Visomo (Dua) Sita Zizofanywa na TANU Mwalimu Nyerere Akishiriki Wakati wa Kupigania Uhuru 1954 - 1961

Visomo (Dua) Sita Zizofanywa na TANU Mwalimu Nyerere Akishiriki Wakati wa Kupigania Uhuru 1954 - 1961

"Nimevutiwa na hiki kipengele nimejikuta napata swali pia.

Lakini pia katika hutuba yake ya kuagana na wazee wa Dar 1985, alieleza kwa ufasaha jinsi wenyeji wa Dar (moslems in particular) walivyochangia katika harakati za uhuru.

Alikwenda mbali akaeleza mpaka baadhi ya MATAMBIKO waliyofanya wazee wa KIISLAMU akiwa peke yake wa imani tofauti.

Ninaomba kupata ufafanuzi je kuna uhusiano wa MATAMBIKO na Uislamu?

VISOMO SITA ALIVYOFANYIWA JULIUS NYERERE NA WANACHAMA WENGINE WA TANU WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961

Mtegite,
Bahati mbaya sana Mwalimu Nyerere kuna mambo yawezekana hakuwa anayajua au labda hakupenda kuyazungumza.

Kwanza ni kuwa kile kilichofanywa kwa Jumbe Tambaza si tambiko ni dua.

Mahali wanapokutana masheikh inafanyika dua na dua ziko katika Qur'an.

Hawakutani masheikh kutambika.

Dua inaweza kufuatia na kuchinja mnyama.

Mwalimu Nyerere hakuwa wa kwanza katika kufanyiwa dua ndani ya TANU.

Mwanachama wa kwanza wa TANU kufanyiwa dua alikuwa Abdul Sykes ambae mwaka wa 1954 alikutwa na kadi za TANU ndani ya ofisi yake akiwa Market Master, Soko la Kariakoo.

Kisa kirefu lakini ilihofiwa atafukuzwa kazi.

Ikafanywa dua na akachinjwa kondoo.

Mwanachama wa pili alikuwa Rashid Ali Meli.

Huyu alikuwa Bwana Fedha wa Dar es Salaam Municipal Council.

Rashid Ali Meli alitoa fedha za Municipal akampa Iddi Faiz Mafungo atie kwenye mfuko wa safari ya Nyerere UNO awahi kusafiri lakini zirudishwe haraka.

Baada ya kutoa fedha zile siku ya pili Wakaguzi wakafika ofisini kwake kumkagua.

TANU ikamfanyia dua kuomba msaada wa Allah Rashid Ali Meli anusurike.

Dua ya tatu ilifanyika ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu nyumbani kwa Ali Msham kuomba safari ya salama kwa Mwalimu Nyerere aliyekuwa anakwenda UNO safari ya kwanza 1955.

Mwalimu alifanyiwa dua ya nne Lindi mwaka wa 1956 na Sheikh Mohamed Yusuf Badi nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji.

Dua ya tano Mwalimu alifanyiwa Mnyanjani kutafuta uelewano baina ya wana TANU katika msuguano wa Kura Tatu mwaka 1958.

Hivi ndivyo visomo vitano na ukiongeza na kile alichoeleza Mwalimu Nyerere jumla vinakuwa visomo sita.

Hapakuwa na matambiko.

View attachment 2470365
Dua ofisi ya TANU Mtaa wa Jaribu Magomeni nyumbani kwa Ali Msham kuomba salama ya safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955.
Mzee wangu Saidi nilitaka kukuuliza hivi!!!Kwani Watanganyika maeneo mengine hawakufanya matambiko kumuombea Nyerere asafiri salama mwaka 1955 kwenda UNO au Tanganyika ilikua kariakoo na Magomeni na maeneo ya pwani tu????Ebu tafuta historia za wadau wa Tanu miaka hiyo kama Siliwale wa Sanya na wale wazee wa Nyanza akina Mohamedi Sufiani,na wale wazee wa Western Province akina Mganga Nyambuke na yule aliyekua anajiita Mungu mtu pale ujiji wote walikua wanachama ndaki ndaki wa Tanu
Tai...
Yawezekana hayo kwa wengine lakini katika Uislam hakuna kutambika.

!!Ebu tafutafuta na hao utuletee historia zao pia!!!!Unatuelimisha mzee wangu ila kuna maeneo mengi ya Tanganyika unayaacha katika historia zako hasa yale ya bara na mchango wa wale wazee wa kibantu kusaidia uhuru!!!
 
Tai...
Yawezekana hayo kwa wengine lakini katika Uislam hakuna kutambika.
Kutambika ni neno la kibantu asili yake limetokana na neno tambika hasa kwa makabila ya eneo Congo basin na uwanda wa rift valley!!!Maana yake kwa kiswahili fasaha ni kutoa zaka au sadaka kwa kuchinja mnyama na kuweka vinywaji!!Uislamu kwa kua umeshahabiana kiarabu katika lugha zake za awali kabisa neno kutambika halipo lipo neno zaka au zakhar inategemea unaongea kiarabu cha maghreb au mashariki ya kati na kiswahili cha kimvita kinachotumika pwani ya afrika mashariki neno kutambika linatafusiriwa tofauti!!Kutambika maana yake maombi ya kuchinja mnyama na zaka!!!Sasa katika uislamu maombi ya kuchinja mnyama na zaka au zakhar yapo mzee wangu!!!Tumefanya sana pale magomeni kwa mzee wetu marehemu Sheik Yahaya katika shughuli mbalimbali!!!Kutambika ni neno tu la kibantu na kwa kiarabu ni zaka au zakhar na zaka katika uislamu zipo!!!!Ni lugha tu Mzee wangu usifikiri neno KUTAMBIKA ni la ajabu sana!!!!
 
Mzee wangu Saidi nilitaka kukuuliza hivi!!!Kwani Watanganyika maeneo mengine hawakufanya matambiko kumuombea Nyerere asafiri salama mwaka 1955 kwenda UNO au Tanganyika ilikua kariakoo na Magomeni na maeneo ya pwani tu????Ebu tafuta historia za wadau wa Tanu miaka hiyo kama Siliwale wa Sanya na wale wazee wa Nyanza akina Mohamedi Sufiani,na wale wazee wa Western Province akina Mganga Nyambuke na yule aliyekua anajiita Mungu mtu pale ujiji wote walikua wanachama ndaki ndaki wa Tanu


!!Ebu tafutafuta na hao utuletee historia zao pia!!!!Unatuelimisha mzee wangu ila kuna maeneo mengi ya Tanganyika unayaacha katika historia zako hasa yale ya bara na mchango wa wale wazee wa kibantu kusaidia uhuru!!!
Nelson...
Kuhusu kufanyika kwa dua ukweli ni kuwa kwa utafiti wangu nafahamu dua 5 na nimeandika historia zake hapa.

