Visomo (Dua) Sita Zizofanywa na TANU Mwalimu Nyerere Akishiriki Wakati wa Kupigania Uhuru 1954 - 1961

May Day,
Najaribu kuliangalia hili suala la tambiko kwa upande wako na pia naliangalia suala hili kwa upande wangu kama Muislam.

Huwa tunafanya dua kisha yule anaefanya hiyo dua akasimama kwa mguu mmoja kaelekea kibla.

Anaweza mtu akatafsiri kitendo cha kusimama kwa mguu mmoja kuwa hilo ni tambiko.

Hapana neno iwe ni dua au tambiko wafanyaji ni walewale ambao walikuwa bega kwa bega na Mwalimu.

Lakini nataka nikueleze kitu katika hotuba ya Mwalimu Nyerere kuwa ina mambo ambayo hayakukaa sawa.
As salaam alaykum Sheikh Mohamed,

Warahmatullahi Wabarakatuh,

Dua ni ufundi na Elimu ya aina yake... Ipo na watu na makabila yote; na ni utundu wa madaraja ya 'utu' na 'ufunuo'.

Kwenye jamii nyingi maarifa ya dua, matambiko na imani yana 'utaratibu wake'; ni maarifa 'yaliyokatazwa' kwenye dini kubwa karibia zote japo kimsingi dini zote zina mambo ya mifumo na kaida za kujinasibu na hayo yote.

Haya, kiukweli hasa, si mambo ya uholela wa 'kutangaza' hadharani kama 'taarifa ya habari'. Ndiyo maana huwa na 'jumuiya zake za siri' hata ndani ya mifumo ya tawala za dini, jamii, koo ama hata taifa. Siyo kwamba hayafundishiki ama 'roho mbaya' tu kwamba wengine wanayajua kwa vikundi huku wengine wengi hawayajui vema/fasaha, la hasha!

Adha kuu ni kuwa, kuna namna uwajibikaji wa kuyafahamu haya 'unataka kifua'--hichi kifua si kila mtu anacho. Vile vile, kuna mawili yanawezekana kwa mtu yeyote anayejinasibu na hayo--anaweza akawa 'mchawi' ama 'mganga', tumaanishavyo wabantu; kwa kuwa 'utundu' kwa mazingara na maumbile hufangamana na hayo. Jamii nyingi zilifikia kupiga marufuku mambo ya 'ushirikina' kwa sababu mambo yake haya hayakawii kuja na 'sumu' za 'makusudio yenye kuharibika'--ulonzi, imani potofu na ubatili...

Ndiyo, ni rahisi mtu kukanusha kuwa dua hii na ile haimbatani na 'shirki'; kiufundi anayedai hivi hajui ukweli wa mambo... Ulimwengu wote una namna iliyoshikiliwa na nguvu za alama na muoano wa alama, mtundu yeyote wa hizo alama anaweza kutumia huo mwanya kufanya 'maajabu'; na ili aweze hilo ndiyo hutumia hata manuizo, kaida (kama hilo jambo la kusimama kwa mguu mmoja--ni mkazo wa nia na dhamira kwa kusudi la fikara italawayo kusudi la kaida yenyewe, na hapo hushirikishwa na 'mmoja mwenye nguvu' ama 'jeshi lake') ama dua. Katika dini, dua ni kuita 'uwepo'--wa 'malaika', ama 'Mungu' mwenyewe ili umshirikishe na dhamira yako... Kwa hivyo dua zina utundu wake, ndiyo maana huwa zina 'masharti'--masharti ya 'shughuli' si chochote bali muoana wa mazingira rafiki kwa muktadha wa kukamilisha 'ombi' na 'majibu'...

Sasa labda tusilazimike kuzungumza kuhusu 'kafara' na 'dua' vinafungamana vipi; ni jambo ambalo 'linakugusa moyo' wa 'kaida' za turufu za jamii na mifumo--labda mpaka ELIMU 2.0 iwe imekomaa katika umma basi, tutakuwa huru kabisa kuzungumza hilo kwa ufasaha wake kabisa...

In Shaa Allah, tuombe kheri tufae kuyafahamu haya yote kwa jicho jema...
 
Mose,
Waleikum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh.

Ahsante sana.
 
changamoto tu ni kwamba huwezi kumaliza kuandika uzi bila kuweka neno [uislamu]. Nadhani ni vizur tu ukataja tukio husika na kuwataja walio husika inatosha mzee wangu. Hakuna ulazima wa kutanabaisha maswala ya dini zao. Hii nchi yetu sote. Wazee wetu wote waislam kwa wakristo mpaka wapagani waliipambania kwa ajili yetu sote bila kujalisha kundi lipi lina mchango mkubwa kuliko kundi jingine. Walisimama na msimamo mmoja tu. Kuipgania TANGANYIKA,
Yaa anafanya hivyo kwasababu wewe pia huwezi kuzungumzia fact zingine zilizo kwenye chapisho baada ya kukutana na neno 𝙐𝙞𝙨𝙡𝙖𝙖𝙢, unalidiscuss hilohilo tu, kwo hasipoliweka utadiscuss nini wakati mengibe huyaoni??
 
Back
Top Bottom