanafunzi itakuwa kubwa au ndogo?Halafu mtoa mada unasema unafanya kama Singapore!!Hivi ni vichekesho yaani maajabu yanaendelea.
 
Kweli Nchi yetu anaipeleka mbele,hasa ukiwa kula kulala au unaishia kwa shemeji,huwezi kujua Kama tuaenda mbele au tunaludi kinyume nyume.

Mazao yaliyokufa tangu aingie Madarakanu ni :-
Tumbaku
Kahawa
Korosho
Pamba
Mkonge
Mbaazi
Ufuta
Dengu
Choroko nk.
Bado makampuni na Benki zilizo kufa.

Cc,
Japo baadhi ya Mazao yalikuwa yameanza kodorola awamu zilizopita,awamu hii ndiyo imeyamalizia kuyaua,
 
Baada ya haya masakata ya TRA nimefuatilia kodi mbali mbali na mazingira ya uwekezaji aisee sijaamini jinsi wawekezaji walivyowekewa mazingira rahisi, contrary to popular beliefs.

Kwakweli watanzania tumelala sana, sasa ndio naelewa kwanini wageni wanaokuja wana tajirika haraka.

Siasa zetu ni tatizo majungu na upotoshaji umekithiri sana, wataalamu wanaopewa nafasi za ku promote uwezekaji ovyo, bungeni tumejaza vimeo wanaopigia makofi kila kitu au wanaopinga kila kitu bila ya kujadili hoja on merit wakati wizara ya fedha ina kodi rafiki mno za uwekezaji wa kibiashara.

Yaani unabaki unashangaa kwanini mwafrika akipata hela anakimbilia kununua viwanja aje kulangua baadae, ajenge hotel au nyumba za kupangisha.

Wakati Shabib na ndugu zake wanaachana na mabasi wanakwenda kulima Rukwa kumbe capital allowance incentives zilizopo kwenye kilimo aisee yaani wewe ukileta mamashine yako ya kisasa yenye thamani za billioni kadhaa (ukishayatoa bandarini ukalipa kodi) icho kiwango cha kodi utakachopunguza kwenye profit tax kwa miaka kadhaa kama ni mkulima mkubwa mungu anajua.

Tatizo sio serikali peke yake na sisi wananchi kumbe; wengi wetu atijui fursa za uwekezaji zilipo.
 
Kweli Nchi yetu anaipeleka mbele,hasa ukiwa kula kulala au unaishia kwa shemeji,huwezi kujua Kama tuaenda mbele au tunaludi kinyume nyume.

Mazao yaliyokufa tangu aingie Madarakanu ni :-
Tumbaku
Kahawa
Korosho
Pamba
Mkonge
Mbaazi
Ufuta
Dengu
Choroko nk.
Bado makampuni na Benki zilizo kufa.

Cc,
Japo baadhi ya Mazao yalikuwa yameanza kodorola awamu zilizopita,awamu hii ndiyo imeyamalizia kuyaua,
Unajua unafuu uliopo kwa sasa ukiweza kuingiza machine za kufanya secondary processes?

Serikali aiwezi fanya kila kitu mmezoea exports matokeo yake bei za soko la dunia zikishuka mnaanza kulia. Badala ya kufikiria kuongeza thamani ya bidhaa mkauze nchi za jirani mnataka serikali ikawatafutie masoko ya primary productions.
 
Huwa ni kwa vile watu ni wagumu sana kuelewa. Vision ya Dkt. JPM ni kuipeleka Tanzania mbele kupitia njia waliyopita Singapore. Singapore walikuwa masikini mara 3 ya Tanzania ya leo. Miaka ya mwanzo ya 70 walikuwa na GDP per capita $320. Sisi leo GDP per capita ni $930. Leo Singapore wana zaidi ya $60,000.

Kama JPM anavyofanya, walianza na elimu ya bure na kuwekeza sana kwenye vyuo vya ufundi. Wakahakikisha wanapata wataalan wa kutosha. Waliekeza sana kwenye miundombinu ya umeme, mabarabara, bandari, viwanja vya ndege, technologia ya mawasiliano etc, walichochea sekta kama za utalii na huduma nyingine. Waliekeza sana kwenye afya hadi kuvutia medical tourism. Walipambana na rushwa na kutoa adhabu kali sana hasa death penalty kwa wahujumu uchumi.

Wali sacrifice bla bla za kisiasa na ku focus kwenye maendeleo. Mwandishi mmoja anasema:-

"Singapore's model of sacrificing freedom for business is highly controversial and heavily debated. Regardless of philosophy, though, its effectiveness is undeniable."

Lakini kikubwa ambacho JPM amekipania sana kipindi hiki ni kujenga mazingira mazuri ya kuvutia mitaji ya ndani na nje. Inabidi kupitia upya tena kwa kuchukua mfano wa Singapore sera za kodi, sheria na sera za kazi, sera za ardhi, sera za fedha, sheria za utatuzi wa migogoro, sera za biashara kwa ujumla nk.