Hizi dua zilianza Dar es Salaam kwa kuwa hapa ndipo TANU ilipokuwa na nguvu Tanganyika yote.

Sehemu nyingine TANU iliingia kadri harakati zilivyozidi kupamba moto.
Kuhusu sehemu na wazalendo wengine ulionitajia hakika hawapo katika kitabu changu kwani singeweza kuandika historia ya kila jimbo, mji na wilaya.

Kuna sehemu hapakuwa na kitu yaani TANU haikuingia kwa haraka ilichelewa sana na sehemu hizo zinafahamika na sababu ya TANU kukawia kuingia zinafahamika.

Siwezi kurudia kuandika historia ya TANU mara mbili kwa kuwa historia ya TANU nimeiandika kwa kadri ya uwezo wangu nikiongozwa na harakati zilizokuwako.

Huwezi kufananisha historia ya TANU Kanda ya Ziwa na historia ya TANU Peramiho na Nachingwea.

Kanda ya Ziwa kulikuwa na Ali Migeyo.

Kiongozi wa TAA shupavu kiasi alipigwa mabomu katika mkutano akihamasisha wananchi kuwa wamoja kudai nchi yao.

Huwezi kwa kuwa TANU haikuweko Peramiho na sehemu nyingi za Southern Province ambako Kanisa lilikuwa na nguvu.

TANU ilikuwa Moshi mjini lakini haikuwapo Mgombani juu Kilimanjaro kwa sababu kwanza Kanisa lilikuwa na nguvu na pili Mangi hawakuiunga mkono.
 
Ni kawaida kwa wabasiasa kufanyiwa dua na yeyote yule.

Wataingia misikitini, makanisani, kwa waganga wa Jadi, machief wa Jadi.

Mwanasiasa kujiweka popote kawaida tu.

Leo utamkuta kavaa baraghashia msikitini, kesho utamkuta kansani, kesho kutwa kwa waganga nk.

Wala hii siyo stori.
 
Nelson...
Kuhusu kufanyika kwa dua ukweli ni kuwa kwa utafiti wangu nafahamu dua 5 na nimeandika historia zake hapa.

Hizi dua zilianza Dar es Salaam kwa kuwa hapa ndipo TANU ilipokuwa na nguvu Tanganyika yote.

Sehemu nyingine TANU iliingia kadri harakati zilivyozidi kupamba moto.
Kuhusu sehemu na wazalendo wengine ulionitajia hakika hawapo katika kitabu changu kwani singeweza kuandika historia ya kila jimbo, mji na wilaya.

Kuna sehemu hapakuwa na kitu yaani TANU haikuingia kwa haraka ilichelewa sana na sehemu hizo zinafahamika na sababu ya TANU kukawia kuingia zinafahamika.

Siwezi kurudia kuandika historia ya TANU mara mbili kwa kuwa historia ya TANU nimeiandika kwa kadri ya uwezo wangu nikiongozwa na harakati zilizokuwako.

Huwezi kufananisha historia ya TANU Kanda ya Ziwa na historia ya TANU Peramiho na Nachingwea.

Kanda ya Ziwa kulikuwa na Ali Migeyo.

Kiongozi wa TAA shupavu kiasi alipigwa mabomu katika mkutano akihamasisha wananchi kuwa wamoja kudai nchi yao.

Huwezi kwa kuwa TANU haikuweko Peramiho na sehemu nyingi za Southern Province ambako Kanisa lilikuwa na nguvu.

TANU ilikuwa Moshi mjini lakini haikuwapo Mgombani juu Kilimanjaro kwa sababu kwanza Kanisa lilikuwa na nguvu na pili Mangi hawakuiunga mkono.
Hapo nimekuelewa mzee wangu kumbe unaielezea Tanu ya sehemu chache chache kutokana ufahamu wako na historia uliyopata au kushuudia!!!Nimekuelewa mzee wangu
 
Ni kawaida kwa wabasiasa kufanyiwa dua na yeyote yule.

Wataingia misikitini, makanisani, kwa waganga wa Jadi, machief wa Jadi.

Mwanasiasa kujiweka popote kawaida tu.

Leo utamkuta kavaa baraghashia msikitini, kesho utamkuta kansani, kesho kutwa kwa waganga nk.

Wala hii siyo stori.
Mose...
Sijakutana na historia hiyo kuwa kulikuwa na maombi ya uhuru kanisani.

Wala sijukutana na historia ya waganga wa kienyeji nk katika utafiti wangu wa harakati za uhuru.

Ila kuna kisa cha mganga mmoja kutoka sehemu za kusini ya Tanganyika jina lake Nguvumali.

Kisa kinasema kuwa Nguvumali alikuwa anasafiri ndani ya basi anakuja Dar es Salaam kwa nia ya kumfanyia ubaya Julius Nyerere.

Basi likapinduka njiani kabla ya yeye kufika Dar es Salaam akafa.
Kuna historia ya Sheikh Issa Nasir mjumbe wa Baraza la Wazee wa TANU kutoka Bagamoyo.

Sheikh Issa Nasir alikuwa bingwa wa elimu na majini.

Huenda wale ambao hawakukulia katika mazingira ninliyokulia mimi hili jambo la majini likampa shida kuelewa khasa ni elimu gani.

Mimi kwa kuogopa mapambano sitaingia ndani zaidi kueleza.

Sheikh Issa Nasir ukiangalia picha kila alipokuwako Nyerere utamuona yeye kakaa karibu yake.

Mpashai wangu anasema kuwa hapo alipo na Mwalimu Sheikh Issa Nasir hayukoi peke yake yuko na ''askari'' wake ambao wewe huwezi kuwaona kwa macho yako haya ya kuvukia barabara.

Mwalimu akimpanda sana Sheikh Issa Nasir au tunaweza kusema wakipendana sana na alikuwa anaweza kuingia Ikulu muda wowote autakao.

Angalia picha hiyo hapo chini ya Baraza la Wazee wa TANU Mwalimu aliposimama chini yake kuwa watu wawili wamechutama huyo wa kulia mwenye fimbo begani ndiye Sheikh Issa Nasir.

Picha ya chini kulia ni Sheikh Issa Nasir akiwa Karimjee Hall siku ilipotolewa tarehe ya uhuru.

Hapo yuko karibu na Mwalimu Nyerere na jeshi lake kutoa ulinzi.
Askari wake hawaonekani.

Nimefaidi sana katika utafiti wa historia ya TANU na kuna mengi sikuyaeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

1673115022819.jpeg

The_National_Archives_UK_-_CO_1069-166-21.jpg

 
Hapo nimekuelewa mzee wangu kumbe unaielezea Tanu ya sehemu chache chache kutokana ufahamu wako na historia uliyopata au kushuudia!!!Nimekuelewa mzee wangu
Nelson...
Hujanielewa.

