Visomo (Dua) Sita Zizofanywa na TANU Mwalimu Nyerere Akishiriki Wakati wa Kupigania Uhuru 1954 - 1961

Mzee wangu Saidi nilitaka kukuuliza hivi!!!Kwani Watanganyika maeneo mengine hawakufanya matambiko kumuombea Nyerere asafiri salama mwaka 1955 kwenda UNO au Tanganyika ilikua kariakoo na Magomeni na maeneo ya pwani tu????Ebu tafuta historia za wadau wa Tanu miaka hiyo kama Siliwale wa Sanya na wale wazee wa Nyanza akina Mohamedi Sufiani,na wale wazee wa Western Province akina Mganga Nyambuke na yule aliyekua anajiita Mungu mtu pale ujiji wote walikua wanachama ndaki ndaki wa Tanu
Tai...
Yawezekana hayo kwa wengine lakini katika Uislam hakuna kutambika.

!!Ebu tafutafuta na hao utuletee historia zao pia!!!!Unatuelimisha mzee wangu ila kuna maeneo mengi ya Tanganyika unayaacha katika historia zako hasa yale ya bara na mchango wa wale wazee wa kibantu kusaidia uhuru!!!
 
Tai...
Yawezekana hayo kwa wengine lakini katika Uislam hakuna kutambika.
Kutambika ni neno la kibantu asili yake limetokana na neno tambika hasa kwa makabila ya eneo Congo basin na uwanda wa rift valley!!!Maana yake kwa kiswahili fasaha ni kutoa zaka au sadaka kwa kuchinja mnyama na kuweka vinywaji!!Uislamu kwa kua umeshahabiana kiarabu katika lugha zake za awali kabisa neno kutambika halipo lipo neno zaka au zakhar inategemea unaongea kiarabu cha maghreb au mashariki ya kati na kiswahili cha kimvita kinachotumika pwani ya afrika mashariki neno kutambika linatafusiriwa tofauti!!Kutambika maana yake maombi ya kuchinja mnyama na zaka!!!Sasa katika uislamu maombi ya kuchinja mnyama na zaka au zakhar yapo mzee wangu!!!Tumefanya sana pale magomeni kwa mzee wetu marehemu Sheik Yahaya katika shughuli mbalimbali!!!Kutambika ni neno tu la kibantu na kwa kiarabu ni zaka au zakhar na zaka katika uislamu zipo!!!!Ni lugha tu Mzee wangu usifikiri neno KUTAMBIKA ni la ajabu sana!!!!
 
Nelson...
Kuhusu kufanyika kwa dua ukweli ni kuwa kwa utafiti wangu nafahamu dua 5 na nimeandika historia zake hapa.

Hizi dua zilianza Dar es Salaam kwa kuwa hapa ndipo TANU ilipokuwa na nguvu Tanganyika yote.

Sehemu nyingine TANU iliingia kadri harakati zilivyozidi kupamba moto.
Kuhusu sehemu na wazalendo wengine ulionitajia hakika hawapo katika kitabu changu kwani singeweza kuandika historia ya kila jimbo, mji na wilaya.

Kuna sehemu hapakuwa na kitu yaani TANU haikuingia kwa haraka ilichelewa sana na sehemu hizo zinafahamika na sababu ya TANU kukawia kuingia zinafahamika.

Siwezi kurudia kuandika historia ya TANU mara mbili kwa kuwa historia ya TANU nimeiandika kwa kadri ya uwezo wangu nikiongozwa na harakati zilizokuwako.

Huwezi kufananisha historia ya TANU Kanda ya Ziwa na historia ya TANU Peramiho na Nachingwea.

Kanda ya Ziwa kulikuwa na Ali Migeyo.

Kiongozi wa TAA shupavu kiasi alipigwa mabomu katika mkutano akihamasisha wananchi kuwa wamoja kudai nchi yao.

Huwezi kwa kuwa TANU haikuweko Peramiho na sehemu nyingi za Southern Province ambako Kanisa lilikuwa na nguvu.

TANU ilikuwa Moshi mjini lakini haikuwapo Mgombani juu Kilimanjaro kwa sababu kwanza Kanisa lilikuwa na nguvu na pili Mangi hawakuiunga mkono.
 
Ni kawaida kwa wabasiasa kufanyiwa dua na yeyote yule.

Wataingia misikitini, makanisani, kwa waganga wa Jadi, machief wa Jadi.

Mwanasiasa kujiweka popote kawaida tu.

Leo utamkuta kavaa baraghashia msikitini, kesho utamkuta kansani, kesho kutwa kwa waganga nk.

Wala hii siyo stori.
 
Hapo nimekuelewa mzee wangu kumbe unaielezea Tanu ya sehemu chache chache kutokana ufahamu wako na historia uliyopata au kushuudia!!!Nimekuelewa mzee wangu
 
Mose...
Sijakutana na historia hiyo kuwa kulikuwa na maombi ya uhuru kanisani.

Wala sijukutana na historia ya waganga wa kienyeji nk katika utafiti wangu wa harakati za uhuru.

Ila kuna kisa cha mganga mmoja kutoka sehemu za kusini ya Tanganyika jina lake Nguvumali.

Kisa kinasema kuwa Nguvumali alikuwa anasafiri ndani ya basi anakuja Dar es Salaam kwa nia ya kumfanyia ubaya Julius Nyerere.

Basi likapinduka njiani kabla ya yeye kufika Dar es Salaam akafa.
Kuna historia ya Sheikh Issa Nasir mjumbe wa Baraza la Wazee wa TANU kutoka Bagamoyo.

Sheikh Issa Nasir alikuwa bingwa wa elimu na majini.

Huenda wale ambao hawakukulia katika mazingira ninliyokulia mimi hili jambo la majini likampa shida kuelewa khasa ni elimu gani.

Mimi kwa kuogopa mapambano sitaingia ndani zaidi kueleza.

Sheikh Issa Nasir ukiangalia picha kila alipokuwako Nyerere utamuona yeye kakaa karibu yake.

Mpashai wangu anasema kuwa hapo alipo na Mwalimu Sheikh Issa Nasir hayukoi peke yake yuko na ''askari'' wake ambao wewe huwezi kuwaona kwa macho yako haya ya kuvukia barabara.

Mwalimu akimpanda sana Sheikh Issa Nasir au tunaweza kusema wakipendana sana na alikuwa anaweza kuingia Ikulu muda wowote autakao.

Angalia picha hiyo hapo chini ya Baraza la Wazee wa TANU Mwalimu aliposimama chini yake kuwa watu wawili wamechutama huyo wa kulia mwenye fimbo begani ndiye Sheikh Issa Nasir.

Picha ya chini kulia ni Sheikh Issa Nasir akiwa Karimjee Hall siku ilipotolewa tarehe ya uhuru.

Hapo yuko karibu na Mwalimu Nyerere na jeshi lake kutoa ulinzi.
Askari wake hawaonekani.

Nimefaidi sana katika utafiti wa historia ya TANU na kuna mengi sikuyaeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.



 
Hapo nimekuelewa mzee wangu kumbe unaielezea Tanu ya sehemu chache chache kutokana ufahamu wako na historia uliyopata au kushuudia!!!Nimekuelewa mzee wangu
Nelson...
Hujanielewa.

Najua kinacho kutaabisha akili yako inakataa kukubali.
Hili si wewe peke yako.

Unatafuta upenyo wa kutokea.
Huwezi kuupata kwani haupo.

Wewe bado hujaamini kuwa mimi naijua historia hii kinyumenyume?

Unataka hii iwe si historia ya TANU.
Lakini hiyo niliyoandika ndiyo historia ya TANU.

Huko ndiko zilikokuweko harakati za TANU na nimetumia Nyaraka za Sykes kwani wao ndiyo waliounda African Association mwaka wa 1929.

Haiwezekani kwa yeyote yule kuja kuandika historia ya TANU nyingine zaidi ya hii.

Huu mwaka wa 25 hakuna aliyekuja na kitabu kupinga kitabu cha Abdul Sykes

Nyerere kaikuta TANU nyumbani kwa akina Sykes hakuja Dar es Salaam na fikra ya kuanzisha chama cha siasa.

Hakuna TANU ya sehemu chache.
Huko kwengine kulikuwa hakuna kitu.

Abdul Sykes anasema yeye kaona kwa macho yake akiwa mtoto wakati ofisi ya AA ikijengwa pale New Street na Kariakoo.
 
Kuna hotuba ya nyerere anadai kule bagamoyo alifanyiwa tambiko akawa anaruka shimo... je kwenye uislamu kitu hicho kipo? Na pili nikuulize hivi inaswihi kumuombea dua asie muislamu?
 
Vipi tambiko la Tambaza ambalo mwalimu mwenyewe alisimulia?
 
SAHIHI.

Ndiyo fasaha ya >ELIMU 3.0<.

