Pamoja na juhudi nzuri za Makonda mimi bado nina shaka na umakini wa suala hili, mfano yeye kaletewa majina ama na vyombo vyake vya ulinzi au sijui watu wake anaowaamini, alitakiwa aipitie na kujiridhisha na hata kuhoji kuwa huyu Pilemoni mbowe ni nani? sasa ukibeba karatasi kama ilivyo ukaenda nayo katika vyombo ya habari ukatamka mbowe, kaka yangu na mbunge wa hai kwa hisia tu bila kujua mtu umtamkae unakuwa unaleta mchanganyiko, kwa sababu unatamka kitu tofauti na kilivyo andikwa ,hapa kinachoonekana watu wametuma majina kama yalivyoandikwa na unatakiwa utamke kama lilivyo, kama halijukani fanyia uchunguzi ubaini huyu ni nani kabla hujataja katika media, kwa hiyo utaona kabisa kuwa ni jitihada nzuri lakini zinaweza zisitoe matunda yeyote kama tutaingiza hisia/ushabiki /siasa/papara .