Najua kinacho kutaabisha akili yako inakataa kukubali.
Hili si wewe peke yako.

Unatafuta upenyo wa kutokea.
Huwezi kuupata kwani haupo.

Wewe bado hujaamini kuwa mimi naijua historia hii kinyumenyume?

Unataka hii iwe si historia ya TANU.
Lakini hiyo niliyoandika ndiyo historia ya TANU.

Huko ndiko zilikokuweko harakati za TANU na nimetumia Nyaraka za Sykes kwani wao ndiyo waliounda African Association mwaka wa 1929.

Haiwezekani kwa yeyote yule kuja kuandika historia ya TANU nyingine zaidi ya hii.

Huu mwaka wa 25 hakuna aliyekuja na kitabu kupinga kitabu cha Abdul Sykes

Nyerere kaikuta TANU nyumbani kwa akina Sykes hakuja Dar es Salaam na fikra ya kuanzisha chama cha siasa.

Hakuna TANU ya sehemu chache.
Huko kwengine kulikuwa hakuna kitu.

Abdul Sykes anasema yeye kaona kwa macho yake akiwa mtoto wakati ofisi ya AA ikijengwa pale New Street na Kariakoo.
 
Kuna hotuba ya nyerere anadai kule bagamoyo alifanyiwa tambiko akawa anaruka shimo... je kwenye uislamu kitu hicho kipo? Na pili nikuulize hivi inaswihi kumuombea dua asie muislamu?
 
Vipi tambiko la Tambaza ambalo mwalimu mwenyewe alisimulia?
 
Mzee unajichanganya. Tambiko ni sadaka ya kuchinda kwa nguvu ya ziada tunayoiamini iwe ni Mungu, Alla, mizimu, majini nk. Ibada dua, maombi au kisomo kinachoambatana na kuchinja au kuua kiumbe chenye damu ni TAMBIKO. Masheikh walitambika na wala sio kitu kibaya. Hata manabii na mitume wa Mwenyeez Mungu walitambika kama hao unaowaita waganga wa kienyeji.
SAHIHI.

Ndiyo fasaha ya >ELIMU 3.0<.

0_0


Kwa ujumla, Urastafari hupinga mifumo japo mapokeo ya namna hii ama ile kiroho—mambo kama yale ya ‘jamii za kikuhani’ na ‘ibada’ ni yenye asili ya jamii za Kiafrika na pia ‘Mashariki ya kati’ yaani Uyuda—na Uhindu vilevile. Nyumba ya Nyahbinghi kwa mfano, ina asili ya ‘ngoma za maruhani’ za kimakabila ya Afrika, ambavyo vilevile mna desturi ya kuambatana na matumizi ya ‘mimea’ ama ‘pombe’ kwa ‘matambiko’. Urastafari, kupitia muingiliano wake na mapokeo kutokea kwa jamii ya Kihindu kule karibia ndilo limeleta ‘sakramenti’ ya matumizi ya ‘Ganja’ katika jamii inayoshiriki wakati wa miditisha ya kikundi cha watu wanaokaa pamoja. Kwa hivyo mahala pa ‘tambiko’ katika urasta huwa si tena jambo la ‘kupunga maruhani’ bali kutafuta ‘utulivu’ na amani ya JAH Rastafari kupitia sakramenti ya ‘Ganja’ na kushiriki furaha kwa wandugu katika Rastafari.

Kwa jicho la Uono na Ufikirifu Mifumo, jamii ya Kihindu huwa na ‘zikri’ ya kusema JAI JAI pale Mhindu anapoonja na kulifurahia lenye kumpa faraja moyoni. Haya hufahamika kuwa ni matendo ya ‘utakaso’ kupitia nidhamu ya ‘kukumbuka’--kumkumbuka ‘Mungu’ katika kila jema unaloliishi—Yoga Bhakti. Hili ndilo linachangia JAH JAH kuwa sehemu ya urithi wa mapokeo ya Kiyuda na hapo hapo Uhindu. Na ndivyo hivi, mlima Sayuni, kwa wahindu ungalitajwa ni >‘Mlima Meru’<; Zaburi ya Daudi kwa Mhindu ingalikuwa si jingine bali muktadha wa Bhakti Yoga-->JAI OM NAMA SHIVAYA<. Kutokuchana nywele na uvijitari pia vinaasili ya ‘maisha ya upweke’ na kujitenga ya mtu wa kutafuta ‘Utakaso’ isivyo kufuatisha mazoea na mkumbo wa jamii pana-->Sannyasi<.

Kwa mtu-Rasta, ‘Dreadlocks—Misokoto ya asili ya Nywele’ ni alama ya ‘upekee’ wake, kujinasibu na uzuri wa asili, na imani yake kwa muambata wa mambo mengine yote, kuitwa ni ‘I-tal Livity’-- muungano na neno ‘Vital’--’uhai pumzi’ na ‘Livity’--’Uisho’. Iwe ni mazingira ya mjini ama shamba, utambulisho wa mtu-Rasta ni maisha rahisi katika kilimo ama kazi huku akiishi nadhiri yake ya Pendo Moja, Amani na Utangamano kati ,yake na dunia na walimwengu.

Sasa tunawezaje kuyashahibisha na dhana nzima ya Utaifa, tuseme labda taifa la Tanzania?

Kiuono na ufikirifu mifumo, ujenzi wa taifa lolote huhitaji ‘nguzo ya imani’. Hili ndilo linalobayanisha ukomo wa ELIMU 1.0 katika jitihada na harakati la ‘kujenga Taifa’. Maarifa ya mambo yakikosa na mzizi wa ‘metafizia na ontolojia’ huishia kutuletea >‘ism’ na ‘schism’<, vile kwenye Urastafari husemwa -- Bob Marley kupata kuimba katika wimbo >‘Get Up, Stand Up’<; vile huja kuwa kutokana na maarifa yanayowatenganisha watu kutokana na makambi ya mafikara na mlengo wa vitendo katika kuwatazama watu na kuwakadirisha hivi ama vile--kwa labda jinsia, umri, rangi ya ngozi, ni wapi anatoka n.k

Fikra na mawazo kuhusu jambo si ukweli wa mambo hasa—haijalishi watu wenye kushiriki fikra hizo ni wengi ama kidogo… Kufuatishwa kwa wazo ama fikara na watu wengi hukufanyi jambo linaloshikiliwa kusadikiwa na wao kuwa ni sahihi ama kweli. Katika dunia ya leo, Elimu 1.0 inatumika hata >‘kuwajaza watu mafundisho’< ama hata ‘propaganda’ pasipo na watu kuhoji mapokeo yao ikiwa ‘yana vina vya tafsiri’ isiyo na chembe ya shaka ama vipi. Falsafa ya elimu ya leo mashuleni si lolote bali ‘ufikirifu’ wa juu juu wa mambo usio na ‘msaada’ katika ‘kuwaunganisha watu’ kweli kweli.