Tukifanikiwa hapo Tanzania ni 'a new Singapore in the making.'

Tumuunge mkono JPM na wale ambao wamepewa majukumu ya kumshauri na kumsaidia wajaribu kujielimisha sana na kuweka pembeni maslahi binafsi.
Acheni kupost ujinga wenu humu, endeleni kumwabudu kimyakimya. Kwani ulisikia huko Singapore kuna wasiojulikana wanaoteka, kutesa na hata kuua watu wasio na hatia? Wefikia hapo kwa kufuata utawala bora na demokrasia ya kweli
 
Muwe na akili hata kidogo basi na muwe mnasoma hata vitabu..na hao viongozi kama mko nao karibu advice them wasome vitabu...there's no way we'll make it and become the next Singapore kwa akili za sasa, za wakina dangote kufunga viwanda? Watu kufilisika? Money circulation kupungua kiasi hiki? Watu kupunguziwa mishahara kwenye tv?

Anyways kasomeni, am glad nimesoma vitabu vingi jinsi Singapore and other tiger countries walifanyaje kuwa hapo...sitaki kusema sana, ila nakuachia home work, ukiweza nitakuja kukujibu kwa undani kwann what we are doing is not even close to what Singapore did to advance economically and scientifically: Rais wako anasema tuzaliane sana tukuze uchumi: Swali kuna economic theories zipi zinasema kuna correlation ya ongezeko la watu na ukuaji wa uchumi? 😂😂😂

Ukiweza nijibu, ukishindwa nataka kukuachia huu ujumbe: Countries are transformed by extremely intelligent people and i don't see any form of intelligence in our leaders...all i see is leaders with no vision and probably don't know what they are doing, na wanavyokopa hivyo na deni la taifa lilipofikia sitashangaa wakisema nchi imefilisika.
 
Kweli Nchi yetu anaipeleka mbele,hasa ukiwa kula kulala au unaishia kwa shemeji,huwezi kujua Kama tuaenda mbele au tunaludi kinyume nyume.

Mazao yaliyokufa tangu aingie Madarakanu ni :-
Tumbaku
Kahawa
Korosho
Pamba
Mkonge
Mbaazi
Ufuta
Dengu
Choroko nk.
Bado makampuni na Benki zilizo kufa.

Cc,
Japo baadhi ya Mazao yalikuwa yameanza kodorola awamu zilizopita,awamu hii ndiyo imeyamalizia kuyaua,
No creature under the sun can be perfect by 100% zipo dosari nadhani zitasahihishwa huku tuendako na shida ni kuwa baadhi ya watendaji walimuangusha wakati rais akitupia jicho zaidi kwenye miradi hii mikubwa hakika alikuwa hapepesi macho pembeni thatswhy nadhani muda ndio huu sasa we can take a modal structure from any developed country in tax colectings and any that could makes tz shines
 
Jana na leo ni tofauti,majira na nyakati vinakinzana, hatuendi kokote bila mshikamano wa kitaifa, wenda ata Mgabe alitamani ivyo but aliishia kulivuruga taifa, simuone aliekua aliekua akiuza karanga kajenga gorofa na wewe ukadhani utajenga kwa kupitia njia hiyo ,Cha msingi pitia njia nyingine ili Hali ujenge gorofa utimize nia yako,
Bila kuleta taifa pamoja, hatuwezi fika popote, ukweli ndo huo
 
Kama umesoma LOGIC hebu fikiria hili:
Kwa asilimia kubwa(around 80%) uchumi wetu unategemea kilimo.Maana yake ili uchumi ukue lazima sekta hii ya kilimo itoe matunda.Sasa unatuambiaje sisi ni sawa na Singapore!!!!!!?
 
Ingekuwa JPM anafuata njia ya Singapore angeanza na kuhakikisha Bandari ya Bagamoyo inajengwa na hatimae Tanzania kuwa the Gateway of East & Central Africa!!!

Singapore ni transshipment port, na ndicho ambach kilikusudiwa pale Bagamoyo, na ndio maana ukiangalia Bagamoyo Port MasterPlan unakuta hadi itakavyokuwa interconnected na land locked countries!!

Ile project ya reli ambayo ilikuwa iwe funded na China, akaipiga chini kwa madai kulikuwa na ufisadi lakini leo ukipitia financing aliyotumia yeye, kisha ukalinganisha na gharama ambazo Wachina walitoa, yeye atajenga kwa gharama kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa plan ya awali!

Kituko zaidi ni pale tunaposikia eti tumerudi tena kwa Wachina wa-finance ujenzi wa reli!! Jukwaa hili hili watu tulisema Mturuki HANA excess fund kama aliyonayo Mchina, na kwahiyo watachelewesha tu mradi kama sio kukwama mbele ya safari!!