 
Kama kawaida Mzee Said ukija na andiko basi una malengo yako fulani, na hapa ni kujaribu kupindisha ukweli wa mambo.

Unarejea kwenye hotuba ya Mwalimu wakati anawaaga Wazee wa Dar es Salaam lakini ni kama unaruka kwa alichosema.

Na niliwahi kuchangia hili kwenye moja ya nyuzi ulizowahi kuleta hapa jukwaani, haswa nikipingana nawe kung;ang'ana kutaja Wazee fulani tu huku Mwalimu alikuwa anawataja Wazee wa Dar Es Salaam kama Washiriki wakuu.

Na lengo la Mwalimu kuelezea yale ilikuwa ni kuonesha ni kwa jinsi gani alishirikiana na Wazee hao wa Dar Es Salaam na hata kulazimika kushiriki baadhi ya mambo yaliyokuwa magumu kwake...na alisema "mimi ni mkorofi kidogo kwenye mambo hayo.." na hapo zaidi alimaanisha mambo ya matambiko au "nguvu mbadala"...na sidhani kama alikuwa na tatizo sana na Dua kama zisingeambatana na matendo yasiyo rasmi.

Na kuna mfano mmoja alitowa kuwa kuna wakati alihisi kuumwa kichwa akaomba Aspro, akaambiwa asubiri...na baada ya kufuturu maumivu yaliisha...ndio akasema kumbe kichwa kilikuwa kinauma kwa sababu ya njaa...walikuwa kwenye mfungo...hivyo Dua pekee haikuwa tatizo....sasa kama kuna kuchanganya Dua na matambiko hilo ni shauri jingine.

Hivyo si kweli kwa unavyojaribu kusema kuwa hakukuwa na matambiko. Alilazimika kwenda Bagamoyo, sasa walifuata Dua huko? Wazee walichimba shimo wakachinja Beberu damu ikamwagikia shimoni wakamtaka Mwalimu aruke...akaruka Wazee wakamwambia "Twaining umekwisha"...hii ni Dua au tambiko?.

Ni si hakika kwa unavyojaribu kutaja idadi ya Dua ili hali hukuwepo kila alipoenda Mwalimu, ni hali ya kawaida tu kuamini ya kuwa kila Mtu au kikundi walijaribu kutekeleza imani kwa upande wao kuona malengo yanafikiwa.

Labda unataka kutofautisha waliokuwa wanatekeleza Dua na wale walitekeleza matambiko...vyovyote lakini hayo yote hayakuwa upande wa imani ya Mwalimu lakini alilazimika kushiriki ili aende sawa na Wazee.
 
May Day,
Najaribu kuliangalia hili suala la tambiko kwa upande wako na pia naliangalia suala hili kwa upande wangu kama Muislam.

Huwa tunafanya dua kisha yule anaefanya hiyo dua akasimama kwa mguu mmoja kaelekea kibla.

Anaweza mtu akatafsiri kitendo cha kusimama kwa mguu mmoja kuwa hilo ni tambiko.

Hapana neno iwe ni dua au tambiko wafanyaji ni walewale ambao walikuwa bega kwa bega na Mwalimu.

Lakini nataka nikueleze kitu katika hotuba ya Mwalimu Nyerere kuwa ina mambo ambayo hayakukaa sawa.

Mwalimu anasema anadhani Abdul Sykes alikuwa Secretary.

Mwalimu kwa miaka yote aliyoishi na Abdul Sykes hakumjua Abdul Sykes ni nani.

Mwalimu anasema mambo yalisinzia yeye ndiye alikuja kuyafufua.

Ukweli ni kuwa yeye alipochukua uongozi ndiyo TAA ikafifia.

Mwalimu kaeleza uchaguzi wa Arnautoglo lakini hakueleza alichaguliwaje na aligombea nafasi ile dhidi ya nani.

Mwalimu anazungumza kuhusu kuandika katiba.

Katiba ya TANU ilinakiliwa kutoka katiba ya CPP ya Kwame Nkrumah.

Mwalimu anasema safari yake ya kwanza ilikuwa Mbeya.

Safari yake ya kwanza ilikuwa Morogoro na aliongozana na Zuberi Mtemvu.

Hii hotuba ina mengi ambayo nadhani kwa kuwa miaka ilikuwa mingi imepita na hii kuwa historia ambayo haikupewa umuhimu na kuhifadhiwa Mwalimu kuna mengi amesahau.
 
Je inaswihi kumuombea dua kwa asie muislamu? Je inaswihi kumfanya kiongozi wenu asie muislamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…