Shule zote za leo duniani, katika mikondo rasmi ya mifumo ni ‘nyumba za vifungo’--vifungo vya namna zote za ustaarabu wa kileo ambao nao pia ni ‘Kifungo cha Mfumo Babiloni’. Mtu anahitaji kujikwamua na fikra na mawazo yote ya ‘kufikia’ katika jamii yake, ambavyo ni liberiti’ katika mtu. Uhuru wa kwanza wa mtu upo kwenye kuondoa ujinga, huu unaweza kumpatia mtu ELIMU 1.0 lakini uhuru wa pili ni liberiti—huu huja na huku kwa mtu kujinasibu na Elimu 2.0. Kwa kuwa Elimu 1.0 bado humtengenezea mtu ‘Utumwa wa Kiakili’; jambo ambalo Bob Marley aliliimba katika wimbo >‘Redemption Song—Wimbo wa Ukombozi’<…

‘Elimu 2.0: Uono na Ufikirifu Mifumo’ ndicho kile kinachokadirisha jambo la kusema ‘Hekima ni Uhuru’, kwetu Tanzania, kutaasishwa kupitia Chuo Kikuu cha Kwanza cha Dar es Salaam kwa kauli mbiu hiyo… Chuo hichi kimeanza, na hata sasa kinaendelea kwa Elimu 1.0; lakini kusudi na azimio, kwa mujibu wa Maono ya Taifa—kadri lilivyoasisiwa na waasisi wake, akiwamo Mwalimu Kambarage Julius Nyerere, ni siku moja hichi kiwe ni ‘Mwenge wa Liberiti’ kupitia Elimu 2.0…

Kiouno na ufikirifu mifumo, wasomi wote ambao ‘wameelimika’ kwa muktadha wa Elimu 1.0 lakini hawajafanya jitihada zozote za kuhama kutoka Elimu 1.0 kuelekea Elimu 2.0 anayoadha ya ‘Utumwa wa Kiakili’. Dhamira na Matendo yao, juu ya utaasisi wowote, hayatoakisi chochote tofauti, ama tuseme kuzidi, ya yale wanayofundishwa mashuleni na vyuoni -- hali hayo yote yana asili ya kujenga mifumo piramidi—nasibu ya wachache kuwatawala wengi, yaani >u-Eliti<.

Urastafari unalingania ‘Utaifa’, na kunasibu Taifa hili na bara la Afrika na Watu wake; ni jambo hili lilikuwa kwa waasisi wa Taifa letu la Tanzania na viongozi walijitoa kidhamira na matendo ili uhuru dhidi ya ukoloni usiwe tunu ya hapa na pale ndani ya bara. Uono na Ufikirifu wa Waasisi hawa juu ya Dhamira ya hawa waasisi ilikuwa ni kuwa Taifa Moja ‘haliwezi kuwa huru’ na hali jingine pembeni yake ‘likiwa si huru’. Jitihada za Mwalimu Kambarage Julius Nyerere katika kuunga mkono harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika kwa vitendo, na tena kwa hali na mali, ilikuwa ni moyo mkuu kwenye kuziishi kauli na kutekeleza azma. Hata leo hii, labda tu watu ni wenye kusahau—ama labda kutozingatia?; wimbo wa Taifa wa Tanzania, unaoimbwa mara kwa mara mashuleni na kwenye matukio makubwa ya Kitaifa, huazimisha Nia ya kusimama kwa Bara la Afrika na Kisha Tanzania…

Kauli za imani, shauku na Matazamio katika ‘wimbo wa Taifa’ zinashahibiana na maudhui ya utamaduni wa Kirastafari. Bob Marley alivyoimba ‘Africa Unite—Afrika Ungana’ alikuwa akisadifu mashauri yale yale ya kulingania watu wa Afrika kuungana ili waweze kusogea kutoka kwenye mfumo mmoja wa ‘kibabiloni’ na basi kuuendea ule wa ‘Baba’. Kwamba, Waafrika waamke na kuungana kwa manufaa ya watu wake na watoto—la leo lisisubiri kesho… Na basi ‘Baba’, kwenye >Wimbo wetu Taifa< ndivyo twataja ni ‘Mungu’… Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania… Kwamba, sisi tu ni watoto wa Afrika--watoto wa Tanzania… Hekima, Umoja na Amani iwe ndiyo ‘Ngao’ ya Viongoza njia kuelekea kulijenga Bara la Afrika; na kutokea kwetu hasa--Tanzania, Kudumisha Uhuru na Umoja, katika jamii ya wake, waume na watoto viwe ni njia ya baraka na uzima kwa Taifa...

Kiuono na Ufikirifu Mifumo, nguvu za ushawishi wa jamii kukaa pamoja asili yenye kufangamana na ‘muundo mkuu’ wa watu, nyakati na taasisi. Haya, walau kupitia Elimu 1.0, tunayafikia kupitia mashauri ya kisosholojia -- kuhusiana na fanusi jamii, nadharia migongano na muingiliano wa alama oanifu. Kutokea kwenye ‘Elimu 3.0: Ilimu ilivyo ni metafizikia ya Elimu’, ndiyo twaja kubaini ni namna gani ‘muundo mkuu’, ‘nyakati’ na ‘taasisi’ ni muktadha wa ‘Metafanusi’ kwa sura na miendendo ya jamii…

Kwa hivi, kwa neema ya Elimu 3.0, Mungu ni ‘Metafanusi’ ya jamii yoyote, kiumbe chochote sentienti—iwe mtu-ardhini, nyangumi-majini, vinyamkera-hewani, majini-plazmani, sayari, mfumo wa Jua na hata ulimwengu wote mzima. Ikiwa mtu hana Elimu 2.0 yenye kukirimika neema za Elimu 3.0 basi atabaini ukweli wa ‘Metafanusi’ hata kwa ‘upofu wa kiroho’--kuamini ama kusadiki chochote alhali hicho ni chenye kufanania na ‘imani’ yake kwa wakati, ‘upeo wake wa uono’ na ‘uwezo na vina vyake vya tafsiri akilini mwake’ kwa yale mambo yajitokezayo katika mazingira yake…