Pili, angehakikisha Gas Extraction inafanyika... I repeat kama nilivyoongea mara kadhaa! Anatumia nguvu kubwa sana kwenye madini wakati utajiri wa nchi hii upo kwenye gas! Mining Industry cash is just a petty cash compared to Gas Industry Cash!!

Tatu, angevutia sana uwekezaji kwenye Service and Banking Sectors... those are pillars of modern economies!!

Hayo uliyosema yote, technically Magu kayakuta watu wameshajenga foundation!! Hivyo vyuo vya elimu ya ufundi sijui ni vyuo gani wakati VETA kaikuta!!

Hiyo Elimu Bure unayoisema wewe sijui ni ipi na ina impact gani wakati nchi bado ina uhaba mkubwa wa Walimu wa Sayansi na Maths, na hata baada ay kuipiga chini Special Diploma (Science & Maths) pale UDOM, miaka 5 imepita na hajaja na plan mpya!!

Lakini pamoja na yote bado unaota kulinganisha jinsi Singapore walivyojenga uchumi wao and how Magufuli anavyofanya?!

Acha utani!
 
Hiyo nchi unayosema ,kwanza mahakama zilikuwa huru hivyo kumfunga yeyote awe Rais au kinyago yeyote, Bunge lilikuwa huru kuisimamia serikali, Vyama vya wafanyakazi vilikuwa huru kufanya mipango yao, Demokrasia ilikuwa inawaka kweli kweli lakini Tanzania ni kinyume chake yaani mtu mmoja ndio anaamua kila kitu.

Jana kituo kimoja cha habari kinaripoti kuwa kuna wahamiaji Haram kutoka Ethiopia wameingia nchini huko kwao kuna maisha magumu sasa nikajiuliza mbona hawa wanandege za kusafiri kama elfu kumi hivi na maisha yao ni dhaifu sana ili hali huku kwetu tunaambiwa ukiwa na ndege maisha yanakuwa mazuri sana?

Bado sikupata Majibu !Jana pia bwana Jafo anasema kuna wanafunzi wamefaulu lakini hawataweza shuleni kwa wakati hivi waziri ameshindwa kujua kwa miaka miwili iliyopita kwamba idadi ya wanafunzi itakuwa kubwa au ndogo?Halafu mtoa mada unasema unafanya kama Singapore!!Hivi ni vichekesho yaani maajabu yanaendelea.
Ivi ndege kumi kwa nchi kubwa Kama Tanzania nazo ni mjadala, bei yake ni sawa kilometa ngapi za barabara ya lami ya Highway? Idadi ndogo ya ndege hizo kwa Tanzania ni sahihi kwa sababu hiyo ni miundombinu na inasaidia kutambulisha fursa nchi. Bora ubabe tu.
 
Ingekuwa JPM anafuata njia ya Singapore angeanza na kuhakikisha Bandari ya Bagamoyo inajengwa na hatimae Tanzania kuwa the Gateway of East & Central Africa!!!

Singapore ni transshipment port, na ndicho ambach kilikusudiwa pale Bagamoyo, na ndio maana ukiangalia Bagamoyo Port MasterPlan unakuta hadi itakavyokuwa interconnected na land locked countries!!

Ile project ya reli ambayo ilikuwa iwe funded na China, akaipiga chini kwa madai kulikuwa na ufisadi lakini leo ukipitia financing aliyotumia yeye, kisha ukalinganisha na gharama ambazo Wachina walitoa, yeye atajenga kwa gharama kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa plan ya awali!

Kituko zaidi ni pale tunaposikia eti tumerudi tena kwa Wachina wa-finance ujenzi wa reli!! Jukwaa hili hili watu tulisema Mturuki HANA excess fund kama aliyonayo Mchina, na kwahiyo watachelewesha tu mradi kama sio kukwama mbele ya safari!!

Pili, angehakikisha Gas Extraction inafanyika... I repeat kama nilivyoongea mara kadhaa! Anatumia nguvu kubwa sana kwenye madini wakati utajiri wa nchi hii upo kwenye gas! Mining Industry cash is just a petty cash compared to Gas Industry Cash!!

Tatu, angevutia sana uwekezaji kwenye Service and Banking Sectors... those are pillars of modern economies!!

Hayo uliyosema yote, technically Magu kayakuta watu wameshajenga foundation!! Hivyo vyuo vya elimu ya ufundi sijui ni vyuo gani wakati VETA kaikuta!!

Hiyo Elimu Bure unayoisema wewe sijui ni ipi na ina impact gani wakati nchi bado ina uhaba mkubwa wa Walimu wa Sayansi na Maths, na hata baada ay kuipiga chini Special Diploma (Science & Maths) pale UDOM, miaka 5 imepita na hajaja na plan mpya!!

Lakini pamoja na yote bado unaota kulinganisha jinsi Singapore walivyojenga uchumi wao and how Magufuli anavyofanya?!

Acha utani!
Nchi hii bado ina wajinga wengi na ndio wanaotutawala don't expect anything ndugu kama Taifa tumekwama!

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom