Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...



Mimi sijaona katika hayo maandishi Palipoandikwa Freeman Mbowe labda iwe ilitamkwa vibginevyo tuache mihemko. Hivi kila jina linaloishia na Mbowe itakuwa KUB??
 
Mzee wa Upako Gwajima tulisema muda mrefu sana kuwa huyu Kijana Anauza Unga. Mkatutukana sana humu .ohh we kahtaan Mdini a ohhh una mashetani.

Haya sasa. Upako na Dawa za kulevya. Halafu Wanakondoo wanampigia makofi eti anafufua wafu.!!
Huyu anafufua au anaua vijana wetu?
 
Well said, mkuu Mpanji. Kwanza ni kweli kwamba "emotions" zinaibuka kutokana na watu wanaoguswa. Na ni kutokana na ukweli huo, miongoni mwa ukweli mwingine, umakini unapaswa kuchukuliwa kuanzia mwanzo ili kuepuka suala la "character assassination" kuchukua nafasi. Kwa mfano, hivi mtu anayekuwa na taarifa zinazohusiana na biashara hiyo unaweza kumwita polisi kwa kumtaja jina lake ukimtaka aje kituo cha polisi kupitia "press conference"? Na kwa maelezo yako unakusudia kuonyesha kuwa ikionekana mtu huyo hana hizo taarifa au hahusiki anaachiwa huru!

Unaona mjadala hapa ulivyo, tayari majina yaliyotajwa yameishahukumiwa kuwa wanahusika na biashara ya madawa ya kulevya. Makonda atatumia nini kuondoa "hukumu" hiyo ambayo tayari watu hao wameishapewa? Je, haiwezekani kwamba Makonda anafanya "character asssassination" kwa sababu anajua kabisa kuwa hata kama watu hao hawatakuwa proven kuhusika au kuwa na taarifa, lakini tayari atakuwa "amewamaliza" kutokana na mtazamo wa jamii ulivyo?

Kumbe basi, kulikuwa na ulazima gani wa kuitisha "press conference" kutaja majina ili watu waje kituo cha polisi kuhojiwa, na sio vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi na kuchukua hatua? Nadhani hili la mwisho linaweza kuwa jibu la swali ulilomaliza nalo:..au imani imeanza kupungua maze..!
 
Eti tunawaita kuwasikiliza,
hamna kusikiliza kamata weka ndani ndo tutajua kweli hapo seriuosness,

hii list ya pili inatia matumaini kuliko ile ya akina wema,
tatizo sasa kwasababu waliotajwa wana pesa,eti wanaitwa kusikilizwa,ha ha ha ha.....
hawa hawatakaa ndani siku 4,ngoja tuone.
 
kusubiri hadi umkamate na ushahidi utakesha kwasabab wao sio wajinga hawabebi mzigo wao wanatuma watu wengine
Kwa hiyo mahakama za magufuli zitafunga watu bila vithibitisho kwa sababu kamtuma makonda awataje ujinga mkubwa
 
Hapo juu sijaona facts yeyote what i see u r too shallow in deep !!ungejua kama Narcoz wanatawala dunia kamwe usingechuliwa na upepo wa alietumwa kupiga zumari na hata kwenye account yake hana hata Mil 100 na ikiwekwa lazima apigiwe kelele
kwa uandishi huo sihitaji kujiuliza how deep you are!
utaonaje facts na kuandika tu unaweka "u r" ndio vidudu gani hivyo mnajifunza, bado tu upo unamjibu asiye level moja nawe, dalili ya uchovu wa akili
 
Namsubiri Mch.Gwajima atakavyoharisha maana kwa vyovyote vile lazima atajibu tu
Kama sio leo subiria kesho au jumapili kwenye ibada akiwa kwenye madhabahu
 
Umewahi kwenda billcana? Kama kuna wabunge wengi wa hai sawa bt kama yupo mmoja tulia na haimaniishi kuitwa ni kuwa muuza unga. Mbona kina TID Wametoka ingekuwa wanauza unadhani wangeitwa kistarabu hivyo. Yaan muuza unga umpe siku ya kuja kituoni si atatokomea na ushahidi, si kila kitu ni UKAWA. tupunguze mahaba
 
Je kweli hii imekaaje kisheria endapo wataweka wanasheria na wao wasipofika Central polisi kutakuwana hatia yoyote??
 
kusubiri hadi umkamate na ushahidi utakesha kwasabab wao sio wajinga hawabebi mzigo wao wanatuma watu wengine
Makonda anasolve tatizo amesema dar ikiwa salama Tanzania itakuwa salama ni approach tu hizi si lazima kuwakamata na kwa kifupi huwa mapapa hawakamatiki, niliwahi kusikia wanaonywa na kushauriwa kufanya Biashara zingine coz ni intercontinental business inahusu watu wengi sana wakubwa na wenye nguvu na hata vikundi vya waasi na majeshi ya baadhi ya nchi yanahusika so huwezi kueliminate bt unajaribu kuweka matuta angalia madereva wapunguze mwendo. Bt magari yataendelea kukimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…