Hili litupe daraja ya kuanza kujinasibu na mambo yaliyositirika…

Kiufundi, hauwezi kuunda taifa thabiti ‘kwa maneno’ na maelekezo rahisi. Walau, kinachowezekana ni kuijenga jamii kutoka nje, kwa kutumia amali za nchi huku ukitaasisha ‘alama’ za utaifa na kuzienzi ‘tunu’ zozote zinazoweza kubayanika katika jamii inayoelekea kudumu kukaa pamoja. Kwa ukweli huu huu ni vigumu kuwaunganisha watu na huku kumbe kila mtu katika jamii hiyo anasadiki lakwake—kuhusiana na ‘muundo mkuu’ wenye nasibu ya kutawala ustawi wa maisha yake. Hili ndilo kati ya mambo magumu ambayo waasisi wa Taifa la Tanzania walishughulika nalo, na Mwalimu Kambarage Julius Nyerere alikuwa akilifahamu hata kwa ‘Jicho la Ziada’…

kuliinua taifa kutoka umma wa makabila zaidi ya 120, yenye mila na desturi mbalimbali; huku ukijitahidi kabisa kuepusha ‘ukabila’ katika taifa jipya ama kasumba ndiko kulitatuliwa na ‘lugha ya Kiswahili’ pia utayari wa nidhamu/uwajibikaji kwa ‘Elimu na Utumishi’ kokote. Katika siku zetu za awali Kitaifa, mtu kutoka Dodoma kwenda kusoma Moshi, tuseme kutoka elimu ya msingi kwenda Sekondari; na huko Moshi kukutana na wenzake kutoka Mikoa mingine mbalimbali—labda Kagera, Mara, Tabora n.k si kulipunguza ama kuondoa ukabila na ukanda—hili ni sehemu ya uhandisi jamii. Haya mawili si tu yametuletea utangamano, pia yametuletea ‘kuoleana’ na ‘muingiliano’ wa kimakabila usioendekeza kasumba na ubaguzi… Vile Mwalimu Nyerere alikuwa akipiga marufuku kasumba za kuulizana makabila—kana kuwa je, tunataka kutambika?

Kwa mtu wa Kiuono na Ufikirifu Mifumo, Mafanikio ya jitihada za Mwalimu Kambarage Julius Nyerere katika kulijenga Taifa la Tanzania, kwa kipindi cha miaka 60+ ya hii leo, ni mkubwa sana na tena ya kipekee sana katika historia yeyote ya karibuni hapa Duniani; ipo namna ya kuona pia alilolianzisha bado linaendelea—halikufika mwisho.

Kutoka kwenye stawi za kimakabila na kuelekea ‘Utaifa’, katika nchi ya Tanganyika na kisha Tanzania, ni jambo lililohitaji maarifa na sanaa ili kukadirisha muktadha wa sura ya mienendo na maendeleo ya jamii. Kuzibuni na kuzitaasisisha mila, desturi na mapokeo mapya ya utaifa, kwetu Tanzania, busara na hekima vilitumika kwa matatu yaliyo ni fasaha, dhamira na makusudi yake—‘Dhana ya Uhuru’, ‘Ukombozi wa kifikra na Maendeleo’ na ‘Kuujenga Umoja wa Kitaifa’… Haya matatu, kwa sanaa ya utaasishaji wa alama oanifu, ndiyo huwakilishwa kwa alama ya ‘Bendera’--usovereini wa nchi-taifa, ‘Mwenge wa Uhuru’--Mwangaza kwa Maendeleo na kujichagulia; na ‘Wimbo wa Taifa’-- nadhiri katika watu kuhusiana na utaifa wao na mustakabali…

kiuono na Ufikirifu mifumo, kutokea kwenye daraja la Elimu 3.0, Ilimu ilivyo ni Metafizikia ya Elimu, ushiriki wa watu kama kikundi katika matendo, mazoea na tabia, na zaidi ‘kaida’ za imani huleta udumifu wa sura ya jamii na tena kwa wakati wake. Kukongoroa hivi huweza kusambaratisha jamii inayoshiriki hayo, lakini kati ya hivyo vyote--’kaida’ za kiimani ndizo zenye nguvu katika mashikizo ya taasisi za watu. Mfano wa ‘kaida’ za kiimani, ni matambiko…Kwa hivyo, Elimu 3.0 inaweza kuleta ufunuo, ni namna gani ‘mizimu’,’maruhani’, ‘miungu nchi-taifa ama dola-jiji’ n.k hupata ‘pumzi ya uhai’…

Kutoka kwenye ‘mifumo ya kikabila’ hadi ‘mifumo nchi-taifa’ Tanzania kama taifa kuna tunayoyapoteza na kuna mapya tunayoyajenga. Labda ni vema sana kujua tulikotoka ili tujue tunakokwenda… Kwenye fremu-kazi ya uono mifumo kwa ajili ya mambo ya ‘machaguo ya kitaasisi, ‘Jamii’, ‘wakati’ na ‘matukio’, jambo hili huchanganuliwa kitopografu kwa mahusiano ya ‘Kumbukumbu/Uzoefu’…

Kiuono na ufikirifu mifumo, utatu wa mihimili ya imani kwa ‘fanusi mtu/jamii’ hufanywa na ‘Jaala’, ‘Kumbukumbu/Uzoefu’ na ‘Wakati’… Hii ni namna ya kubaini kwamba mtu ama jamii huwa na vipawa vya akili kumfaa yeye/yenyewe na ‘kumbukumbu/uzoefu’ ili apate kujitambua msimamo ama mustakabli wake kiwakati. Wakati una usiku na mchana, asubuhi-mchana-jioni, masika-vuli-kiangazi-kipupwe kulingana na jiongrafia na mazingira. Kumbukumbu/uzoefu wa kuendana na haya mambo ya nyakati ndiyo hadhi ya ‘uwezo au uduni’ wa mtu kuyamudu mazingira yake—Elimu basi, ndiyo shughuli ya ziada inayoweza kuchochewa kwa mtu/jamii kusudi mtu/jamii iweze kujikwamua kutoka kwenye sura duni/hafifu ya ustawi, kulingana na vitendo vya miundo ya jamii yake, hadi ile bora. Hatua kutoka kwenye sura duni hadi sura bora ya ustawi wa jamii ndiyo dhana hasa ya ‘Maendeleo’.

Elimu 1.0: Kujua kusoma na kuandika, kwa mapana ya ujumla wake ndiyo huwa na shabaha kumpa mtu/jamii maarifa ili ibaini uduni wa hali na utendaji wake wa kila siku; kuufuta ujinga kwa kuipatia jamii na wanajamii wake ‘fikra’, ‘ujuzi’ na ‘maarifa’ kwa ‘visomo rasmi’. Kiuono na ufikirifu mifumo, Elimu 1.0 inasaidia sana jamii kupata taarifa na ufahamu wa mambo kufaa ’kumbukumbu la mtu’ na si zaidi. Walau katika hii, Taarifa/Habari ni nguvu… Mtu mwenye elimu, kwa sura hii, anawezakuwa ni mtendaji bora kulingana na maarifa aliyoyapata – pale ambapo huyu alinganishwa na yule asiye na hayo maarifa.

Elimu 1.0: kujua kusoma na kuandika, haina majibu hasa ya ‘ukweli wa mambo’ ila tu kwa habari za kuandikwa, kusimulika, kudadavuliwa na fasihi. ‘Ukweli wa mambo’ kwa Elimu 1.0 ni kitendawili, kila mtu/mwanajamii hubidi ‘hutoa mji’ ili kiteguliwe… Hii ni kwa kuwa Elimu 1.0 hutegemea na ‘kiu ya mtu’ ya mtu kutafuta maarifa, na kama vile tusemavyo Wabantu, ‘kimfaacho mtu ni chake’… Ikiwa mtu/wanajamii wanaridhika na vile vilivyo—kwa maandishi, simulizi na mapokeo, kadri vipatikanavyo katika jamii husika, basi yote yanayoambatana na ‘kujua mambo’ kwa sehemu – iwe ni kwa ‘kina’ ama ‘ujuu juu wa mambo’; basi hivyo ni halali yao.

‘Upokeaji’ ama ‘utayari’ kwa Elimu 1.0 katika mtu huratibiwa na ‘hali ya kujisikia’ ama ‘kuhamasika’ katika mtu/mwanajamii. Hili ndilo linaloingiliana na >‘tabia za kuigana’< kama ‘chachu’ ya mabadiliko ya jamii. Kuna namna ya kuona binadamu kama kiumbe ana ‘matatu katika moja’ ilivyo ni (1)Mwili, (2)Imosha (hisia) na (3)Roho… Vitatu hivi katika moja ni sehemu ya muktadha wa ‘mbegu’ ya kuwa kwamba ‘akipandacho na kukivuna’, mtu ama jamii, katika jamvi la ‘wakati’.

Matukio yote katika maisha ya mwanadamu, ndiyo basi kusema ni ‘kuvuna ama/na kupanda’ yale yote yafanyayo ‘ustawi’ ama/na ustaarabu wa mtu/jamii husika.

Mtu ni mwenye nasibu ya kuiga kutoka kwenye ‘matendo ya asili/dhahiri’ ama ‘matendo ya mwanajamii’ mwingine kama sehemu ya ‘kuotea’ maarifa. Kadiri mtu aridhikavyo na ‘kawaida’ ama ‘kaida’ ya matendo ya jamii, huyu pamoja na wanajamii wenzake hufanya muktadha wa ‘desturi’. Na yale matendo ya kujirudiarudia katika jamii ndiyo visomo vya leo kisosholojia hufahamika kama >‘nomu mahsusi/nomu jamii’<; nomu, tunatohoa kutoka kwenye neno la Kiingereza ‘norm’--kawaida ya jambo/mambo. Basi ndivyo hivi sisi wabantu husema ‘Kawaida ni kama Sheria’… Kwamba katika jamii, Mazoea hujenga Tabia…

Sehemu ya Maarifa isiyofasaha katika jamii, itokanayo na mambo ya kuigana, ndiyo hufanya ‘mila’ za wanajamii. Mila ni muktadha wa matendo ‘usiohojiwa’ kwa wanajamii, bali kufuatishwa na kuenziwa kutokana na ‘busara’ za ‘wazee’ ama pia ‘Wahenga’. Hili kuwa kana kwamba, mila ni daraja la jamii kupata ‘baraka’, ‘kinga’, ama pia ‘bahati’ kwa kadiri ya kufuatishwa kwake na tena kwa taratibu zake. Kwa hivyo kiufundi, mila ni ‘utaasisi’ juu ya ‘jaala na wakati’ kwa wanajamii. Mila ndiyo msingi wa ‘mema’ ama ‘mabaya’ ambavyo kufuatishwa ama kutofuatishwa kwake huonekana, kwa kusadiki, ni chanzo cha ‘mapatilizio’ ama ‘thawabu’ kwa wanajamii…

Kwa mujibu wa ususi wa Taifa letu la Tanzania, kati ya adha kuu zilizopata kuwa ni kigingi kwa mageuzi ya kijamii ilikuwa ni utitiri wa ‘mila na desturi’ za makabila mbalimbali yaliko katika mipaka ya ‘nchi-dola mpya’. Yumkini watu wengi hata leo hii(2022), hawang’amui wala kubaini mambo ya ‘kiufundi’ yaliyohusika ama/na yaliyopitiwa na viongozi waasisi wa taifa hili, miongo ya awali, baada ya kupata ‘uhuru’. Ikiwa watataka kufahamu basi inawapasa kuwa na mapana sahihi ya maarifa juu ya ‘sosholojia’ na ‘uhandisi jamii’.

Elimu 1.0: Kujua Kusoma na Kuandika, tokea siku za awali za kupatikana uhuru wa taifa, ilikuwa na makusudi si tu kuwapitia ‘taarifa’ na ‘maarifa’ wanajamii ya Tanzania(Tanganyika) juu ya taratibu za maisha bora—yakuendana na mambo ya walimwengu kungine kote duniani; hii ilikuwa inakusudiwa pia kutokomeza ‘mila na desturi’ potofu za hao hao wanajamii.

Kutokomeza ‘Mila na Desturi’ potofu, haijawahi kuwa jambo rahisi kokote duniani… Mila na desturi ni ‘Utaasisi’; hivi hufangamanisha ‘miundo ya kijamii’, ‘kujisikia’ na ‘ushawishi’… Haya ndiyo kwa mfano, hufanya koo na uchifu kwa makabila yetu ya Kiafrika. Chifu kuwa ndiye >‘Bwana wa ma-Bwana’< na Baraza lake kuwa ni ‘Wazee wa ki-Mila’. Kazi ya Wazee wa ki-Mila ndiyo kusaidia utawala wa Chifu-- >Washiriki-kwa-Kina<, kwa ‘mambo ya jadi’ na >‘Ufundi wa Mizungu’<…

Labda watu wengi, wamepuuzia kama si kujisahau juu ya misingi ya mila na desturi zetu kama watu wa makabila anuai kutoka katika vizazi vyetu humu barani Afrika. Kuna mambo ni vema wanajamii wakayatafuta na kuyadadisi ili wapate vina sahihi vya maarifa na ukombozi wa kifikra. Kutokufanya hivi, wanaweza kujidanganya kufikiri wamepiga hatua na kumbe bado ni ‘wabichi’ katika dhana na tafsiri ya ‘maendeleo na ustaarabu’.

Marja Liisa Swantz, almaarufu 'Mama Maendeleo', ni miongoni mwa wanavisomo wengi ambao wamefaulu kufanya visomo maridhawa juu ya jamii zetu za asili pasi kasumba yeyote, na kuleta hazina ya kipekee ya Kisomo Elimu 1.0, kwa mfano yeye kutuletea: >'Kaida na Alama katika Jamii Mabadilikoni ya ki-Zaramo--Ritual and Symbol in Transitional Zaramo Society'<. Humu anaeleza mengi, kuhusu maisha yake nchini Tanzania kipindi cha mabadiliko makubwa ya Kijamii, akitumikia jamii ya Mwambao, Bunju. Kutoka katika jamii hii yeye alipata fursa ya kufahamiana na wenyeji kadhaa; na kutoka kwao kujifunza; na pia kufanya kisomo kuhusu mambo ya watu wa kabila la Wazaramo--mila na desturi, imani na mazoea yao... Haya yote akiyabaini katikati ya mabadiliko ya ‘Kitaifa’ kutoka kwenye 'sura ya mienendo ya kiasili' kuelekea katika harakati na pilika za kutekeleza 'Siasa za Ujamaa na Kujitegemea'…

Mama Marja Liisa Swantz, ni mfano wa 'Waafrika' kwa moyo, ‘Wazungu kwa Asili ya Mwili’... Hawa, tunaoweza kuwaita ni ‘raia wa ki-geni’ kwa macho ya juu juu na utaasisi wetu wa kileo juu ya uzalendo, wamekuwepo, wapo, na wengine watakuja, kutokea kote mashariki-magharibi-kaskazini-kusini na 'kuimalizia kazi'... Tutakuja kuyafahamu mengine mengi kuhusiana na hili kupitia Elimu 3.0...

Kwa mtu Uono na Ufikirifu Mifumo, Mambo ya ‘Elimu 1.0’ pamoja na ‘Mila na Desturi’ ndiyo huleta muktadha wa ubainufu wa >‘elementi ya Kiza’< katika jamii yoyote; jana leo na kesho. Elementi ya Kiza ni ile sifa ya mtu kuwa na sehemu ya yeye, >asiyofahamu ama kujifahamu<, na huku hiyo ikiwa ni sehemu ya ‘uzima’ wa maisha yake na mwenendo wake kama mtu mmoja ama jamii. Hii ni matokeo ya ‘mwangaza’ alionao juu ya ‘hisia zake’ na ‘vina vya tafsiri’ kwa >‘uono’< wa >‘ontolojia ya Taasisi’< zake na >‘Sura na Mienendo’< ya jamii yake… Kukosa mwangaza kamili katika kuyamulika haya, ndiko humfanya mtu >kujua mambo kwa sehemu<, na basi yeye atayaishi maisha yake kadiri ya vile Elimu 1.0 ya sosholojia itazungumza kwa minajili ya >‘fanusi jamii’, ‘nadharia migongano’ na ‘Muingiliano wa alama oanifu’<…

Kwa hivyo kwa mtu wa Uono na Ufikirifu Mifumo, suluhu ya adha za ukomo wa manufaa ya 'Elimu 1.0', 'Mila na Desturi' na pia 'Elementi ya Kiza' ipo katika jambo tunaloweza kulibayanisha ni >'UPENDO'<. Ili mtu kunasibika 'nuru ya ufahamu' juu ya fanusi zake jamii, nadharia migongano na muingiliano wa alama oanifu, huyu hana budi kuwa na 'hisia' na 'vina vya tafsiri' tofauti na makundi ya watu wasio na upeo ama kukosa kujua ilivyobora…

Kama vile tunavyoweza kuona katika Urastafari juu ya ‘Upendo JAH’, ‘Pendo Moja’ na ‘Udugu I’n’I’, Kumuona mwingine kwapasa kuwa ni Kujiona mwenyewe kadri Akuonaye wewe, ndiye amuonaye mwingine – mlivyo wote ni ‘Moja’… Kiufundi hii ndiyo ile asili ya >‘Jicho la Upaji’< kama alama ‘fumbo’ ya >jumuiya siri ya Illuminati<, japo alama yenyewe ni ya siku nyingi kupita mwanzo wa Illuminati yenyewe ya kuanza na Adam Weishaupt... Jambo kama hili hili kuwa ni asili ya usemi >lak'ech ala k'in< kwa staarabu za Mayani, Amerika ya Kati ya Zamani…

Kwa mtu wa Uono na Ufikirifu Mifumo, vile katika sayansi huzungumzwa ya >'Muona ni Muonwa'< katika ulimwengu wa fizikia ya kikwantumu, ni topografu sambamba na haya yote ya 'utabia wa kichanzo' na basi pia 'Ontolojia ya Taasisi'. Hivi ni sawa sawa na kusema, >kupitia kila mmoja wetu sentienti, Mungu ni jicho lionalo kote na mote< na hali kumbe >'ufahamu pofu wa milango sita'< wa kiumbe huwa na 'kibanzi/pazia' katika ile sifa na hadhi ya kukosa ubayanifu wa ukweli wa jambo. Kwamba mtu, si mkamilifu--akipata ukamilifu atang'amua, mambo yake yote--ustaarabu wake wote na ustawi, kabla ya ukamilifu kufika, umepata kuwa ni 'utoto'. 'Atajijua' kama vile 'Ananavyojulikana'--na hili ndilo labayanisha muktadha wa >'kukumbuka, kujikumbuka na Kukumbukwa'<.…

Wakati mmoja, siku za mbele, ‘Muona ni Muonwa’ ndiyo itakuwa alama yunivasali ya ‘ujuzi na uwezo wa kubaini sura nyingi za mambo kwa wakati’--intelijensia...

Haya yote yanatukaribisha kwenye ‘Elimu 3.0: Ilimu ilivyo ni metafizikia ya Elimu’…

...
-_-

 
Kama kawaida Mzee Said ukija na andiko basi una malengo yako fulani, na hapa ni kujaribu kupindisha ukweli wa mambo.

Unarejea kwenye hotuba ya Mwalimu wakati anawaaga Wazee wa Dar es Salaam lakini ni kama unaruka kwa alichosema.

Na niliwahi kuchangia hili kwenye moja ya nyuzi ulizowahi kuleta hapa jukwaani, haswa nikipingana nawe kung;ang'ana kutaja Wazee fulani tu huku Mwalimu alikuwa anawataja Wazee wa Dar Es Salaam kama Washiriki wakuu.

Na lengo la Mwalimu kuelezea yale ilikuwa ni kuonesha ni kwa jinsi gani alishirikiana na Wazee hao wa Dar Es Salaam na hata kulazimika kushiriki baadhi ya mambo yaliyokuwa magumu kwake...na alisema "mimi ni mkorofi kidogo kwenye mambo hayo.." na hapo zaidi alimaanisha mambo ya matambiko au "nguvu mbadala"...na sidhani kama alikuwa na tatizo sana na Dua kama zisingeambatana na matendo yasiyo rasmi.

Na kuna mfano mmoja alitowa kuwa kuna wakati alihisi kuumwa kichwa akaomba Aspro, akaambiwa asubiri...na baada ya kufuturu maumivu yaliisha...ndio akasema kumbe kichwa kilikuwa kinauma kwa sababu ya njaa...walikuwa kwenye mfungo...hivyo Dua pekee haikuwa tatizo....sasa kama kuna kuchanganya Dua na matambiko hilo ni shauri jingine.

Hivyo si kweli kwa unavyojaribu kusema kuwa hakukuwa na matambiko. Alilazimika kwenda Bagamoyo, sasa walifuata Dua huko? Wazee walichimba shimo wakachinja Beberu damu ikamwagikia shimoni wakamtaka Mwalimu aruke...akaruka Wazee wakamwambia "Twaining umekwisha"...hii ni Dua au tambiko?.

Ni si hakika kwa unavyojaribu kutaja idadi ya Dua ili hali hukuwepo kila alipoenda Mwalimu, ni hali ya kawaida tu kuamini ya kuwa kila Mtu au kikundi walijaribu kutekeleza imani kwa upande wao kuona malengo yanafikiwa.

Labda unataka kutofautisha waliokuwa wanatekeleza Dua na wale walitekeleza matambiko...vyovyote lakini hayo yote hayakuwa upande wa imani ya Mwalimu lakini alilazimika kushiriki ili aende sawa na Wazee.
 
Kama kawaida Mzee Said ukija na andiko basi una malengo yako fulani, na hapa ni kujaribu kupindisha ukweli wa mambo.

Unarejea kwenye hotuba ya Mwalimu wakati anawaaga Wazee wa Dar es Salaam lakini ni kama unaruka kwa alichosema.

Na niliwahi kuchangia hili kwenye moja ya nyuzi ulizowahi kuleta hapa jukwaani, haswa nikipingana nawe kung;ang'ana kutaja Wazee fulani tu huku Mwalimu alikuwa anawataja Wazee wa Dar Es Salaam kama Washiriki wakuu.

Na lengo la Mwalimu kuelezea yale ilikuwa ni kuonesha ni kwa jinsi gani alishirikiana na Wazee hao wa Dar Es Salaam na hata kulazimika kushiriki baadhi ya mambo yaliyokuwa magumu kwake...na alisema "mimi ni mkorofi kidogo kwenye mambo hayo.." na hapo zaidi alimaanisha mambo ya matambiko au "nguvu mbadala"...na sidhani kama alikuwa na tatizo sana na Dua kama zisingeambatana na matendo yasiyo rasmi.

Na kuna mfano mmoja alitowa kuwa kuna wakati alihisi kuumwa kichwa akaomba Aspro, akaambiwa asubiri...na baada ya kufuturu maumivu yaliisha...ndio akasema kumbe kichwa kilikuwa kinauma kwa sababu ya njaa...walikuwa kwenye mfungo...hivyo Dua pekee haikuwa tatizo....sasa kama kuna kuchanganya Dua na matambiko hilo ni shauri jingine.

Hivyo si kweli kwa unavyojaribu kusema kuwa hakukuwa na matambiko. Alilazimika kwenda Bagamoyo, sasa walifuata Dua huko? Wazee walichimba shimo wakachinja Beberu damu ikamwagikia shimoni wakamtaka Mwalimu aruke...akaruka Wazee wakamwambia "Twaining umekwisha"...hii ni Dua au tambiko?.

Ni si hakika kwa unavyojaribu kutaja idadi ya Dua ili hali hukuwepo kila alipoenda Mwalimu, ni hali ya kawaida tu kuamini ya kuwa kila Mtu au kikundi walijaribu kutekeleza imani kwa upande wao kuona malengo yanafikiwa.

Labda unataka kutofautisha waliokuwa wanatekeleza Dua na wale walitekeleza matambiko...vyovyote lakini hayo yote hayakuwa upande wa imani ya Mwalimu lakini alilazimika kushiriki ili aende sawa na Wazee.
May Day,
Najaribu kuliangalia hili suala la tambiko kwa upande wako na pia naliangalia suala hili kwa upande wangu kama Muislam.

Huwa tunafanya dua kisha yule anaefanya hiyo dua akasimama kwa mguu mmoja kaelekea kibla.

Anaweza mtu akatafsiri kitendo cha kusimama kwa mguu mmoja kuwa hilo ni tambiko.

Hapana neno iwe ni dua au tambiko wafanyaji ni walewale ambao walikuwa bega kwa bega na Mwalimu.

Lakini nataka nikueleze kitu katika hotuba ya Mwalimu Nyerere kuwa ina mambo ambayo hayakukaa sawa.

Mwalimu anasema anadhani Abdul Sykes alikuwa Secretary.

Mwalimu kwa miaka yote aliyoishi na Abdul Sykes hakumjua Abdul Sykes ni nani.

Mwalimu anasema mambo yalisinzia yeye ndiye alikuja kuyafufua.

Ukweli ni kuwa yeye alipochukua uongozi ndiyo TAA ikafifia.

Mwalimu kaeleza uchaguzi wa Arnautoglo lakini hakueleza alichaguliwaje na aligombea nafasi ile dhidi ya nani.

Mwalimu anazungumza kuhusu kuandika katiba.

Katiba ya TANU ilinakiliwa kutoka katiba ya CPP ya Kwame Nkrumah.

Mwalimu anasema safari yake ya kwanza ilikuwa Mbeya.

Safari yake ya kwanza ilikuwa Morogoro na aliongozana na Zuberi Mtemvu.

Hii hotuba ina mengi ambayo nadhani kwa kuwa miaka ilikuwa mingi imepita na hii kuwa historia ambayo haikupewa umuhimu na kuhifadhiwa Mwalimu kuna mengi amesahau.
 
May Day,
Najaribu kuliangalia hili suala la tambiko kwa upande wako na pia naliangalia suala hili kwa upande wangu kama Muislam.

Huwa tunafanya dua kisha yule anaefanya hiyo dua akasimama kwa mguu mmoja kaelekea kibla.

Anaweza mtu akatafsiri kitendo cha kusimama kwa mguu mmoja kuwa hilo ni tambiko.

Hapana neno iwe ni dua au tambiko wafanyaji ni walewale ambao walikuwa bega kwa bega na Mwalimu.

Lakini nataka nikueleze kitu katika hotuba ya Mwalimu Nyerere kuwa ina mambo ambayo hayakukaa sawa.
Je inaswihi kumuombea dua kwa asie muislamu? Je inaswihi kumfanya kiongozi wenu asie muislamu?
 
Back
Top Bottom